Posts

Showing posts from October, 2019

SMS nzuri ya kumwambia mpenzi wako unampenda

Image
Ningependa nikuambie neno ambalo halina gharama na likutumiwa vibaya halina maana wala thamani. Neno hilo haliandikiki kwenye karatasi wala hata halitamkiki ila tu Linatokea Bila kujua na halina sababu. Neno hilo mi mwenyewe silijui ila ndo linatufanya tuwe pamoja Japo tupo Kasi Na Kusi.

Meseji nzuri ya kumtumia mpenzi umpendaye kwa moyo

Image
Katika nyuso za dunia, na kati ya miamba ya jangwani, Kuna SAUTI! Neno la pendo lako liotapo karibu yangu. Ni zaidi ya roho iendayo safarini.  

SMS ya kumtumia mpenzi wako kumtakia mahangaiko mema ya kazi

Image
  Ukipata tutakula na wala usijali mpenzi wangu. Ukikosa tutalala na hiyo itabaki siri yanguuuuuuuu.nakupenda mpz

Mahaba: Punguza Moto Wali Uive

Image
H ALOOOO eeeehhh shoga wanakwambia mjini raha jipe mwenyewe, hata kama mtu mzima nunua pampas kisha jikojolee, kwani bei gani! Unajifanya kuvaa viatu virefu wakati hata ndala ya msalani huna!  Shoga usiwe kama pipa lililokosa mfuniko maana kila taka itarushiwa humo! Unajifanya kulingia uzuri wakati kwa wanaume wanakukimbia kisa umbo la michelini, umbo lisilo na shepu! Heee heeeiyaaaa acha wenye uzuri wetu tulinge, wenzio tuna utamu wa kuku tunatafunwa hadi mifupa, upo nyonyo? Leo nipo na wewe mwanamke mwenzangu ambaye hujui harufu ya chumbani ipoje, ya sebuleni hadi ya nje.. wee kutwa kunuka moshi kama mchoma mkaa! Jamani ifike mahali basi tuwe tunabadilika, kuna vitu hadi unajiuliza huyu atakuwa amejitakia mwenyewe! Si unanijua tena mwenzako nilivyo, hakuna linalonipita bure! Umri unakwenda shoga, usipobadilika ukiwa kijana usitegemee kubadilika ukizeeka! Hivi huoni haya wenzako wakiwa na utamu wa samaki wanaliwa  hadi miba wakati wewe mwenyewe unakimbiwa kama gari

KUNA WATU, KUNA WAUAJI KWENYE MAPENZI,JIELIMISHE

Image
 NI Jumatatu nyingine tunakutana kwenye darasa letu. Hapa tunajifunza na kupeana misingi ya kuhusu masuala mbalimbali ya uhusiano na maisha kwa jumla Uhusiano mzuri ni ule ambao hausikii kelelekelele kila wakati. Hata ikitokea wametofautiana kauli kidogo, wanarekebisha na maisha yanaendelea. Dunia ya leo makelele ni mengi zaidi kuliko amani. Watu wanagombana zaidi kwenye uhusiano wa kimapenzi kuliko kuwa na wakati mzuri wa kufurahia maisha yao ya uhusiano. Ndugu zangu, mnapokuwa kwenye aina hii ya maisha ni hatari. Unapaswa kuishi ukiwa na amani ya moyo, mfurahie uwepo wenu hapa duniani vya kutosha huku mkijiandaa na kurudi kwake Muumba maana ukweli ni kwamba sisi sote tutakufa hivyo tujiandae pia na kifo. Kwenye masuala ya kusaka mwenza wa maisha, mara zote kumekuwa na changamoto sana kwani kwa vyovyote vile huwezi kumjua mtu moyoni mwake yukoje. Hujui anawaza nini, akikasirika anakuwaje au tabia zake zikoje. Ndiyo maana nasema kweli eneo hili lina changamoto sana.

Shoga usipojitambua utasema umerogwa!

Image
W ANAKWAMBIA nazi nazi tu hata ivunjwe uile haiwezi kuwa embe, upo nyonyo? Heee heeeiya nashanga unavaa mini msibani kwenye sherehe unavaa kanga hadi usoni, inahu?  Kama ulikuwa hujui jua sasa, unashangaa poda ina unga  inatoa harufu wakati unga wenyewe hadi uingie maji ndiyo utoe hiyo harufu! Haloooo eeeeehhh! Mji leo umekuwa wa baridi kama barafu linalochanganywa kwenye kapu la samaki! Leo nipo na wewe shoga yangu unayejifanya umeshajifunza kwa kungwi wako lakini kwangu ndiyo kwanza mvua za vuli zimeanza, upo? Shoga ukitaka kujua uchungu wa kitanda chaga ivunjike! Wapo walioolewa na wanaume wanaofanya kazi za kusafiri, pia wapo ambao waume zao hupendelea kusafiri pale wanapopata likizo ofisini kwao! Shosti, mumeo kama akisafiri andaa basi jinsi ya kumpokea ili ajue ulivyommisi, siyo anakuja anakutana na mambo yaleyale aliyoyaacha wakati anakwenda likizo. Ngoja nikung’ate sikio likuume kidogo shosti wangu! Kama mumeo kaenda likizo yake ya kiofisi na wewe ndiyo waka

