Posts

Showing posts from June, 2022

Meseji za Kumuomba Mpenzi wako Msamaha

Image
Kugombana katika mahusiano ya kimapenzi ni sehemu ya mahusiano hivyo inapotokea kwamba mmegombana, basi unatukaiwa kumtumia meseji zifutazo ili aweze kukusamehe: 1. Hivi kweli haya ndiyo mapenzi ama naota njozi? Nimefanya kila naloweza kuliimarisha letu penzi lakini naishia kuambulia majonzi, nimekuwa mtu wa kububujikwa na machozi kwa sababu ya lako penzi, kama nimekukosea tafadhali niwie radhi mpenzi, nakupenda na amini wewe pekee ndiye uliyetimiza ndoto yangu ya mapenzi. 2. Hivi ni kosa gani nilililokutendea ambalo sipaswi kusamehewa? Ni kweli nilikosea nahitaji kusamehewa mpenzi, plz naomba nielewe kwani sina mwingine zaidi yako wewe. Luv u 3. Nakiri kweli nimekukosea naomba wako msamaha kwa yote yaliyotokea hakika nimekukwaza. 4. Lakini kwa hakika hii ni mara yangu ya kwanza naamini,naamini utanisamehe laaziz na kunipa nafasi ya kulienzi lako penzi. 5. Unajua nakupenda ila tu umeamua kunitenda rudisha moyo nyuma kisha twende sambamba mapenzi yanavyokwenda. 6. Mapenzi ni usanii ukii

Sababu 5 Kwanini Wanawake Wenye Akili Nyingi Hupata Tabu ya Kupata Mapenzi ya Kweli

Image
Akili nyingi ni zawadi na laana. Wanapojiangalia kwenye kioo, wanawake wenye akili nyingi huona picha ya mtu mwenye nguvu mwenye malengo, anayejua anachotaka. Kuwa na akili nyingi ni kitu muhimu kuwa nacho, lakini wakati mwingine kinaweza kuwatisha wengine. Pengine ndio maana watu wenye akili nyingi hupata shida ya kupata pendo. Kama unajiuliza kwanini bado upo single, hizi ni sababu tano kwanini unaweza ukawa unapata shida kupendwa. 1. Unakuwa mchambuzi mno Wasichana wenye akili mara nyingi huchambua sana vitu. Huwa na shaka na kesho yao, njia nzuri za kuimarisha mahaba, na wanataka sana kumpata mtu sahihi. Hiki hata hivyo sio kitu kibaya. 2. Unajua ni bora kuwa peke yako kuliko kuwa na mwenza asiye sahihi Na hakuna tatizo katika hilo pia. Watu wenye akili wako makini katika kumpata mwenza sahihi ambapo wanaweza kuamua kubaki wenyewe kama asipopatikana. 3. Unajua kuwa mahusiano mara nyingi hufa Hawa hujua ukweli unaouma kuwa mahusiano mengi hayafiki popote. Matokeo yake, wakati mwingi

Huyu Mwanamke Ndio wa Kuoa ila Sijui Kama Anapatikana Tanzania.......

Image
1. Mpenzi wako akija kwako na akakakuta unakula ugali na kachumbari na akaamua kula nawe..huyo muoe.... 2.ukienda nae hotelini akaamua kuagiza ugali dagaa na maji tu...muoe anajua uchumi. 3.Mdada ambaye akimuona mkaka mwingine anaendesha Land cruiser na wewe una vitz yako Number A lakini akaamua kuja kwako...usimuache... 4.Mwanamke akikutembelea kwako akakuta nguo zako chafu akafua zote mpaka za wadogo zako, huyo mke usimuache! 5. Mwanamke unampa sh elfu tano akafanye shopping sokoni anakurudishia chenchi..huyo usimuache...anajua kubana bajeti na muaminifu. 6. Ukimpata mwanamke ambaye anakupigia simu na kukuuliza kama anaweza kukutumia credit au hela ya lunch, au anakupa pocket money saa nyingine, huyo tangaza ndoa fastaaa! 7.Mwanamke ambae anakupa password ya benki,laptop, simu na emails zake, huyo ni zaidi ya malaika.oa haraka..watamgombania wenzako! 8.Ukipata mwanamke ambaye mkipanda daldala analipa nauli au mkitoka out analipia bill ya chakula na vinywaji...huyo usimuache! anajua w

Hivi Kwanini Wanawake wa Kilokole Wengi Wana Roho Mbaya?

