Posts

Showing posts from April, 2020

KWENYE MAHUSIANO YAPO YA KUVUMILIANA LAKIN SIO HAYA

Image
Neno uvumilivu lisitumike vibaya kiasi cha kuharibu mfumo wako wa maisha.. Kuna mengine hayavumiliki zaidi ya mara moja.. Kuna tabia zenye kuumiza na kukera unapo vumilia unafuga ubovu. Ukiona mtu mpenzi au rafiiki yako havumiliki kwa tabia zake usiogope kukaa nae mbali.. Huwezi vumillia kupigwa au kutukanwa hadharani. Huwezi vumilia mpenzi kukusaliti zaidi ya mara mbili zote anasema shetani alimpitia tu..alimpitia waende wapi? Huwezi endelea kuvumilia mtu asiye kuheshimu wala kukusikiliza hata mambo ya msingi. Kumbuka, Siku zote anaye penda na kujali sana katika mahusiano ndiye anayeishia kuumia. Wanasema mwenye upendo wa dhati hana bahati...unaweza mpenda sana mtu naye akajua ila yeye atapuuza hisia zako na kwenda kwa mwingine au kukusumbua makusudi akiamin kuwa huwezi muacha. Anapo taka kuachana nawe kamwe usimlazimishe kamwe abaki kwako. Kuna wakati bado una mhitaj ila yeye ameamua kuachana nawe huenda ameona amempata bora zaidi yako au amechoshwa na tabia zako. Nikwambie k

MWANAUME EPUKA KUMWAMBIA MANENO HAYA MPENZI WAKO

Image
Wanaume wengi hudhani ni vigumu sana kuwafurahisha wanawake lakini si hivyo, ni jambo rahisi, matendo yako kwenye mambo madogo madogo ya kimapenzi na kuchunga ulimi wako vinaweza kumfanya mwanamke wako kuwa na furaha kupita kiasi na kama yeye akiwa na furaha basi ndugu yangu maisha yako yatakua na amani na wewe utakua na furaha. Kwa kawaida wanaume kuna vitu tunaviona vya kawaida sana na vya kipuuzi lakini kwa wanawake ni vitu muhimu na tunatakiwa kuwa makini tunapovizungumzia. Katika kukusaidia tu ndugu yangu katika mahusiano hapa nimekuandalia mambo matano ambayo unapaswa kuwa makini unapoyaongelea, hizi ni kauli tano ambazo mwanaume ni dhambi kabisa kumuambia mwanamke. 1. Hiyo Nguo imekutoa vizuri imefanya makalio yako yaonekane makubwa; Ingawa wanwake hupenda sana kusifiwa na kauli yako ilianza vizuri lakini umemalizia vibaya kumuambia ‘imefanya makalio yako yawe makubwa’ ni sawa na kumuambia umepigwa pasi na hata kama hatakujibu utamuumiza mbaya na kumuondolea kujiamini. S

Jinsi ya Kuwazuia Marafiki Wasingilie Mahusaiano Yenu ya Kimapenzi

Image
Sio mbaya kwa marafiki wa karibu au ndugu na jamaa kufahamu kushirikiana nanyi katika mapenzi yenu kama vile wakati wa sherehe au msiba. Pia sio mbaya kujuliana hali na kutambulisha mambo ya msingi yanayoendelea katika mahusiano yako wewe na mpenzi wako. Hata hivyo kuna wakati watu wengine wa pembeni, wawe majirani, ndugu, wazazi au marafiki wanaweza kuwa ‘sumu’ ya mahusiano yako, hasa pale unapowategemea sana kutoa msaada, maoni au maelekezo katika maisha yako ya mapenzi. Makala hii inaeleza mambo ya msingi unayoweza kufanya ili kupunguza uwezekano wa rafiki, ndugu, jamaa, au wazazi kuwa ‘sumu’ ya mapenzi yako. 1. Udhibiti wa taarifa kwa wengine Kadri unavyoelezea mahusiano yako kwa watu wengine ndivyo unavyowapa nafasi watu kutoa maoni, na hata kudhani kuwa wana dhamana ya kukuelekeza unavyotakiwa kuishi na mwenza wako. Hivyo basi, chukua muda wa kutosha kutafakari na kufanya uchunguzi kuhusu maswala yako ya mahusiano kabla haujaanza kutafuta maoni, ushauri kwa watu wengine.

