Posts

Showing posts from October, 2018

Kuna changamoto na athari kubwa sana ukioa mwanamke mzuri

Image
AWALI ya yote naomba niseme kwamba, raha ya ndoa ni kumpata mtu ambaye anajua maisha na anajua mapenzi pia. Ukipata mwanamke ambaye anajua kutafuta pesa tu lakini kwenye ulimwengu wa mapenzi ni limbukeni, atakusumbua sana. Lakini pia ukijichanganya ukaoa mwanamke ambaye ni mtaalam wa mapenzi lakini hajui pesa inavyotafutwa, nalo ni tatizo licha ya kwamba kwa wengine si tatizo kwani wapo ambao hawataki kuoa wanawake wenye vipato kutokana na yale yanayosemwa kuwa, baadhi yao wakijua kutafuta pesa, wanakuwa viburi. Hata hivyo, kwa wanaume wanapofikia muda wa kuoa kila mmoja huwa na chaguo lake. Kila mtu atakuwa na vigezo vyake ambavyo vinaweza kutofautiana kutoka kwa mmoja hadi kwa mwingine. Tofauti hiyo inakuja hata kwenye suala la tabia na uzuri. Kwa mfano, wapo ambao wanaangalia sana suala la tabia nzuri na muonekano mzuri pia. Lakini unaweza kushangaa mwanaume akatafuta mwanamke ambaye anakunywa pombe na anayependa kujirusha kwa kuwa na yeye ni mtu wa mambo hayo. Aidha, wanaume we

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki

Image
KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi. Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria. Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao. Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka, balaa linaanzia hapo! Kwa kuliangalia hilo, ndio maana leo nimekuj

Zijue Dalili 5 za tezi Dume

Image
Ugonjwa wa tezi tume imeelezwa ya kwamba ni miongoni mwa magonjwa ambayo yanasumbua jamii yetu kwa kiwango kikubwa sana na hata kupelekea kusababisha vifo. Hata hivyo tafiti mbalimbali zinazidi kuonesha ya kwamba  wanaume ambao wanatumia pombe kali kwa kiwango kikubwa wapo hatarini kupata ugonjwa huo. Licha ya wanywaji wa pombe kali lakini inasadikika ya kwamba wanaume ambao wanafanya kazi za viwandani, husasani viwanda vya rangi au wanaofanya kazi ya kupaka rangi wapo hatarini kupata  ugonjwa huo. Lakini pia wanaume ambao wapo hatarini kupata ugonjwa huo ni pamoja na wanaume wenye historia ya tatizo hili wenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zake (kaka au mdogo wa kiume) au baba kama amewahi ugua ugonjwa huu. Lakini pia watalamu mbalimbali wa masuala ya afya, wanazidi kueleza ya kwamba wanaume wenye umri wa kati ya miaka 40-70 wapo hatarini kupata ugonjwa huu wa tezi dumi. Lakini licha ya kuendelea kusambaa kwa kasi kwa ugonjwa huu watalamu wa afya wanaeleza ya kwamba

Unaweza Kuolewa na Mwanaume usiempenda?

Image
MUNGU ni mwema, Ni siku nyingine tunakutana kwenye kilinge. Tunajadili yale ambayo yanahusu uhusiano, uchumba na hata ndoa. Moja kati ya fikra ambazo zimekuwa zikiwatesa wanawake wengi katika mioyo yao, ni suala la kuolewa na mtu asiyempenda. Kila mmoja amekuwa na mtazamo wake katika suala hili. Kuna ambao wanaamini kwamba unaweza kuolewa na mtu usiyempenda lakini wapo ambao wanaamini huwezi. Wanaosema unaweza, huwa wanasimamia hoja ya kwamba hamuwezi kufanana kwa kila kitu. Mnakutana ukubwani, hivyo suala la mmoja kutompenda mwenzake, linaweza kubadilishika tu mbele ya safari kama vile mtu anavyoweza kumbadilisha mtu tabia yoyote ile. Wale ambao wanaoamini huwezi, huwa wanasimamia hoja moja tu kwamba utaishi katika kuudanganya moyo wako, hutafurahia ndoa yako na mwisho wa siku unaweza kuwa msaliti. Hoja hizi mbili zote zina mashiko. Kabla ya kuendelea, tusome kwanza mfano huu ambao msomaji wangu aliyejitambulisha kwa jina moja la Jack alinisimulia. “Kaka mimi naitwa Jack, nina mi

Maneno sita ya kumfurahisha mpenzi wako

Image
Mnakubaliana nami kuwa kupenda mtu ni tofauti na kuishi kwa upendo. Kumpenda mtu ni rahisi lakini kwa kuishi huo upendo, yaweza kuwa ngumu kidogo. Ian Isherwood anasema kuwa kurudiarudia huu mshororo wenye maneno matatu tu, "I Love You" Mara kwa mara haitoshi kuweka mapenzi ya uhusiano wenu kunoga zaidi milele. Kuna Sentensi sita muhimu sana ukimwambia mpenzio mara kwa mara napenzi yenu yafikia upeo. Kila mtu ana njia yake ya kumwonyesha mpenzi wake kuwa anampenda na kumjali. Haijalishi ni maneno yepi hutumia. La maana ni kwamba uhusiano wake na mpenziwe unadumu kwa raha tele. Ukitumia maneno mazuri kwa mpenzi wako unampa furaha na kumwonyesha kuwa yeye ndiye mtu wa kipekee kwako duniani. Kama unaye mpenzi, anza kutumia , maneno haya sita na uhusiano wako utakuwa wenye raha;   1. Nimebahatika kuwa nawe Kumwelezea mpenzio vile unajisikia kubahatika kuwa naye katika maisha yako ina uzito zaidi kuliko " Love You". Wakati unampenda mtu sana unajiona duni kwamba hata

