Posts

Showing posts from January, 2020

MWIMBAJI HUYU ATANGAZA KUPUNGUZA MAKALIO YAKE KWA SABABU YA MAPENZI

Image
Pichani Queen Haizel mwimbaji wa Ghana katika interview mpya amewaacha watu midomo wazi kwa kufunguka kuwa kuanzia sasa muda wowote ataziteketeza sehemu zake nyeti ili asahau kabisa issue za mapenzi kusudi ajikite vizuri Kwenye kazi zake za muziki akidai zimekuwa kikwazo kwa maendeleo yake. Amesema ataenda nje ya nchi kwa miezi miwili kufikia lengo hilo la kuzikata

USITAFSIRI VIBAYA HURUMA YA MWANAMKE KAMA UDHAIFU WAKE

Image
Hii ni kwa ajili ya wanaume wote ambao wamekuwa na tabia ya kudharau pale mwanamke anapumuonesha huruma na upole. Mwanamke akipenda kweli yu-radhi kukufanyia lolote lile! Atakuvumilia kwa kila hali, inabidi kutambua huruma na upendo wake ili kumtia nguvu. Atapokupa dhati ya upole na huruma yake kisha wewe ukamlipa dharau na kuona umemuweka kiganjani,basi huruma hiyo hufika ukomo. Moyo wa mwanamke ukiamua kukatia tamaa basi tambua hakuna kitu waweza fanya ukamrejesha katika hali yake ya awali. Thamini jitihada za mwenzi wako anazokuonesha, zichukulie kwa uzito usije ukawa wewe ndiye sababu ya kuona kuwa hafai na hajitoshelezi

JIFUNZE KUMMISS MPENZI WAKO, INASAIDIA SANA

Image
Ni lazima uipe pumzi penzi lenu kama mnafanya kazi ambayo inawafanya wewe na mke wako kuwa pamoja kila wakati, basi kila mmoja anahitaji muda wa peke yake awe na muda wa kummiss mwenzake. Huwezi kummiss mtu ambaye kila dakika unamuona, sana sana utaishia kuona mapungufu yake na kugombana tu. Utammiss vipi wakati kila wakati uko naye, kila mmoja anahitaji kummiss mwenza wake ili mapenzi yawe na raha. Mume/mke wako anahitaji maisha mbali na wewe, anahitaji angalau nusu saa kwa siku ambayo hataona sura yako, atakuwa na watu wengine, atakuwa na marafiki au atakuwa anafanya kitu kingine bila wewe. Kama uko kwenye ndoa au mahusiano ambayo kila kitu mnafanya pamoja, kila wakati mko pamoja, kila muda wa ziada mko pamoja basi suala la kugombana kwenu ni la muda tu. Jifunze kuwa na furaha nje ya mwenza wako, si kuchepuka hapana, hata kucheza tu karata na majirani inatosha kukufanya ummiss mwenza wako. Kama kila wakati mko pamoja, hata kama hamfanyi kazi pamoja lakini kama ule muda wa z

Ujumbe wa kimahaba kumwambia mpenzi wako kuwa mnafiti kuwa pamoja

Image
Mvua na jua haviwezi kuwa pamoja, usiku na mchana hazigongani, lakini mimi na wewe, hata wasemaje, ‘tunafiti’ kuwa pamoja.

Ujumbe wa mahaba wa kumwambia mpenzi wako penzi lake ni tamu sana

Image
utamu wa penzi hunogeshwa na pendo la dhati pia utamu wa penzi ni uwepo wangu na wako,ladha yake ni zaidi ya nazi kwenye wali au royco kwenye mchuzi au pilipili kwenye kachumbari, utamu wake ni zaidi ya asali au jam kwenye mkate ,blueband kwenye uji.penzi tamu halina kifani

SMS nzuriiii ya kumpa mtu hai

Image
Nakupa HAI, kwa sababu uko HAI, usingekuwa HAI, ni vigumu kupewa HAI, basi nawe wape HAI, walio HAI, maana ni bahati kuwa HAI, wengi walitamani kuwa HAI, lakini wamepoteza UHAI, Usione najidai, ila mimi naringia UHAI, Haya basi pokea HAI, ili moyo wako ufurahi. HAIIIIIIIIIIIII!!!