Madhara Ya Kuchaguliwa Mwenzi Wa Kuishi Naye Katika Mahusiano Ndoa

Image
Mtanzania? Ni imani yangu kuwa uko salama rafiki na unaendelea vizuri katika harakati zako za kila siku kuhakikisha unapata kile unachokitaka kwenye maisha yako. Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya siku hii ya leo ameweza kutustahilisha tena kuiona siku hii ya leo. Kwa hiyo rafiki, tutumie muda huu wa leo vizuri kwani leo ni siku bora ambayo haitokuja tena kutokea katika maisha yetu hapa duniani. Mpendwa rafiki, napenda kukualika tena katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza kwa pamoja yale ambayo nimeweza kukuandalia siku hii ya leo. Hivyo basi, nakusihi ungana nami mwanzo hadi mwisho wa makala hii ili tuweze kusafiri wote kwa pamoja. Leo tutakwenda kujifunza juu ya madhara ya kuchaguliwa mwenza wa kuishi naye kwenye maisha ya mahusiano. Je ni madhara gani rafiki? Karibu rafiki tuweze kujifunza wote kwa pamoja. Katika moja ya matatizo yanayowasumbua watu duniani basi moja wapo ni mambo ya mahusiano. Mahusiano haya yanaweza kuwa mahusiano ya uchumba, mahusiano ya ndoa na nk.

Kumvumilia Mwanaume Asiyekupa Nipa Hela Nacho Kipaji....Mimi Nimeshindwa Walahi!

Image
Naitwa Fatuma Kutola Mwananyamala, kwa hili mimi sijui ila nikipata Mwanaume asiyenihonga sioni raha ya mapenzi hata kidogo, Yaani Mwanaume akinitongoza alafu akionekana hana mwelekeo wa kunipa hela simpi papucha, nasikia wadada wengine wanavumilia na wanaume wasiowapa hela eti sababu wazuri kisura sijui wanawaita Ben ten sikuhizi...yaani kwangu hata uwe mzuri kivipi bila hela ni Big Nooooooooooooo.......Yahitaji moyo aiseeee au nina kasoro?

Unamkataa Mtu Halafu Unamtangaza Chuo Kizima au Ofisi Yote Hadi Walinzi Wanajua

Image
Kuna watu wa ajabu sana, Anatokea mtu anaweza kuwa mwanamke au mwanaume kuomba mahusioni ya kimapenzi kwa mwingine. Sana sana kwenye jumuia mfano chuo,maofisini na ata kwenye viwanda mahali ambapo watu wanakutana mara kwa mara. Mtu amekutungoza umemkataa au amekukuta tayar una mtu unaishi nae kuna sababu gan kumtangaza kwa watu wote kua fulan nimemkataa. Kinachokufanya kila mtu kumwambie kua umekataa mtu fulani nini? Ili uonekana unatafutwa sana na watu au mzuri sana. Ukimkataa mtu na yeye akikuelewa basi hakuna sababu yakutangaza chuo kizima au ofisi yote adi walinzi wajue. Wenye tabia hii acheni Mara moja.