UKIANGALIA MBELE UTAYAFURAHIA MAISHA YA UHUSIANO

Image
HELLO marafi ki! Naamini mtakuwa poa kabisa na maisha yanaendelea kwa kasi kama kawaida. Mimi kwa upande wangu ni mzima na ninaendelea na mishemishe zangu vema. Nakukaribisha sana kwenye ukurasa wetu wa Boyfriend & Girlfriend ambao naamini umekuwa msaada kwako kila kukicha. Marafi ki, maisha ni safari yenye mambo mengi sana njiani. Kuna wakati unaweza kukutana na vitu ambavyo huvipendi. Havikuvutii lakini inakubidi ujitahidi kukabiliana navyo kwa kila hali ili uweze kuvuka na kusogea kwenye hatua nyingine. Ndivyo maisha yalivyo, kila mmoja ana kumbukumbu mbaya katika maisha yake ambazo kwa hakika hapendi kuzikumbuka mara kwa mara. Kuna mambo yanayoumiza ambayo kwa kawaida binadamu wengi hawapendi kukumbuka machungu. Ndiyo maana binadamu mwenye utashi huyaacha yaliyopita yabaki nyuma na kusonga mbele, mambo ya nyuma yanabaki kuwa somo au daraja la kumfi kisha kwenye eneo jingine. Hayo ndiyo maisha. Marafi ki zangu, nimeamua kueleza yote hayo kama utangulizi ili iw

MLELA ANASWA NA MREMBO

Image
UTAWAAMBIA nini watu! Mwigizaji kunako kiwanda cha filamu Bongo, Yusuph Mlela amenaswa na mrembo mpya na baada ya kubanwa ameomba mpenzi wake wa sasa, Anastazia Exavery ‘Ebitoke’ amvumilie tu. Mlela alinaswa na mrembo huyo juzikati kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa staa wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel ambapo alipobanwa kama ni shemu mpya mjini, alisema ni rafiki yake tu. “Unajua Ebitoke asipojikaza atakuwa hajielewi kabisa kwa sababu nina marafiki wengi wa kike, hivyo ajikaze tu na akinifuatilia anaweza kujinyonga,” alisema Mlela.

Unaambiwa Hakuna Madhara Kisayansi Kujamiiana na Mwanamke Akiwa Hedhi

Image
Kisayansi hakuna madhara kujamiiana na mwanamke akiwa kwenye hedhi kwani kufika kileleni hupunguza maumivu na idadi ya siku za hedhi. Hii ni kwa sababu wakati mwanamke anapofika kileleni misuli ya nyumba ya uzazi hujikunja na hivyo tando laini (hedhi) hujinyofoa na kutiririka. Kwa wale wanawake wenye tatizo la kipanda uso (migraine) kinachojitokeza zaidi wakiwa kwenye hedhi hupata ahueni wakifanya tendo hilo kipindi hicho. Pamoja na kushiriki tendo hilo kuna faida hizo lakini kunaongeza hatari ya maambukizi kirahisi ikiwamo VVU, virusi vya homa ya ini na magonjwa yanayoenea kwa kujamiiana na kugusana na damu

Kajala afunguka kutoswa na Aunt, Uwoya

Image
BAADA ya kutoalikwa kwenye sherehe mbili za mastaa wenzake, Irene Uwoya na Aunt Ezekiel, muigizaji Kajala Masanja amesema kuwa haoni tatizo na hakuna kitu kilichopungua.  Akizungumza na Amani, Kajala amesema hawezi kujisikia vibaya au kuwa mnyonge kwa sababu hujaalikwa, kwani sherehe hizo zinaisha siku moja na kusahaulika lakini maisha yake yanaendelea. “Yaani hata nisipopewa mualiko wa kwenda kwenye pati zao, naona sawa maana wanafurahia siku moja tu, wanakuwa kwenye hali ya kawaida kwa hiyo hali hiyo hainiumizi hata kidogo,” alisema Kajala. Hivi karibuni, Kajala hakuonekana kwenye sherehe mbalimbali za mastaa wenzake ikiwemo bethidei ya Aunt na uzinduzi wa Reality Show ya Uwoya

Tatizo la kupoteza hamu na uwezo wa kushiriki tendo la ndoa!

