WANAWAKE ACHENI KUTOA SIRI ZA WAUME ZENU KWA MARAFIKI


Unapoingia katika mahusiano hasa wanawake jitahidi kujifunza kuwa msiri na mambo yako sio kila jambo ni kwenda kulizungumza ama kusimulia marafiki.

Katika mambo ambayo wanawake wanakosea ni hilo kutoa siri za mpenzi wake kwa marafiki ama kwa watu wengine.

Wengi wamejikuta wakiachwa katika mahusiano kwa kukosa kifua na kuanza kusimulia mambo ambayo wanafanya na mpenzi wake hadi yale ya chumbani.

Wanawake hivi huwa mnakosa ya kusimualiana mpaka unaanza kumsimulia mara mwanaume wangu ana mashine mashallah akitembeza mashine yake basi mwili unasisimuka nina pata raha sijawahi kuziona.

Yaani anajua kufanya mpaka utasikia unahama dunia, yaani hutamani hata atoe mashine yake maana utamu wake sio wa nchi hii, yaani ni raha kwa kwenda mbele anayajua mahaba yule mwanaume sijawahi kuyaona anajua kunidatisha mpaka ninadata saa zote nawaza penzi lake.

Unapokuwa unasimulia wenzako wanakusikiliza hivi unamsimulia mtu jinsi unavyopewa raha mpaka unafika kilelele wakati huyo unayemsimulia hajui kileleni kukoje.

Huwa nashindwa kuelewa nyie wanawake wenye akili chache hivi mnakosa vitu vya kusimulia mpaka unaenda kuelezea mambo yako ya chumbani kwa watu wengine.

Huyo unayeenda kumsimulia hayo mambo na yeye anatamani kufanywa vizuri kama wewe, hivyo ni lazima ahakikishe anakuchukulia mwanaume wako ili na yeye azipate hizo raha.

Jambo la kushangaza utaona huyo rafiki akishamchukua anahakikisha mwanaume hakukumbuki na kummiliki mwanzo mwisho na kujikuta umeachwa kwa ujinga wako.

Hivyo mahusiano yetu tunayavunja wenyewe tujitahidi kuwa wasiri sio kila jambo linalomhusu mpenzi wako kila mtu analijua.

Ukiachilia mbali ya mpenzi wako hata mambo yako binafsi unatakiwa kuyafanya yawe siri sio vizui kila akayajua mambo yako.

Baadhi ya wengine wanamjua mwanaume wa shoga yake kabla hata hajamuona kutokana na habari ambazo amepatiwa, hili sio jambo nzuri tujirekebishe tabia zetu.

Hivi mnapokutana na marafiki zako huwa mnakosa ya kuzungumza mpaka muanze kuelezeana masuala ya faraga na mpenzi wako. Huwa najiuliza unaanza vipi kuelezea jinsi mnavyofanyana yaani habari inaazaje mpaka kuanza kueleza jinsi mwanaume anavyokutembezea mashine yake.

Yapo mambo mengi ya kukutana na kujadiliana na marafiki zako hapa mimi nawaza jinsi ya kupata fedha huwezi kunikuta naelezi ujinga huo.

Kwa nini mnapokutana msijadiliane masuala maendeleo mambo yapo mengi mnaweza kujiunga kama kikundi kutengeneza sabuni za maji na kuziingiza sokoni.

Angalieni fursa zilizopo na kujipanga jinsi ya kuzichangamkia mkue kiuchumi, hizo mashine zipo na wala huwezi kuzimaliza. Hivi ulishawahi kusikia uchumi wa mashine? Maana mwingine kila kukicha yeye anawaza mashine hana jambo jingine kichwani kwake.

Tubadilike wanawake wenzangu usipojipanga katika maisha kila siku utakuwa unalalamika vyuma vimekaza na hiyo mashine haiwezi kukusaidia sanasana itakupa njaa.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUMFANYA MWANAMKE AKOJOE HARAKA WAKATI WA TENDO

JINSI YA KUMKOJOLESHA MWANAMKE KWA HARAKA

JINSI YA KUMFANYA MWANAMKE ASIKUSAHAU KATIKA TENDO LA NDOA