Posts

Showing posts from November, 2020

Makosa Makubwa Wanayoyafanya Wanawake linapokuja Swala la Kupenda..!

Image
  Je wewe ni mtu wa kupenda ghafla, yaani mwanaume anapokutamkia kwamba anakupenda huwa unamuamini kwa kiasi gani, unakuwa ni mwepesi wa kumuamini na kujitoa kwa ajili yake au unakuwa na kujivuta vuta ili kujiridhisha kabla ya kuingia katika uhusiano? Hebu fikiri kabla ya kuamua, jipe muda kwani hakuna jambo lililo jema kama subira linapokuja swala la kupenda. Subira itakuepusha kupoteza muda wako katika mahusiano ambayo hayana mashiko wakati dhamira yako ilikuwa ni kumpata mwenzi mwenye sifa muafaka, pale utakapoingia mahali ambapo sipo. Kwa kawaida kutoka katika uhusiano huo kuna gharama kubwa na kunaweza kukusababishia matatizo mengi yakiwemo ya kiafya. Hapa chini nitajaribu kueleza makosa kadhaa ambayo wanayafanya wanawake linapokuja swal la kupenda: 1.Kumbadili mtu awe vile utakavyo: Usije ukajidanganya kwamba unaweza kumbadilisha mtu mzima na akili zake. Kama umepata mwanaume ambaye kwa mtazamo wako unamuona ana sifa muafaka lakini anatabia ambazo huzipendi kwa mfano ulevi au kuv

Yafahamu mambo ambayo mwanamke anayahitaji katika mahusiano ya kimapenzi

Image
  1. Anataka mume anayemjali na kujali kila anachokitaka. Sio tu mahitaji ya kimwili, bali pia ayatambue mahitaji yake ya kisaikolojia, upendo na kujali hisia zake. 2. Anataka mume anayemlinda na kumfanya ahisi kuwa yuko salama wakati wowote, kiasi kwamba hana hofu ya chochote kwa sababu anajua kwamba mumewe atamlinda na kumkinga na maudhi. 3. Mume anayehisi kwamba ameshikamana naye na kuridhika naye. 4. Mume anayeshiriki naye katika maongezi matamu yenye hisia tamu. mume anayempa maneno laini, sio maongezi makavu yasiyokuwa na hisia za kimahaba. 5. Anataka mume anayembusu kila anapoagana naye au anapokutana naye. Mke anapenda jambo zuri linalofanywa mara kwa mara hata kama ni dogo, kuliko jambo kubwa linalofanywa kwa kuchelewa au kwa muda mrefu. Busu unalompa kila siku kabla ya kwenda kazini ni bora kwake kuliko “outing” unayompa baada ya miezi sita. 6. Anataka mume anayeyaona yanayofanywa na mkewe kwa ajili yake, hata kama ni madogo. “Attention” ya mume kwa mke ni jambo muhimu mno. A

Jinsi ya kumshawishi mwanaume akuoe

Image
  Kumfanya mwanaume aweze kuwa na majukumu ya kimaisha ni vigumu, lakini hizi mbinu ambazo tuko nazo za kumfanya mwanaume akuoe zitahakikisha umesimama na yeye madhabahuni haraka sana. Hivi wewe umekuwa katika mahusiano na mwanaume kwa muda mrefu mpaka unaanza kushuku iwapo huyu mwanaume yuko serious na wewe ama anakuchezea tu? Na umekuwa kila siku ukimwomba Mola akusaidie angalau amfanye huyu mwanaume ulie naye atoe ishara za kuwa atakuoa mbeleni. Well, sote tunajua kuwa ndoto ya kila mwanamke ni kuwa siku moja katika maisha yake atakuja kuolewa kwa harusi…so sisi hapa tunataka kukupa maujanja ya kumfanya huyo mwanaume atake kukuoa haraka sana. Jinsi ya kumshawishi mwanaume akuoe; Kuwa girlfriend kamili. Hivi wewe na mwanaume huyu mumekuwa na maisha ya fanaka. Nyote wawili mumeinjoy maisha ya furaha, mumezama katika mapenzi, na unaona kwamba una uwezo wa kumwambia kila kitu ambacho unakifikiria. Lakini hebu ngoja kidogo na ufikirie mambo ambayo unaweza kufanya zaidi ya hayo. Mfanye aj

Ni Kweli Mapenzi ya Wizi ni Matamu Kuliko Katika Ndoa Halali?

