Posts

Showing posts from December, 2019

MAMBO MUHIMU YA KUFAHAMU UNAPOACHANA NA MPENZI WAKO

Image
Watu wengi, wanaume kwa wanawake wakiachwa na watu wanaowapenda kitu cha kwanza kufanya ni kuangalia kasoro zao.  Kujiangalia wamekosea wapi na wanamapungufu gani ambayo yamewapelekea kuachwa. Hali hii huwafanya kutokujiamini na kujiona kama wana  kasoro flani hivyo kuwawia vigumu wanapoingia katika mahusiano mapya.  Lakini hembu nikuulize kama ulishakutana na hali hii je ulishakaa kitambo kidogo na kujiuliza labda tatizo sio wewe. Kwamba kweli kakuacha lakini inawezekana kakuacha kwakua hakuwezi na sio kwamba hufai. Kwamba ingawa wewe unamuona wamaana, unamuona anajiamini lakini yeye hajiamini kuwa na mtu kama wewe. Anajidharau na anaona kama akiendelea kuwa na wewe ipo siku utamuacha na ataumia sana. Sasa nikuambie kitu Kama mpenzi wako kakuacha Kwa matusi, kejeli na vitu kama hivyo. Kuna uwezekano mkubwa hajiamini au alishaona dalili kuwa unaelekea kumaucha na kaona akuche mapema ili aibu iwe kwako. Kwamba usije ukaringa kuwa umemuacha kwakua yeye ndiyo kakuacha! Unapoachwa

UKIKOSA SABABU; USIVUMILIE KWENYE MAPENZI

Image
N IMEWASIKIA  washauri wengi wakisema uvumilivu ni kitu muhimu katika mapenzi! Bila shaka hata wewe umewahi kuambiwa na wazazi au rafiki zako “vumilia tu” ukiaminishwa kuwa ndoa au mapenzi yana changamoto nyingi zinazohitaji uvumilivu. Kama hujui, uvumilivu ni mzigo mzito; ukikubali kuvumilia, lazima uwe na sababu ya kufanya hivyo. Ukikosa sababu ya kuvumilia katika mapenzi hutakuwa tofauti na mtu aliyebeba furushi zito kichwani halafu hajui alipeleke wapi na wakati gani atalitua na kwa faida gani. Kamusi ya Kiswahili inaeleza maana ya uvumilivu kuwa ni; “Hali ya kustahimili machungu.” Huku kamusi hiyohiyo ikitafsiri ‘machungu’ kama matatizo makubwa yanayosababisha masikitiko. Ukiambiwa vumilia maana yake uwe tayari kustahimili matatizo makubwa yatakayoleta masikitiko ndani ya moyo. Kwa kisingizio hiki kuna baadhi ya wanawake wanakesha wanalia kwa manyanyaso yasiyokoma kutoka kwa wapenzi wao. Ukiwauliza kwa nini hawaachani na matatizo hayo makubwa watakuambia; “Tunavumilia.” L

MADHARA YA WAPENZI KUGOMBANA NA KUNUNIANA

Image
M ADHARA  Karibu tena katika ukurasa huu mzuri. Wiki iliyopita tuliianza mada hii kama inavyojieleza hapo juu. Nilianza kwa kukupa ushuhuda wa mmoja kati ya wasomaji wangu, dada yetu ambaye yupo kwenye wakati mgumu sana akihitaji msaada wa kimawazo kutoka kwetu.   Suala lake kwa kifupi ni kwamba, alikuwa na kawaida ya kugombana mara kwa mara na mumewe kisha wananuniana kwa muda mrefu, mwisho akajikuta akiingia katika mtego hatari wa kumsaliti mumewe. Tatizo linakuwa kubwa zaidi kwa sababu anaonesha kuanza kuzama kwenye penzi la mchepuko! Nakushukuru msomaji wangu ambaye umenitumia ujumbe wa kumshauri dada yetu huyu, meseji zilikuwa ni nyingi na zenye ujumbe maridhawa, niseme tu kwamba mchango wako ni wa muhimu sana. Tukija kwenye hoja yetu ya msingi, ushauri ambao wengi wenu mmeupendekeza na ambao ndiyo hasa unaomfaa dada huyu, ni kwamba alifanya makosa makubwa kwa kumsaliti mumewe na hata kama mume ndiye aliyekuwa sababu ya yeye kufanya dhambi hiyo, bado ukweli unabaki palepale