Ukijaliwa Kuwa Msichana Mzuri na Mrembo Usidhani Kamwe Utatetemesha Kila Mwanaume

Image
Ukijaliwa kuwa Msichana mzuri na mrembo,usidhani utatetemesha kila Mwanaume, kuna wanaume na akili zao kichwani,urembo wako hauwasumbui kama bichwa lako ni kanyaboya,uzuri wako hausaidii kitu,na utashangaa no one is paying attention,watu utakaowapata ni walewale kanyaboya wenzako, na hawana futuretabaki unaliwa bure kila siku unatoa macho. Ukipata mwanaume anakupenda unaanza drama zako na kupiga watu danadana,madai yako hujali na unadhani hata akiondoka utapata mwingine kisa wewe ni mzuri, la hasha Mwanaume akijitoa mhanga kukupenda kwa uzuri wako mheshimu,maana viumbe wa kike wakiwa wazuri ni shida na matatizo hakuna mtu anataka,sasa ukimwongezea na drama pamoja na yeye kujigeuza mpalestina kwako utajikuta umeolewa na kioo cha chumbani kwako,maana hicho ndo kinakudanganya sana kwamba we ni mrembo. Watch out drama zina mwisho, leo unacheza na mioyo ya watu unajiona we kifaa usidhani wanaume hawaumii, tunaumia sema hatusemi tu,machozi yetu kama ya samaki.

JINSI YA KUEPUKA UTUMWA WA MAPENZI

Image
Rafiki zangu, uwanja wa mapenzi ni mpana sana, wakati mwingine unatakiwa kutumia akili na uwezo wako wa mwisho wa kufikiri ili uweze kung’amua ufanyacho kama ni sahihi au lah! Lakini kama unataka mambo yako yakuendee vizuri zaidi na zaidi na uache kujuta, lazima umshirikishe Mungu. Mweke yeye namba moja katika uhusiano wako, mweke mpenzi wako mikononi mwake na mwisho wa siku utaona mafanikio yake. Machozi yako hayatamwagika tena ikiwa utamtanguliza yeye. Wengine hujisahau mapema, wanajiona wanaweza kila kitu bila msaada wa Mungu, nani amekudanganya? Usijidanganye ndugu yangu, wengi ambao wanamtumainia Mungu mambo yao huwanyookea. Katika mapenzi kuna aina nyingi za uhusiano, wengine huwa na mtu kwa muda mfupi wakati wapo ambao wanatamani sana kuishi na wenza wao baada ya kuwa katika uhusiano wa kawaida. Inapendeza sana kama wote mtakuwa mnawaza katika umoja, yaani lililopo kichwani mwako ndilo lililomo kichwani mwa mpenzi wako, vinginevyo lazima mmoja wenu atalia! Unapokuwa kati

MWANAUME UNAPASWA KUKUMBUKA HILI KATIKA MAHUSIANO YAKO

Image
Mwanaume acha ubahiri kwa sababu ni maagizo ya Mungu mwenyewe. In fact ni furaha ya mwanamke yeyote yule kuwa na mwanaume anaeweza kumhudumia mahitaji yake licha ya mwanamke nae kujikwamua kiuchumi kama ziada na nyongeza tu lakini sio wajibu wake. Mwanaume Mungu anapokubariki na kipato sio vibaya ukamfanyia vitu vizuri mwanamke wako anataka manicure au pedicure. Mpe fedha akaweke mwili katika mwonekano bomba! Mfanyie hata suprise ya shopping mara moja moja. Tuache ubahili, tusihonge pembeni tutafilisika, vichenchede vya nje huwa vinakamua mpaka unabaki na sharubu tu! tujifunze kuwahonga wake zetu! Anataka vacation, peleka Ngorongoro huko huyo baby wako akashangae tembo. Anataka kula vitu vizuri, give her the treat. Kazi yako kama mwanaume ni kuhakikisha mwanamke wako anaridhika na anafurahia uwepo wako. Kila mwanamke ni mzuri, inategemeana na wewe utakavyompa kipaumbele! Mwanamke nae asibweteke, Mumewe anaporudi nyumbani huku akiwa na furaha ya kufanikisha dili kadhaa au huzuni

NIFANYE NIN ILI NIACHE TABIA YA KUPENDA MAJIMAMA??