Image
  Mapenzi ni kitu ambacho kinafanya wapenzi kufurahia wakiwa pamoja lakini kwa sasa kumekuwepo kwa kusalitiana katika mahusiano. Imekuwa kama kawaida mwanamke/mwanaume kuwa na mchepuko huku tayari yupo kwenye ndoa yake. Kwa nyakati za sasa uzinifu si kitu cha ajabu tena.Wahusika wanadai kufaidi uasherati kuliko tendo la ndoa.Kumekuwepo kuchokana kwa wawili walio katika ndoa na kufanya mmojawapo ajaribu kutafuta kuridhishwa nje ya ndoa.Jamii yahitaji kuelimishwa juu ya kuridhishana katika ndoa kwani itafikia mahali ndoa itakuwa ni ya jina tuu. Tusaidiane katika Kushauriana  Unafikiri nini chanzo cha utamu wa mapenzi ya kuchepuka kuliko mapenzi ya ndoa halali?

Ni Sawa Kutumia Mswaki Mmoja na Mpenzi Wako?

Image
  Jamani usiombe mapenzi yakakunogea utatamani ugandane na mpenzi wako kila mahala. Katika kona kona za mapenzi mapenzi leo nimekuta na hii kitu. Mara nyingi watu wanapokuwa katika mahusiano ya kimapenzi huwa wanaaminiana kupita kiasi hata kama hawakuwahi kuchunguza afya zao. Hali hii hupelekea wapenzi kuchangia vitu mbali mbali kama nyembe, mswaki,mkasi hata wengine hufikia hatua ya kuchangia pichuu! "ukivaa BOXER yangu na vaa KIBINI yako" Hapa leo nitahitaji tuongelea kitu kimoja. Mswaki,hivi ni sahihi wapenzi kuchangia mswaki? Na kiafya iko vipi, hakuna magojwa yoyote yanayoweka kutokea kwa kuchangia mswaki? Au matumaini yetu yako juu ya zile dawa za meno tupe Mtazamo wako.

Hii Ndio Jinsi ya Mwanamke Kuepuka Kuwa Mchepuko

Image
  Mara nyingi asilimia kubwa ya wanawake hupenda kuwa na wanaume wanaojiweza kiuchumi. Lakini baadae wanapotambua kwamba mwanaume huyo ameshaoa hushangaa sana, huumia na kusema waliwaamini kuwa wako single na kwamba wanaume wote ni mbwa tu. Wanaume sio mbwa au paka shume, ni nyie wenyewe ndio mnashindwa kuwaelewa na hamtaki kufanya uchunguzi. Mlishaambiwa kwamba nyuma ya mwanaume mwenye MALI na MAFANIKIO kuna mwanamke. Na wewe unataka mwanaume aliyefanikiwa. Unategemea nini? Kama utakutana na mwanaume ambae ni handsome, ana mali, anaendesha gari nzuri, yuko vizuri kiuchumi, basi huyo sio mumeo mtarajiwa, huyo ni mume wa mtu fulani kwa muda huo. Ni agharabu sana kukutana na mwanaume anayejiweza halafu akawa single, either uwe shareholder au unyang'anye share zote za mwanamke mwenzako kitu ambacho sio busara hata kidogo. Mume wako mtarajiwa yupo anahangaika kutoka na maisha, anapigania ndoto zake. Huenda yupo shambani, Konda wa Dala dala, yupo anauza duka mahali, anapiga kitabu chuo,

JE Unafahamu Laana ya Kutembea na Mume wa Mtu na Madhara Yake ?