TABIA ZA WATU WENYE USALITI KATIKA MAHUSIANO

Image
Usaliti ni jambo baya sana katika mahusiano, usaliti si ujanja japo wengi wanaowaza kusaliti huwa wanajiona wajanja. Wanajiona wamefanikiwa pale ambapo wanasaliti na wenza wao kutogundua kama wanasalitiwa. Siku zote anaesaliti huwa anajiona mjanja kwamba yeye anasaliti wakati mwenzake hasaliti. Kwa asilimia kubwa wanaume hujiona kama usaliti ni halali yao, wanataka wao wasaliti lakini wapenzi wao wasithubutu kusaliti. kwanini hawataki wenzi wao wasaliti? Eti wanaumia, hakuna kitu kinacho mchukiza mwanaume kama kusalitiwa. Kusaliti asaliti yeye, akisaliti mwenzake ni kosa la jinai anaona amedhalilishwa. Anajisikia fedheha kwamba mpenzi wake amemuonaje? Amemchukuliaje? Hajakamilika idara gani? Anawaza sana na kujiuliza jamii nzima inayojua kitendo hichoitamtazamaje? Hapo ndio unakuta mwanaume anaamua kuchukua uamuzi mgumu ikiwemo hata kuhatarisha maisha ya mwenza wake. Zifuatazo ni dalili za usaliti: Kutopenda kuchimbwa. Mara nyingi anaesaliti huwa hapendi kuchimbwa mambo kwa und

MBINU RAHISI ZA KUMFANYA MWANAMKE AJIGONGE KWAKO

Image
#1 Mfanye mwanamke ajieleze kwako Unaweza kumuuliza swali kama “Ni kitu gani ambacho kinakufanya unique/tofauti na wengine?” Ama kumwambia, “Wewe unakaa mdogo sana kiumri kwangu. Ni kitu gani ambacho uko nacho ambacho kitaziba pengo hilo?” Ataanza kukupatia sababu ambazo anajiona kuwa yeye ni unique – kiufupi atakuwa akijaribu kujieleza zaidi ili ajipendekeze kwako/ umpende zaidi. Yaani atakuwa anajaribu kuhakikisha kuwa unaridhika na kila kitu ambacho atakwambia. Na uzuri wa kutumia mbinu hii ni kuwa kadri mwanamke anavyokuwa mrembo ndivyo zaidi utakavyohitajika kumfanya ajihitimishe kwako, usiogope kumuuliza maswali ambayo yatamlazimu ajihitimize kwako. Muulize maswali mazito. Muulize maswali ambayo itakuwa ngumu kwake kujihitimu kwako. Na kitu cha kufurahisha kuhusu wanawake warembo, ni kuwa wamezoea kufukuziwa na wanaume kiasi cha kuwa ukianza kuuliza maswali na kujihitimu kwako, atafall na wewe zaidi. Hii ni kwa sababu hawajazoea kuulizwa maswali kama hayo. Hawajazoea kuam

UKIMPATA MCHUMBA MWENYE SIFA HIZI USIMWACHE AENDE

Image
Mahusiano yoyote mazuri yanatengenezwa. Yana hatua za kupita. Hauamki tu asubuhi ukawa na uhusiano mzuri, ni lazima ukubali kujifunza na kufanya maamuzi sahihi ili uweze kufikia malengo yako katika muda muafaka. Wengi wamejikuta wakipoteza muda kwa kushindwa kufanya maamuzi sahihi. Wamejikuta wakiingia kwenye uhusiano bila kujua wanataka nini na matokeo yake kujikuta wakipoteza muda na uhusiano wao unakuwa hauna malengo. Tunafahamu kwa pamoja kwamba, ili ufikie kwenye hatua ya ndoa ni lazima upitie hatua mbalimbali. Urafiki, uchumba na hatimaye muingie kwenye hatua ya ndoa. Ukikosea kwenye moja ya hatua hizo lazima upate madhara mbele ya safari. Mchumba mzuri ana sifa gani? Utamjuaje? Hili ndiyo darasa la leo na hapa chini utakwenda kupata elimu, twende sambamba. Mchumba mzuri ni yule ambaye tangu awali anaonesha kujitambua, anajua nini anapaswa kufanya kwa wakati muafaka. Aina au mfumo wa maisha yake unauona kabisa tangu mwanzoni kwamba huyu amekomaa kiakili, anayatamani maish