Image
 HALI hii huwatokea wanaume na wanawake. Ni tatizo linaloathiri uwezo wa kisaikolojia na kimwili wa mtu yeyote aliye katika umri wa kuzaa. Tatizo hili kitaalam huitwa loss of libido au sex drive. Uwepo wa libido na sex drive katika kiwango kilicho bora, ndivyo humsukuma binadamu ashiriki tendo hili. Libido au sex drive hutofautiana kiwango kati ya mtu na mtu. Wapo wanaume au wanawake wenye kiwango kikubwa na wapo wenye kiwango kidogo na wenye kiwango cha wastani. Mwanaume mwenye kiwango kidogo cha libido au sex drive, uhisi amepungukiwa nguvu za kiume, kumbe yupo vizuri ila tatizo hana hamu na hisia. Hivyohivyo mwanamke mwenye kiwango kidogo, hulalamika kutokuwa na hamu, msisimko wala hisia za tendo. Watu wenye viwango vya juu vya libido au sex drive, awe mwanaume au mwanamke huwa hawatulii na hawatosheki, huangaika huku na kule kama ni mwanaume hutamani kila mwanamke anayemuona na kama ni mwanamke hivyohivyo kila mwanaume humuona anafaa. Ingawa ongezeko hilo wengi huliona

Amani ya moyo ni muhimu, itafute kwa gharama yoyote!

Image
WATU  wanateseka sana kwenye mahusiano kwa kuipoteza amani ya moyo. Wanaishi kwenye maugomvi, wanapoteza kabisa muelekeo kutokana na visa mbalimbali wanavyopitia kwenye mahusiano.   Unakuta mtu anaumia sababu yupo na mtu ambaye pengine anampenda sana, anaogopa kuchukua uamuzi wowote mbaya akifikiria kwamba moyo wake utateseka. Hapo ndipo kwenye kiini cha mada yangu ya leo. Migogoro katika mahusiano huwa ni jambo ambalo linarudisha nyuma sana. Kunapokuwa na migogoro kwenye mahusiano hamuwezi kusonga mbele, hata mafanikio ya kimaisha hamuwezi kuyapata sababu muda wa kufikiria vitu vya mafanikio haupo. Wakati ambao pengine mlipaswa kufurahi ili akili yenu iweze kupanga mambo, nyinyi mnaukosa huo utulivu. Kila mmoja wenu anakuwa amemkasirikia mwenzake, anawaza namna ya kujinasua kwenye migogoro hiyo anashindwa. Kushindwa kujinasua kwenye migogoro hii mara nyingi huwa kunatokana na kila mmoja kushikilia hoja yake na kujiona yupo sahihi na mwenzake ndiye mwenye makosa. Hivyo, hakuna a

Unakubalije Ndoa na ‘Chui’ Aliyeficha Makucha?

Image
N I  wiki nyingine tunakutana tena kupitia ukurasa huu nikiamini kwamba umzima, bukheri wa afya na unaendelea nyema na maisha yako kama kawaida.   Mimi niko poa kabisa tayari kukuletea mada nyingine ambayo naamini itakuwa ni yenye faida kubwa katika maisha yako ya kimapenzi. Mpenzi msomaji wangu, suala la kuoana si la kukurupuka, ni suala linalotakiwa kuchukua muda ambapo wawili waliotokea kupendana, hupata nafasi ya kuchunguzana katika mambo mbalimbali. Kabla ya kufikia hatua ya kuoana, ni lazima kwanza mtaanza kuwa marafiki wa kawaida. Kipindi hicho ndipo wewe utapata nafasi ya kubaini kama huyo uliye naye anastahili kuwa wako wa maisha. Mkishaona kwamba mmeridhiana kitabia, hapo mnaweza kuingia katika hatua ya uchumba na wakati huo penzi lenu halistahili kuwa la siri tena. Ndugu, jamaa na marafiki wanatakiwa kujua kwamba ninyi ni wanandoa watarajiwa! Elewa tu kwamba, kama utakutana na mtu kwa mara ya kwanza na akakueleza kwamba anataka kukuoa, atakuwa anakudanganya, na kama