Image
Mimi ni kijana wa Miaka 21 , Na umri wangu huu mdogo lakini nimesha experience vitu vingi katika mapenzi...mwanamke wangu wa kwanza alikuwa na miaka 41 mimi nikiwa namiaka 19, toka kipindi hicho mimi nimekuwa nikipenda wanawake wazima wenye umri mkubwa...na cha ajabu kila nikiwatongoza wanakubali wengi wao ni wake za watu ... Madhara ya Kufanya Mapenzi Kipindi cha Hedhi Sasa imenikaa akilini nikimpata msichana mdogo siridhiki kabisa na mwishowe namuacha natafuta Mwanamke aliye nizidi umri...Tatizo wengi wao wameolewa sasa tunafurahishana tu alafu wanawahi kwa wanaume wao..Naombeni ushauri.. Je nifanyenje hizi feelings za kupenda majimama ziiishe?

MADHARA YA KUFANYA MAPENZI KIPINDI CHA HEDHI

Image
Kuhusu kujamiiana wakati wa hedhi; medically hakuna madhara yeyote yaliyothibitishwa kiafya kutokea kutokana na mtu/watu kujamiiana wakati wa hedhi, ISIPOKUWA zipo hatari zinazojulikana, nazo ni urahisi wa kuambukizwa magonjwa ya zinaa, ukiwemao UKIMWI japo vitabu vya dini kama biblia inakataza kujamiana wakati wa hedhi. Cha msingi,unapotaka kufanya tendo hili wakati wa hedhi, ni vema ukashirikiana na mtu unayefahamu hali yake kiafya, preferably mkeo/mwenza wako muaminifu(aliyepima?), na kabla ya tendo ni vizuri akanawa vizuri hii itapunguza uwezekanao wa ku soil bed sheets na damu (but the good news ni; damu ya hedhi haigandi na haiwezi kuweka permanent stains kwenye shuka, sabuni kidogo, imetoka!) Pia wataalamu wenaongeza kuwa, wakati wa hedhi wanawake wengi hupata raha zaidi kuliko kipindi kingine, pengine kwa kuwa huwa relaxed, na bila hofu ya kupata mimba Kitaalam wanasema hakuna madhara ya kitabibu zaidi ya STDs. Wengine wanasema inasaidia ku-relieve cramps

ULIMBUKENI WA WANAUME LINAPOKUJA SUALA LA MAPENZI NA UZURI WA MWANAMKE

Image
Leo inabidi tuambiane ukweli, kuna baadhi ya wanaume ambao sijui ndo tuite "nzi kufia kwenye kidonda" yani utakuta mwanaume anamfukuzia mwanamke kwa miaka 3, kisa ni nini? eti oh yule demu ni mzuri, oh i have a crush on her, ooh nimemzimia..utakuta huyo mwanamke anaefukuziwa wala hamuwazi huyo mwanaume tena usiku analala usingizi mnono na vijambo juu. Mtu anakaa kwenye relationship isiomfaidisha wala kumpa furaha eti kisa demu ni mzuri, aise i advise ni bora kuwa single tu kuliko kupitia haya mateso ya kujitakia, sisemi mtu usiwe na crush kwa demu, ila wanaume (including me) tuwe tunajaribu kusoma upepo, mpende demu ukiona haeleweki na hakutilii maanani.. sepa fasta it will be good for ur emotional health, naamini ukitubu dhambi kiukweli na ukimuomba Mungu atakupa mke mwema. Some of my friends wanaapa kutumia hela nyingi sana kwa demu wanaemuona kuwa ni mzuri, they're like yule demu bwana ni high status ngoja ntamchukua na prado, kumbe huyo demu anapigwa mate na muu

HIVI NI KWELI WANAWAKE WALIOAJIRIWA HUJITONGOZESHA KWA MABOSS WAO??