SMS nzuri ya kumuomba mtu muwe wapenzi

Image
Ama baada ya salamu, mimi ni mzima wa afya njema. Mie ni ndege nipo angani na nimetafuta mti wa kutua kila pembe ya dunia lakini sijaupata bado. Je naweza nikatua kwako?

SMS ya kumuonyesha mpenzi wako unavyompenda

Image
natamani usaini moyoni mwang,ikiwezekana pia upige muhuri moyoni mwangu wajue nan mmiliki wa huo moyo wenye shibe upendo kwaajili yako mpenzi

SMS ya mapenzi kutakia maisha marefu siku ya kuzaliwa au birthday

Image
Happy birthday mpenzi, nakuombea kwa mwenyezi akupe maisha marefu na kukuepusha na maradhi, pongezi kwa wako wazazi kwa kukuzaa mpenzi, nakupenda la azizi.

HIKI NDO KINACHOSABABISHA USIOLEWE MPAKA LEO

Image
Mwanamke kutwa unalalamika wanaume waongo kwenye mapenzi wakikutumia tu wanasepa, huna hata akili ya kufikilia kwann kwako wagonge wasepe hawaingii ndani? Na daily unahudhuria harusi za wasichana wenzio wakiolewa? Au wao wanaolewa na majini eti? Hii dhana kujiona watoto wa mjini, wanawake wa kisasa sijui, basi ndo mnakuwa kama makuku ya kisasa kweli hamfai kwa kufugwa shida tupu!! Maana makuku ya kisasa ukitaka kuyafuga basi ujipange kweli kweli kuanzia mtaji wa kipesa hadi muda wa kuyahudumia!! Ndo nyie sasa, yaani kiukweli wanawake wa sikuhizi hata radha mmeisha kabisa  We unataka mwanaume akuoe wakati hujawahi kujiongeza hata kusema umfulie, kazi kumsifia kapendeza hujui hata anafuliwa na nani? Hujawahi hata kumpikia kazi kumsifia ananenepa hujui hata anakula wapi, halafu unataka ndoa? kila siku ukienda gheto kwake we kazi kuulizia series za kikorea kama kaleta mpya, huulizi hata Leo unanunua mboga gani nije kukupikia, mwanamke mzima bila haya unaenda kwa bwana wako unafika

JE? UNATAKA KUWA BABA BORA? BASI UNATAKIWA KUFANYA HAYA

Image
Baba alirudi nyumbani na kumkuta mkewe jikoni, akamkombatia, akamtazama sana mkewe na kumbusu kwenye lips, wakasalimiana na mkewe akampokea na kwenda nae chumbani kisha kurudi jikoni ili kumalizia kupika. Ilipofika wakati wa kula, mume alikaribishwa mezani na mkewe, pamoja na watoto. Chakula kikapakuliwa na kila mmoja kuanza kula, ghafla watoto wakaguna "MMMH". Baba anapata shauku ya kutaka kujua kilichopo ndani ya chakula, akaonja na kugundua maharage yalikuwa yameungua hivyo kutoleta radha nzuri. .. Mama akajisikia vibaya sababu alijua kilichofanya watoto wagune, akamtizama mumewe huku akisubiria kuona kile ambacho mumewe angesema, hofu ilimjaa. Mume akamtizama mkewe na kugundua wasiwasi alionao mkewe, akageukia sahani yake na kuanza kula, akamaliza sahani, akavuta hotpot na kuongeza chakula tena na kuweka maharage mengi zaidi ya mwanzo. Alipomaliza akamtizama mkewe na kumuambia "Mke wangu asante kwa chakula, umenitibu njaa yangu kipenzi''. Watoto wakam