MADHARA YA KUFANYA TENDO LA NDOA MARA NYINGI KUPITA KIASI

Image
Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono. Kuna watu ambao hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.  Mtu anaweza kuwa na mke na kujikuta kila siku anatumia ‘chakula cha usiku’ kwa sababu tu hakuna wa kumkataza na kwamba ana haki ya kufanya hivyo kwa sababu amelipa mahari. Hilo linaweza kuwa jambo jema kwa upande mwingine, lakini uchunguzi unaonyesha kuwa watu wengi kati ya watu wanaolalamika kupoteza hisia za kimapenzi hutoka katika kundi la watu wapenda ngono.  Pamoja na tatizo hilo, yapo madhara mengine mengi ambayo mtu asiyekuwa na kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo, hivyo ni vema tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi cha kulazimika kufanya mapenzi kila tunapokutana hata kwenye nguzo ya umeme na chini ya miti kwa vile tu miili imetaka kufu

MAMBO MATANO (5) YATAKAYOKUSAIDIA ILI UWEZE KUFANIKIWA

Image
Je una shauku ya kutaka kuongea na Mungu moja kwa moja? Ili akupe majibu yako kwa habari ya maisha yako?! fuata kanuni hizi ili uweze kufanikiwa moja kwa moja katika mambo unayoyafanya au unayotaka kufanya: 1. Kuwa mtu wa kusamehe, usipende kubeba vinyongo vya kutowasamehe wengine, kwani kufanya hivyo kuna kuweka katika mazingira ambayo kimisingi utashindwa kufanya mambo yako na kijamii yaletayo mafanikio. Lakini pia kumbuka kama hautakuwa mtu wa kusamehe pia hata wewe utashindwa kusamehewa pia. 2. Ichukie dhambi na uiache  kabisa, kuwa mtu wa toba, jikague moyo wako na matendo yako kila siku, omba rehema za Mungu unapoona umeenda kinyume na maagizo yake. 3. Acha tabia ya kuwasengenya na kuwasema  watu na watumishi wa Mungu, wapende na uwaombee, maana siyo kazi yako kuhukumu. Wapende na wengine, mtu akikosea muite muonye kwa upendo na umuombee acha tabia ya kusengenya wenzio, unajichelewesha. 4. Kuwa mtu wa maombi, maana yake siyo kila siku ushinde umejifungia, hapana kuwa mtu

MAKOSA YANAYOFANYWA NA WANAUME KATIKA MAHUSIANO

Image
Kuna mambo ambayo mtu anaweza kufanya pasi na kujua kuwa anafanya makosa. Ikija katika masuala ya mahusiano, wanaume wengine huchukulia kama mzaha. Wakishafaulu kutongoza na kumteka hisia mwanamke, wao hujisahau na kuanza kuishi nao kama mtu wa kawaida. Leo tumekuja na ujuzi wa kukuonyesha makosa ambayo unaweza kuwa unayafanya bila kujua kuwa yana athari. Kiufupi ni makosa ya kijinga ambayo yanaweza kuepukika kirahisi iwapo utayafuatilia. Hii ni muhimu kwa kuwa ukiachana na makosa haya basi unaweza kudumu katika mahusiano marefu na mpenzi wako zaidi. Yafutayo ndiyo makosa yanayofanywa na wanaume katika mahusiano; Unasahau kujijenga kibinafsi Kosa lengine ambalo wanaume hujipata katika uhusiano ni pale ambapo wanatelekeza majukumu yao ya kujiendeleza kimaisha. Wanasahau mambo ambayo walikuwa wakifanya ama walikuwa wakitarajia kufanya kabla kuingia katika uhusiano wa kimapenzi. Kusahau marafiki zako Ni kawaida kupunguza mawasiliano na marafiki zako pindi ambapo utaingia katika ma

UKIMPATA MWANAMKE MWENYE SIFA HIZI 16 USIMUACHE KAMWE

Image
Hizi ni sifa halisi za mwanamke wa kweli 1. Ni nguvu ya mwanaume 2. Ni jasiri 3. Mchapakazi 4. Mwenye kujiamini 5. Tegemeo la familia 6. Mwalimu wa watoto na familia yake kiujumla 7. Mlinzi wa mwanaume. 8. Chanzo cha baraka ya familia. 9. Adui wa maadui wa familia. 10. Sauti ya familia. 11. Mponyaji wa familia yake na taifa. 12. Mlezi wa huduma. 13. Mkombozi wa familia na taifa. 14. Msaidizi wa Mungu tumfanyie msaidizi wa kufanana naye. 15. Mwombezi wa familia, huduma na taifa. 16. Mficha siri wa Mungu