WANAWAKE ACHENI KUKAGUA SIMU ZA WAPENZI WENU, MTAJIPA MAGONJWA YA MOYO BURE

Habari wa ya muda huu wasomaji wetu karibu kwenye ukurasa wetu wa mahusiano.
Leo nina jambo moja ambalo nataka kuwaeleza wanawake wenzangu hasa katika kipengele cha kukagua simu ya mpenzi wako au mumeo.

Nakushauri usiwe mwepesi sana wa kukagua simu ya mumeo mara kwa mara kwani haiwezi kukusaidia lolote sana sana inaweza kuhatarisha mahusiano yenu na kujikuta mkaachana.

Mahusiano mengi yamekuwa yakivunjika kutokana na masuala ya simu. Kama hujawaji kuipekua simu ya mpenzi basi nakushauri uache kufanya hivyo.

Kama wewe kazi yako kila uionapo simu na kuanza kupekua nakushauri uache kufanya hivyo mara moja.

Unaweza kuigusa lakini usiangaike na yaliyomo katika simu. Wapo wengine hadi wakiona namba inapigwa mara kwa mara anaichukua na kuipiga.

Hilo sio sahihi yupo aliyefanya hivyo katuma message katika hiyo simu na kuanza kumtukana kumbe ni bosi wa mumewe.
Pia huwezi kukua mawasiliano yote anayofanya mumeo wengine labda ni wateja wake sasa ukifuatilia sana utamkosesha hata mawasiliano mazuri na wafanyabiashara wake.

Jambo unalitakiwa ni kuweka uaminifu kwa mume wako acha kuangaika na kupekenyua simu haziwezi kukusaidia wapendwa.

Kwanza unatakiwa kuelewa mwanaume wako yupo vipi je unawajua marafiki zake ni akina nani kuna wengine wanataniana ofisini labda gafla ukakuta message baby vipi leo hauji ofisini basi ukiona hivyo ni kununa na kumshikilia bango huyo ni kimada wako wakati ni mambo ya utani wa ofisini.

Nani asiyejua mautani ya ofisini inabidi mtu uyavumilie maana akili za ofisini wakati mwingine mnakuwa kama wanafunzi mna utani wa kijinga na inabidi tu ukubaliane nayo huwezi kuzuia.

Mwanamke mwenzangu inabidi kuvumiliana katika hilo usiwe mdadisi sana wa simu ya mumeo jitahidi kumjengea uaminifu mumeo au mpenzi wako.

Hivi kwa nini unaangaika na simu ya mwenzako kama umeamua kumpenda basi mkabidhi moyo wako hayo mengine achana nayo.

Unapojenga uaminifu kwa mpenzi wako au mume wako itasaidia mwanaume wako kukupa heshima yako na hawezi kukufanyia mambo ya ujinga.

Na endapo akifanya ujinga basi ujue atajitahidi kukujengea heshima yako usijue kile kinachoendelea kutokana na uaminifu wako kwake.

Kuna wanaume wengine ukipekua simu zao utatamani kuzimia kwanini uumize moyo wako jifunze kuwa na mipaka na simu ya mume wako.

Kuna wanawake wengine ukimuuliza ni lini kamkagua mwanawe madaftari yake hakumbuki ila yupo bize na upekuzi wa simu ya mume.

Embu wanawake wenzangu jirekebisheni mnawafanya hadi wanaume zenu wanakwenda kuoga na simu kwa kuogopa kukaguliwa simu zao. Waacheni wajinafasi na simu zao jamani.

Kumpekua sana simu mwanaume sio kumfanya awe mwaminifu katika penzi lenu. Kama ni mtu wa kufanya mambo ya ujinga ama kuchepuka atachepuka tu hata ukikagua simu mara 50.

Hivi unajua jinsi wamavyofanya wakikaribia nyumbani anafuta message zote na kumpigia mchepuko wake kuwa anaingia nyumbani asipige simu wala kutuma message.

Ina maana ukija kuikagua kuiona hakuna chochote ndio furaha yako au maana hapa mimi ndio ninachoshindwa kuwaelewa wanawake wenzangu. Embu jiongezeni wapendwa simu haikusaidii chochote.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUMFANYA MWANAMKE AKOJOE HARAKA WAKATI WA TENDO

JINSI YA KUMKOJOLESHA MWANAMKE KWA HARAKA

JINSI YA KUMFANYA MWANAMKE ASIKUSAHAU KATIKA TENDO LA NDOA