Image
Kuna dhana kwamba wanawake walioajiriwa wanakabiliwa na mazingira ambayo yanawalazimisha kuingia kwenye vitendo vya kutoka nje ya ndoa zao, ukilinganisha na wanawake ambao hawajaajiriwa hususani mama wa nyumbani jambo ambalo katika maisha ya kawaida bila utafiti linaonekana kama vile ni kinyume yaani akina mama walio majumbani ndio ambao hutoka nje zaidi. Niliwahi kuwahoji wanawake kadhaa jijini Dar, mwanamke mmoja kati ya watano alikiri kwamba yuko tayari kujitongozesha kwa bosi ili kujaribu kulinda nafasi yake kazini au kupandishwa cheo. Nilifanya mahojiano hayo ili kujua idadi wanaume wanaotumia nafasi zao kazini kuwadhalilisha wanawake kijinsia. Lakini bila shaka suala la mapenzi kwa wanawake walioajiriwa lina nguvu na kwa hiyo limekuwa likifanyiwa tafiti katika sehemu mbalimbali duniani. Tofauti na tafiti ambazo zimefanywa hivi karibuni zinaonyesha kwamba mwanamke mmoja kati ya kumi walioajiriwa huwa anaonyesha tabia za kimapenzi au kujitongozesha kwa bosi wake. Kim Jong

MWANAMKE UKIFAULU HILI, NDOA YAKO ITADUMU

Image
Moja kati ya vitu vinavyowavutia wanaume kwa wake zao ni mapishi. Mke ukiweza kumteka mumeo katika suala la mapishi, mumeo hatokuwa na sababu ya kutokula chakula unachokipika, lakini pia atakauwa mwenye kujitahidi kurudi nyumbani mapema kuja kula chakula kitamu kilichopikwa na mkewe. Mke unapokuwa upo jikoni unaandaa chakula, ni lazima ujue kuwa atakaekula chakula hicho ni mumeo, hivyo ni vizuri ukatumia ujuzi wako wote kuhakikisha mumeo anakula chakula kizuri. Wanawake wengi wanakawaida ya kupika chakula kizuri siku za sikukuu, hapo ndio anajitahidi kutumia uelewa wake wote katika kupika ili tu aonekane na majirani na si mumewe, au siku akisikia mume anakuja na mgeni au rafki yake ndio unataka upike vizuri, hilo si jambo jema. Jitahidi kumpikia mumeo kila siku chakula kizuri, mvutie mumeo kwa chakula chako, mfanye kila anapopata muda wa mapumziko kazini arudi nyumbani kula. Utundu wa mwanamke unaanzia jikoni

JINSI YA KUEPUKA UTUMWA WA MAPENZI

Image
Rafiki zangu, uwanja wa mapenzi ni mpana sana, wakati mwingine unatakiwa kutumia akili na uwezo wako wa mwisho wa kufikiri ili uweze kung’amua ufanyacho kama ni sahihi au lah! Lakini kama unataka mambo yako yakuendee vizuri zaidi na zaidi na uache kujuta, lazima umshirikishe Mungu. Mweke yeye namba moja katika uhusiano wako, mweke mpenzi wako mikononi mwake na mwisho wa siku utaona mafanikio yake. Machozi yako hayatamwagika tena ikiwa utamtanguliza yeye. Wengine hujisahau mapema, wanajiona wanaweza kila kitu bila msaada wa Mungu, nani amekudanganya? Usijidanganye ndugu yangu, wengi ambao wanamtumainia Mungu mambo yao huwanyookea. Katika mapenzi kuna aina nyingi za uhusiano, wengine huwa na mtu kwa muda mfupi wakati wapo ambao wanatamani sana kuishi na wenza wao baada ya kuwa katika uhusiano wa kawaida. Inapendeza sana kama wote mtakuwa mnawaza katika umoja, yaani lililopo kichwani mwako ndilo lililomo kichwani mwa mpenzi wako, vinginevyo lazima mmoja wenu atalia! Unapokuwa kati