Maneno sita ya kumfurahisha mpenzi wako

Image
Watu Wengi Ambao Wako Kwenye Uhusiano Wanalalamika Kuwa Wenzi Wao Hawawaoneshi Upendo Kama Ilivyokuwa Siku Za Mwanzo Za Uhusiano Wao. Wanaeleza Kuwa Wanaona Uhusiano Wao Unalegalega Na Mapenzi Yanapungua Taratibu Kama Barafu Iyeyukavyo Juani. Ili Kuepuka Yote Haya, Hauna Budi Kujifunza Njia Za Kuwasha Upya Moto Wa Upendo Kila Wakati Kwa Kuongeza Ukaribu (Intimacy) Kati Yako Na Mwenzako. Zifuatazo Ni Mbinu Zitakazokusaidia 1. Kucheka Pamoja na mpenzi wako Kicheko Ni Mlango Wa Ukaribu, Kama Mwaweza Kucheka Pamoja Basi Mwaweza Kulia Pamoja, Na Hapa Mwaweza Kuaminiana Zaidi Katika Kuwasiliana Hisia Zenu, Kama Waweza Kuitofuta Furaha Katika Kila Kitu Basi Unaweza Kupenya Katika Vyote. Usiwe Mgumu Na Mwenye Msimamo Mkali Katika Kila Kitu. Jifunze Kujizuia Pale Unapoanza Kuelekea Kwenye Kukasirika Na Badala Yake Tumia Kucheka Kama Mlango Wa Kutokea. Kama Utaanza Kujizoeza Hivi Ukiwa Nyumbani, Taratibu Utaweza Ukiwa Ofisini Na Hata Kwingine Kokote. 2. Kutiana Moyo na mpenzi wako Kila Mmoja

Namna ya kuachana kwa amani na mpenzi wako

Image
Kumaliza mahusiano si kitu rahisi sana hata kama ni hakika umemchoka mwenzi wako na hata kama uhusiano wenu si mzuri kiasi kwamba uko tayari kuwa huru. Kwa hiyo basi, kuvunja mahusiano ya kimapenzi ni jambo ambalo haliwezi kuepukika. Hata hivyo kumaliza mahusiano kwa amani ni vizuri na inapendeza kuliko kuumaliza kwa ugomvi na jazba. Kumbuka "The Golden Rule": Kwamba ungekuwa ni wewe ungependa uachwe vipi? Kama upo katika mahusiano yasiyo na tija na unafikiri kwamba imefika wakati unahitaji uhusiano wenu uvunjike, basi dondoo zifuatazo zitakusaidia kumaliza mahusiano na mpenzi wako kwa amani. Kitu kimoja kikubwa cha kuzingatia ni kuweka Jazba pembeni: 1. Kuwa Na Uhakika Na Unachotaka Kufanya:  Kama huna uhakika juu ya hisia zako kwa mwenzi wako unapotaka kuvunja uhusiano bora usifanye hivyo maana utafanya moyo wako usiwe na maamuzi dhabiti aka "Maamuzi magumu". Kama una hisia naye pia itamfanya achanganyikiwe na ajisikie kuwa bado anayo nafasi ya kuwa na wewe ama

Mambo 40 yanayovunja au kuharibu Mahusiano au Ndoa

Image
1. Kutokuwa na mawasiliano ya karibu na mwenzi wako. 2. Kutojali maumivu ya mwenzi wako. 3. Ubishi usiokuwa na maana. 4. Kupenda kujihesabia haki. 5. Kutokubali makosa. 6. Kutokuwa na roho ya msamaha. 7. Kutokuwa muwazi kwa mwenzi wako. 8. Usaliti wa mapenzi. 9. Kuigiza kupenda. 10. Kutomheshimu mwenzi wako. 11. Kuwa mjuaji kila kitu unajifanya unajua. 12. Kutokutambua uthamani wa mwenzi wako katika maisha yako. 13. Kuwa na jeuri. 14. Kutokuwa na kifua cha kuficha mambo ya nyumbani. [chumbani] 15. Kuto kujali watu wa nyumbani kwako [ndugu,watoto n.k] 16. Kujiamulia kufanya vitu bila ushauri wa pamoja. 17. Kutokuwa na faraja na mwenzi wako [kutokujua jinsi ya kumfariji mwenzi wako] 18. Kutomridhisha mwenzi wako kimapenzi. 19. Kuwa na amri kwa mwenzi wako hata kwa mambo yasiyokuwa na maana au malengo katika maisha yenu. 20. Ugomvi wa muda mrefu usiokuwa na suluhu. 21. Kuwa na ahadi za uongo. 22. Kumdhalilisha mwenzi wako mbele za watu. 23. Kupenda starehe kuliko kuujenga uhusiano wa k