Jinsi Vanessa na mpenzi wake mpya wanavyomtesa Jux

Image
Penzi linapokuwa maarufu inaleta raha, lakini shubiri ni pale ambapo wapenzi hao wanapofikia hatua ya kufarakana na kila mmoja kupita njia yake. Juz na Vanessa ni moja ya ”Couple” iliyokuwa maarufu na iliyopendwa na watu wengi, wawili hao walipogombana wengi walidhani Vanessa anaweza kuwa katika wakati mgumu kuliko Jux ambaye mapema aliweka wazi juu ya mahusiano yake mapya na mpenzi wake raia wa China aliyefahamika kwa jina la Nnayanka. Huku Vanessa akisikilizia mashambulizi ambayo Jux amekuwa akiyafanya katika mitandao ya kijamii akirusha picha mbalimbali zikimuonesha akiwa katika viwanja kadha wa kadha vya dunia akila raha na mpenzi wake huyo. Wawili hao ni kama wapo kwenye vita kali inayowafanya mashabiki wabaki midomo wazi na kuona pambano kama ngoma droo, kwani huku Jux na mchina, huku Vanessa na star wa Marekani, Rotimi  raia wa Nigeria ni mtangazaji lakini pia mcheza filamu Marekani, moja ya kazi yake kali ambayo amefanya vizuri ni tamthilia ya ”Power” ambayo alicheza ka

MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE

Image
Kama nilivyoelezea kwenye mada zilizopita, mchezo huu unatumika sana katika mapenzi ya sasa, watoto wa mjini wana usemi wao kwa kitu kilichovuma kuwa ‘ndiyo habari ya mjini’. Mchezo huu umekuwa ukipendwa sana na wanaume wengi ambao wengi wao huwa hawatumii kinga na kusababisha wengi kupata magonjwa ya zinaa pamoja na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU). Lakini mchezo wa kuruka ukuta umekuwa na madhara makubwa sana kwa wanaume wanaoufanya kwa muda mrefu. Tulipoangalia upande wa wanawake, tuliona sehemu kubwa ya wanaopenda mchezo huu ni wanaume ambao wengine wamebatizwa majina ya ‘basha’, wakimaanisha mwanaume mpenda kuruka ukuta bila kuangalia ni wa mwanaume mwenzake au wa mwanamke. Kwa vile nia ya kona hii ni kuelimisha madhara ya mtu kupenda kuruka ukuta ili aache mara moja, tunaendelea kutoa elimu ya bure ili mtu yakimkuta ajue yamempata kwa kiburi chake na kwa kupenda starehe ya kipuuzi. Madhara anayoyapata mwanaume anayependa mchezo huo ni kama ifuatavyo: 1.     Husababis

Meseji Nzuri za Mapenzi zitakazomfanya Mpenzi Wako Akupende zaidi

Image
Hutakiwi kwenda kwa waganga wa kienyeji ili kumfanya mpenzi wako akupende bali unahitaji mbwembwe ndogo ndogo ambazo zitamfanya mwenza wako huyo akupende zaidi. Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kumtumia meseji mwenza wako, mfano wa meseji hizo ni: 1. Moyo wangu umekupenda wewe peke yako, kamwe sifikirii kwenda kwa mwingine. I luv you honey… 2. Hata kama nitajidanganya kwamba sikupendi, moyo wangu umeganda kwako na hakuna dalili za kukuacha, wewe ni wangu peke yako dear… 3. Hata kama watasema mengi kiasi gani, kwako wewe nitaendelea kuwa mpole, maana nakupenda sana… 4. Siyo rahisi kuishi bila wewe, maana wewe maishani mwangu ni sawa na maji katika maisha ya binadamu. Mwaaaaa 5. Ni kweli nakiri ndani ya nafsi yangu kwamba nilikukosea mpenzi wangu, naomba unisamehe na unipe nafasi nyingine katika moyo wako mpenzi wangu. Nakupenda sana, pokea busu mwanana kutoka kwanngu….mwaaaaaaaa…

Kwanini Penzi la Mbali Linanoga Kuliko Penzi la Karibu

Image
  Wadau nimeona niwashirikishe hili jambo ili wale wataalam wa malavidav watupe utaalamu wao kwanini Penzi la Mbali huwa linanöga kuliko penzi la karibu nikiwa na maana kwamba; kama una mpenzi wako mnaishi umbali wa kuweza kusitisha shughuli zako japo kwa siku mfano arusha-dar ili muonane, hisia zake ni kubwa na kuheshimiana kunakuwepo sana kuliko yule wa pale mtaani? Wanandoa ambao hawakai pamoja wengi wao wanaheshimiana zaidi kuliko wale wanaoishi pamoja? Mkianzisha mahusiano katika hali yoyote kabla ya kuonana au kufahamiana mnaonyeshana lv sana, ila mkikutana tu hata kama ni sms mlikuwa mnatumiana zinapungua? Ni Theory gani inafaa kutumika hapa?