FAHAMU KIASI CHAMAJI UNACHOPASWA KUNYWA KULINGANA NA UZITO WAKO

Image
Ni kiasi gani cha maji unakunywa kwa siku na unakunywa wakati gan! Kama tunavyojua kuwa maji ni uhai, maji yakinywewa kwa nidhamu na kuzingatia uzito mtu alionao tunaweza kukwepa zaidi ya asilimia sitini (60%) ya maradhi mbalimbali. Muda gani sahihi wa kunywa maji! Mara tu unapoamka asubuhi. Nusu saa au dk 45 kabla ya muda wa chakula  cha mchana au cha jioni. Na muda uliobaki kunywa kiasi kwa kipindi fulani cha muda. Yanywe maji ukiwa umekaa na kunywa kidogo kidogo. Muda gani usinywe maji! Usinywe maji wakati au mara tu baada ya kula. Ijulikane kuwa maji na chakula ni vitu viwili tofauti ambavyo mwili unahitaji lakini sio kwa mkupuo. Ukifanya hivyo maji yanaharibu baadhi ya virutubisho vilivyopo kwenye chakula. Usinywe maji mengi kwa wakati mmoja ili kufikia kiwango kinachohitajika kwa siku. Hakikisha inapofika saa 12 jioni uwe umeshafikia kiwango chako cha mwisho, usinywe maji zaidi ya muda huo yatakuharibia usingizi usiku. Kiasi gani cha maji ninywe kwa siku kulingana na uzit

MANENO UNAYOPASWA KUMWAMBIA MPENZI WAKO ILI KUONGEZA LADHA YA MAHUSIANO

Image
Mapenzi yanayotawaliwa na maneno matamu hunawiri na kuchanua kama mmea uliopandwa kando ya mto. Hakika maneno mazuri husadifu mambo mengi mazuri baina yenu ikiwemo upendo, kujali, kuthamini, heshima, utii, upole, nidhamu, uaminifu, unyenyekevu, usikivu, ukarimu na faraja hivyo ni vema kuhakikisha kama kweli unampenda kinywa chako daima kimtolee lugha nzuri ya maneno matamu. Weka desturi ya kusema mambo haya kwa mwenza wako hakika inazidisha furaha na amani kati yenu.. Nakupenda Nakupenda ni kitu rahisi na cha wazi cha kumwambia mwenza wako. Hakikisha tu kuwa unamaanisha. Jaribu kulisema neno hilo pindi mwenza wako anapokuchekesha au pale anapofanya kitu kinachokukumbusha kwanini mko pamoja.....``` Umependeza Kama umekuwa kwenye ndoa kwa muda mrefu, ni rahisi kujisahau katika mengi. Ni muhimu kumkumbusha mwenza wako kuwa anakuvutia. Kumjulisha kuwa ulivo vaa umependeza sana’ kutamfanya ajisikie vizuri na kukumbusha kwanini ulimchagua yeye. Samahani Kila mtu hukosea wakati fulani

Ni kweli mapenzi yana maumivu makali lakini unaweza kuyasahau

Image
Ni wiki nyingine mpenzi msomaji wa safu hii tunakutana tena jamvini hapa kwa neema na rehema za Mwenyezi Mungu. Leo tunaangalia ni kwa namna gani mapenzi yanaweza kuwa sumu kali inayosambaa kwa haraka sana katika miili ya wanadamu wa jinsia zote. Ni kweli kwamba, mapenzi yanatesa kuliko kitu chochote katika uso wa dunia hii. Ni mapenzi hayohayo ambayo yana nguvu na maumivu makali kuliko maumivu ya kitu chochote unachokijua chenye kusababisha maumivu. Pia ni kweli wapo watu wengi wameumizwa na kuteswa na mapenzi. Wengine wanaendelea kuteseka na kuumia kila siku. Wengine wanatamani kuyaepuka ingawa hawawezi zaidi ya kupumzika kwa muda. Wapo wanaotamani kuyakimbia ila hayakimbiliki. Wengine wanatamani kujiua ila roho wa Mungu anawashindia. Inawezekana ni kweli mpenzi wako amekuumiza sana lakini vumilia kwani maumivu hayo ni ya muda na ninaamini ipo siku utayasahau. Maumivu unayoyapata kwa sababu ya mke, mpenzi, mchumba au mume wako ni ya mpito tu, ni kama masika na kiangazi kinavy