Image
  Kutembea na mume wa mtu sio jambo zuri japo wanawake wengi wanaona ni kawaida bila kujua wanajilimbikizia laana itakayofanya maisha yao kuwa magumu mbeleni. Machozi ya uchungu ya mwanamke mwenzio juu ya mume wake hayafutiki haraka.. Ni kama zigo la kinyesi mgongoni linavutiwa na inzi pekeake. Huyo mwanaume unaemuona Leo ana mke, Pesa na mali na kuona ndo fursa kwako kumpata kwasababu anajua kujali na anapesa za kutosha kukugharamia.... Ukirudi nyuma miaka 10-15-20 mwanaume huyo huyo alikuwa kama huyu unae mkataa leo Unaye muona hajui kuvaa.... Hana pesa za kutosha.. Hana mali kwahiyo hakufai. Wanaume wengi wanaanzia chini... Jitihada za wake zao zinawafikisha walipo Leo. Heshimu jitihada hizo. Heshimu siku walizofunga kwa ajili ya waume zao. Heshimu machozi waliomlilia Mungu awafikishe walipo... Heshimu muda na jasho walilolitoa kuhakikisha waume zao wanaonekana watu mbele za watu. Muombe Mungu akupe wa kwako hata kama masikini mpate utajiri pamoja. Na wewe ubige magoti , ulie na kuf

HASARA ya Kushauriwa Uamuzi Juu ya Mapenzi..!!!

Image
  Wengi wamekuwa wepesi sana kukimbilia kwa rafiki, ndugu zao ili kuomba msaada wa mawazo ya nini wafanye kwenye mapenzi. Imani iliyojengeka kwa watu wengi katika jamii yetu ni kuwa ushauri ni kitu muhimu sana kwa kila hatua. Kwa mtazamo wa haraka unaweza kuishia kwenye ukomo huo wa fikra na kuamini juu ya ushauri wa mtu kukufikisha mahali sahihi kwenye mapenzi. Unapokerwa na mpenzi unakimbilia kushauriwa na wakati mwingine hata unapotaka kuoa au kuachana na umpendaye, unamuomba rafiki yako ushauri. Je, umeshawahi kufikiria hasara za kuomba ushauri wa kimapenzi kwa rafiki yako? Hebu ungana nami nikumegee kidogo hasara za ushauri ambao siku zote ndio unaona kimbilio kwako UTAKUPOTOSHA Ni wazi kwamba kipimo cha uelewa kinatofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Ifahamike kuwa, uhodari wa mambo nao hutofautiana, mtu anaweza kuwa mahiri katika siasa na akaaminika kwenye jamii, lakini ukimpelekea suala la mapenzi anakuwa hajui kitu, hivyo ni rahisi kukupotosha. Uchunguzi unaonesha ku

KISA Cha Kusikitisha 'Baba Yangu Alisababisha Nilale na Mjomba Wangu, Kamwe Sitamsamehe'

Image
  Nimeona leo nitoe siri yangu hapa ya muda mrefu ambayo imekuwa ikiniumiza sana pale tu ninapokumbuka, nakosa raha na amani inapotea. Kwa ufupi kabisa, nilizaliwa mkoani Mara wilaya ya Musoma mjini maeneo ya Nyakato, mama yangu alibeba mimba yangu akiwa darasa sita hivyo hakumaliza shule. Ilibidi akae nyumbani mpaka pale alipojifungua, kwa wakati kulikuwa hakuna sheria kali kwa wanaowapatia wanafunzi mimba wakiwa shule. Na aliyempatia hiyo mimba naye alikuwa mwanafunzi mwenzake lkn alikuwa la saba yeye alimaliza shule. Baba yake mama ambaye ni babu yangu alikuwa na uwezo mkubwa hivyo hakushindwa kutulea mimi na mama. Nikiwa na miaka 6 ndipo nilipokuja kumjua baba yangu wakati huo nae alikuwa amekuwa mtu mzima, alikuja akanisalimia akaondoka, kwao pia walikuwa vizuri kimaisha. Nikiwa na miaka 9 naanza darasa la kwanza wakati huo tulikuwa tunaingia shule tukiwa na umri mkubwa tofauti na sasa. Mama aliolewa na mume mwingine na alikuwa ni askari jeshi, alifanikiwa kuzaa nae watoto wanne j