Image
Habarini wadau, Hili nina ushahidi nalo, wengi wao nimegundua wana roho mbaya kwakweli na nina mifano mingi tu. Yaani hao huwa wanaona kama watu wengine wasio walokole ni waovu tu. Niliwahi kushauriwa kuwa ni bora umuoe msichana aliyecharuka na kupitia starehe zote za dunia akatulia kuliko anayejiita mlokole namimi sasa naamini ule ushauri ni mzuri. Naamini wapo wanawake wacha Mungu kweli ila wapo neutral kama hawa waroman catholic na walutheri na huwa hawajikuti sana na kujiona watakatifu kama walokole. Mabinti wa kilokole mbona mpo hivyo? Au ni stresses za makanisani kwenu?

Tahadhari Kwa Wadada Mnaopenda Kuvaa Shanga Kiunoni...

Image
Bwana Yesu asifiwe!!! Wanawake wengi wanapenda kuvaa shanga kiunoni wakiamini zinawavutia wanaume wengi katika mapenzi. Napenda kutoa tahadhali kwa wanaopenda kuzivaa hasa kiunoni kuwa asilimia 80% ya shanga zinazouzwa zikiwa zimeshasokotwa zinatengenezwa na waganga WA kienyeji au watu ambao ni mawakala WA shetani na kuzinuizia mapepo kwa malengo yafuatayo: Kuharibu au kuiba nyota za watu Kuwafunga wanawake uzazi Kuwaunganisha na mtandao WA kuzimu Kuvuruga mfumo WA hedhi WA wanawake Kuwafanya wanawake kuwa makahaba, kwa sbb unatamani kukutana na wanaume wengi ili wakujue km unavaa shanga na unazitumia Kuwafunga kimafanikio Kuwafanya wasidumu kwny ndoa wanapoolewa. Kuwafanya wafikirie ngono zaidi. Sasa unaweza usinunue kwa mganga lakn aliyetengeneza ni mganga au agent WA shetani. Ww unaweza kununua kwa MTU na ukamwona WA kawaida, au yeye anaeuza yamkini hajui lakn alyetengeneza alikuwa na kusudi Unahitaji kuwa makini sana Dada zangu na vitu vinavyovaliwa sirini. Ni unaponunua ukazikombo

Nimeona Utupu wa Mke wa Mtu..Sasa Imekuwa tabu!! Ushauri

Image
Ilikuwa wiki moja iliyopita.Wakati wa asubuhi naingia bafuni kuoga kumbe kulikuwa na mke wa jirani yangu ambaye pengine hakusikia ujio wangu nami sikujua kama yumo. Ile anataka kutoka tu pale mlangoni,kanga yake ikaanguka na akabaki mtupu Macho hayana pazia niliona utupu wake nae aliona kuwa nimeona.Ile tu anajizoazoa kujisitiri akateleza akaanguka ikabidi nimsaidie kumuinua , nikamwinua huku akiwa uchi wa myama na kuhakikisha hajaumia popote ...then nikamfunika na kumwambia pole nikaondoka kiistaarabu. Ila sasa naona ustaarabu wangu uliniponza sasa naona ananifanyia vituko Mwanzo nilifikiri yameisha,alianza kwa kukwepesha macho na mimi,,mara akajenga mazoea na mimi.Na sasa vituko vimezidi,mara sms za ajab,wakati wote anataka kujua niko wapi na nafanya nini, siku ingine ananiletea chakula alichopika nile.. Kwa tabia na msimamo wangu naheshimu sana ndoa za watu. Nishaurini nifanye nini kumuepuka ? Nimepanga chumba hapa na nimelipa kodi ya mwaka mzima,ni jirani tu chumba cha nne toka kwa

Wanaume Wakimya Hawatabiriki Wanaposalitiwa Kimapenzi..Soma Hapa Jamaa Alichomfanyia Huyu Msichana

Image
Nilikutana na rafiki yangu Frank jijini Dar baada ya kua tumepoteana tangia tulipomaliza sekondari O Level na kila mmoja wetu akapangiwa mkoa tofauti kwa masomo ya A Level. Sasa hivi yeye ni muajiriwa wa taasisi moja nyeti ya fedha na huku akiwa na biashara zake kadhaa Tukawa na kawaida ya kuonana tunapopata nafasi na alipokua anakujua mitaa ninayokaa siku moja macho yake ya kaangukia kwa dada mmoja anaitwa Victoria. Kwa mwanaume uliyekamilika mara ya kwanza unapomuona Vicky huwezi kumuanagalia kwa mara moja lazima utamuangalia tena na tena! Itoshe kukwamambia Vicky alikua mzuri hasaa Nilifanya juhudi hafifu(minimum efforts) kumzuia Frank asianzishe mahusiano na Vicky maana namjua Vicky nae akinijua japo tulikua hatujazoeana na sababu kubwa ni kwamaba mambo ya kumkataza mtu asiingea kwenye mahusiano yalishawahi kunitokea puani na kuna uzi nilileta humu Mahusiano yao yalikolea haswaa na kwa muda mfupi Vicky akahamishwa na kupangishiwa nyumba sehemu nyingine, kukawa na safari za Nairobi,