Sababu 7 za baadhi ya wanaume kukimbiwa na wanawake

Image
Imezoeleka katika jamii kwamba wanaume hukimbiwa na wanawake kwa kukosa kipato au alichonacho ni kidogo, au muonekano na maumbile ya mwanaume bila kuzingatia kwamba wanawake huangalia vitu vingine zaidi ili kugundua kama wanaweza kuishi na aina hiyo ya mwanaume. Zifuatazo ni sababu 7 zinazowafanya wanawake wakimbie mahusiano na wanaume wenye tabia hizi:- 1.Kulazimishwa au kusukumwa kwenye maamuzi. Wanawake hupenda mwanaume mwenye msimamo wake na mwenye kufanya maamuzi na kusaidia wenzie wanapohitahi msaada kutoka kwake pamoja nayeye mwenyewe bila shinikizo kutoka kwa yeyote. Usisukumwe sukumwe hovyo hata kama ikiwa na mama yako hili huonyesha udhaifu. 2. Ulevi wa kupindukia. Sawa, Unywaji wa pombe haujawahi kupingwa ila endapo mwanaume ni mnywaji kupindukia kiasi anaweza akalala hata baa, akaazisha ugomvi au kuzima kabisa haipendezi. Hakuna kitu wanawake wanachukia kama mwanaume asiwejiweza anapokunywa pombe. 3. Matusi na lugha chafu. Inawezekana wote

Aina 8 za watu ambazo ni sumu unatakiwa kuwaepuka maishani mwako

Image
Watu wasiofaa wapo kila mahali, kwa hakika wanakwaza na kurudisha maendeleo ya watu nyuma. Ukiwa kama mjasiriamali au mtu mwingine yeyote unatakiwa kufanya bidii kufikia malengo yako bila kuruhusu aina za watu wasiofaa kukuvuruga. Inawezekana unawafahamu watu ambao ni sumu; yawezekana wanafanya kazi na wewe, ni marafiki zako au unaishi nao. Kadri unavyowaepuka katika maisha au kazi yako ndivyo mambo yatakavyozidi kuwa mazuri. Fuatana nami katika makala hii nikushirikishe aina 8 za watu ambazo ni sumu unazotakiwa kuziepuka katika maisha yako. 1. Watu wanaohoji kila kitu Watu wanaohoji kila kitu hutafuta njia ya kupinga na kukosoa kila unachokifanya. Utatumia muda mwingi kuwaelewesha lakini watasikia kwa sikio moja na swala hilo kutokea sikio la pili. Kujaribu kutafuta msaada na ushauri kutoka kwa watu wa aina hii ni kupoteza muda. Watu hawa huwa na maswali kama vile kwanini unafanya hivi? Unapoteza muda; si jambo zuri; la fulani liliharibika; nani kakuambia ufanye; nitapata nini

Tuambizane tu ukweli ili tupate kilicho bora katika mahusiano ya kimapenzi

Image
Kwenye swala zima la mahusiano ya mapenzi pesa haina chochote cha kuthibitisha. Na anayetanguliza pesa mbele katika mapenzi hana upendo wala mapenzi ya kweli. Wanawake Usikimbilie kumpima imani mpenzi wako kwa kumuomba pesa ili ujue kama anakupenda au laa mwanaume ni kiumbe anayeweza kufanya kila unachotaka akamilishe malengo yake. Be careful utachezewa na utatumika sana lakini kumpata wa kuishi naye forever hutapata. Wanaume Kumpatia pesa mpenzi wako kila akihitaji hakumfanyi yeye akuone ni kiasi gani unampenda ila huenda ukageuzwa kitega uchumi chake. Lugha ya mjini tunaita atm yake. Unampomuapproach mwanamke epuka kumuonyesha maisha ambayo siyo level zako maana kama utampa pesa sana kabla ya kumuoa jiandae kufanya hivyo baada ya ndoa Ukishindwa black brother huna ndoa tena, Wahenga wanasema "mtoto umleavyo ndivyo akuavyo" Nyote Epuka kuweka mbele katika mahusiano vitu ambayo vinaisha na kupotea kabisa kama pesa, mali na mengine mengi maana yakiisha hayo yatatengene