Ukweli Kuhusu Kupata Watoto Mapacha na Jinsi Wanapatikana

Image
  Inasemekana kwamba haijalishi kama mume/mwenza wako ni pacha ama ametoka kwenye familia yenye historia ya mapacha. Mwenye uwezo wa kusababisha watoto mapacha ni mwanamke pekee. Ikiwa na maana mwanamke ambaye ni pacha ama ndugu zake wa kike kama vile dada, mama wana historia ya kuwa na mapacha ama wao ni pacha basi mwanamke huyo ana nafasi kubwa ya kupata watoto mapacha. Kwa mfano: Mwanamke ambaye mke wa mjomba wake ana mapacha haimpi yeye nafasi ya kupata mapacha kwa sababu hana uhusiano na mke wa mjomba wake kibailojia. Ila mwanamke ambaye dada yake ana mapacha inampa uwezekano wa kupata watoto mapacha kwasababu wana uhusiano wa moja kwa moja. Hembu tujifunze hatua moja baada ya nyingine. Kwanza tufahamu mimba inatungwa vipi? Na kisha tuone jinsi gani mimba ya watoto mapacha inavyotungwa. Mimba inatungwaje? Kipindi cha ovulation ndipo ambapo mwanamke anaweza kushika mimba. Ovulation ni kipindi ambacho yai kubwa ama yai lililo tayari hutoka kuelekea kwenye tumbo la uzazi kupitia miri

Haya Mambo Yafuatayo Huwafanya Wanawake Wengi Kushindwa Kuingia Katika Ndoa (Kuolewa)

Image
  Pamoja na kuwa kuna wanawake husita kuolewa, lakini jambo hili si kubwa sana kwa wanawake kama ilivyo kwa wanaume. Kwa kiasi kikubwa katika suala la kutaka kuingia ndani ya ndoa, wanawake ni wengi ambao hutaka kufunga ndoa kuliko ilivyo kwa wanaume. Hilo tunaliona wazi tokana na shamra shamra awazo nazo mwanamke wakati wa maandalizi ya shughuli za Ndoa na Harusi. Hata hivyo, kwa wale wanawake wachache ambao husuasua kuolewa hizi ni baadhi ya sababu zinazopelekea kusuasua huko. (Izingatiwe hii ni kwa wanawake ambao hawajawahi kuolewa kabisa) Vigezo vilivyopitiliza viwango (hasa kwa muonekano) Wanawake wengi hasa wa umri mdogo (lakini unatosha kuolewa) hutumia muda mwingi katika kuchagua aina ya mwanaume ambaye angependa awe mume wake. Wanawake hawa hujiamini zaidi na kusimamia sifa zile ambazo huamini ni muhimu mwanaume wa kumuoa awe nazo.  Vigezo hivyo huwa hata kwa misingi ya muonekano wa mwanaume huyo – kuna wale ambao hutaka mwanaume huyo wa kumuoa awe na sifa kama vile, mrefu, al

Nimegundua Wanawake wengi (85%) Wanateseka Sana Ndani ya Ndoa....Embu Zindukeni.....

Image
  Hili jambo limeniuma sana tena sana, wanawake wengi wanaonewa na waume zao bila kusema popote wakijua ndio kuvumilia kumbe hawajui wanajiua pasipo kujua inaniuma sana. Nimeongea nawanawake zaidi ya 20 walio wengi hawana raha ya ndoa au tuseme tuu ya maisha wanasema wanavumilia huku miaka inaenda wakiwa ndani ya mateso makali, Kama kulea familia wenyewe bila kusaidiwa na baba hata senti, kufungiwa nje bila huruma yani kufukuzwa, kutukanwa na kudharauliwa, kupigwapigwa hivyo hata kuachiwa ulemavu, kubebeshwa mzigo wa kulea watoto wenyewe au kutelekezewa watoto mwanaume akapotea kabisa nyumbani baada ya miaka kumi hadi ishirini ndio anarudi na watoto wanamfurahia bila mama kufanya lolote, wanaume 98% kutokuwa waaminifu ndani ya ndoa zao, kuambukizwa magonjwa ya zinaa na ukimwi, na kugeuzwa kuwa punda wake bila huruma, kwakweli hili jambo limeniuma sana wanaume walio wengi ni mashetani wanaigiza kuwa binadamu hivyo kupelekea wana wake kufa haraka. Wanawake embu zindukeni kuna maisha zaid