SABABU 6 ZINAZOFANYA MTOTO MCHANGA KULIA USIKU

 KWA mzazi yeyote anaelewa usumbufu unaotokana na mtoto anayelia usiku. Watoto wachanga wenye umri chini ya miezi 6 wanakuwa na matatizo haya zaidi. Mtoto anapolia huwa inaleta hisia kuwa mtoto ana shida na mara nyingi wazazi au walezi wanakuwa hawajui sababu au hata wakijua huenda wasijue jinsi ya kurekebisha tatizo na kumnyamazisha mtoto.

Ifahamike kwamba kulia ndiyo njia pekee ambayo mtoto anaitumia kuwasiliana na wengine juu ya shida ambayo anayo. Ni ujumbe kwa mzazi au mlezi kuwa hajisikii vizuri na anahitaji msaada. Sababu 6 kubwa za mtoto mchanga kulia usiku au mchana ni hizi:

UGONJWA WA TUMBO/ MAUMIVU MENGINE

Watoto wachanga wanasumbuliwa sana na maumivu ya tumbo na inaweza kusababishwa na chakula ambacho katika umri mchanga ni maziwa ya mama au maziwa ya bandia ambayo anapewa.

Kwa kuwa mfumo wake wa chakula bado ni mpya na unaendelea kukua basi unapata shida kumeng’enya chakula. Mara nyingi gesi inajaza tumbo na kusababisha maumivu kwa mtoto. Shida hii si rahisi kukabiliana nayo na imekuwa ikiwapa wakati mgumu wazazi kwa watoto chini ya miezi 3.

TIBA YAKE

Kumlaza mtoto kifudifudi ili atoe upepo ni njia mojawapo inayoshauriwa lakini katika usimamizi. Hata hivyo, ni hatari kumlaza mtoto mchanga kifudifudi kwa kuwa anaweza akajiziba hewa na kusababisha kifo.

Kumshikashika tumbo kwa mikono au kitambaa chenye maji ya uvuguvugu inaweza ikasaidia kumtuliza. Kuna dawa za kusaidia kulainisha utumbo wa mtoto na kutoa gesi. Tafadhali onana na daktari wa watoto upate ushauri zaidi.

NJAA

Mtoto akiwa na njaa na anahitaji chakula anaweza kulia ili kutaka shida yake itatuliwe. Lakini kwa bahati mbaya hana namna ya kukujulisha kuwa ana njaa ni kilio. Ni vyema kufahamu aina ya sauti ya kilio inayoashiria njaa. Utajua hili kwa mazoea yako ya kila siku na mtoto wako. Njaa ni mojawapo ya sababu kubwa kabisa ya mtoto mchanga kulia usiku.

TIBA YAKE

Ili kujihakikishia kuwa hatakuwa na tatizo hilo, mpe mtoto chakula kila mara. Kumbuka mtoto anakula kidogo na mara kwa mara. Kama mtoto anaendelea kulia baada ya kula au anakataa chakula basi kutakuwa na sababu nyingine ya kiafya, muone mt aalamu wa afya.

JOTO AU BARIDI

Kama ilivyo kwa watu wazima, joto kali kupita kiasi au baridi inakufanya ujisikie vibaya na kutafuta jinsi ya kurekebisha kama vile kuvaa vazi zito kama kuna baridi au kuwasha feni au kiyoyozi,vivyo hivyo kwa mtoto mchanga.

Hakikisha mtoto anavaa nguo sahihi kulingana na hali ya hewa. Mpunguzie nguo au kufungua madirisha kama kuna hali ya joto. Kama kuna baridi basi hakikisha unamvalisha nguo nzito mwilini ikiwemo miguuni na kichwani.

UCHOVU NA USINGIZI

Watoto wanalia wakiwa na usingizi. Hii inatokea mara nyingi sana. Watoto wengi wana tabia ya kulia kabla ya kulala. Fahamu kuwa mtoto anahitaji kulala muda mwingi sana inakadiriwa kwa masaa yafuatayo:

Mtoto wa miezi 1-3; masaa 15 (Mchana-5,Usiku-10), mtoto wa miezi 3-6; masaa 14 (Mchana- 4,Usiku-10), mtoto wa miezi 6-13; masaa 12-14 (Mchana- 3,Usiku-11). Kama ukifahamu mtoto analia kwa sababu ya usingizi au uchovu basi muogeshe na kumweka katika mazingira ya kulala.

Watoto wengine wanalala vizuri wakiwa wameshikwa mikononi na kuchezeshwa badala ya kitandani. Watoto wanahitaji kubebwa na kukumbatiwa. Hii ni njia ya asili ya kuonesha upendo kwa binadamu huyu mdogo. Mtoto anapokuwa amelazwa kwa muda mrefu huwa anachoka na hulia, anahitaji kugeuzwa na pengine kubebwa mikononi na kukumbatiwa hata kama ni usiku.

KUBADILISHIWA NEPI

Mtoto anapojisaidia katika nguozake anajisikia vibaya na kukosa uhuru au pengine kuwashwa. Anahitaji kubadilishwa nepi, kuoshwa na kuvikwa upya. Walezi wengi hujisahau kubadilisha nguo hasa usiku, hivyo kumfanya mtoto kulia. Mtoto akilia sana usiku fikiria, huenda amejisaidia na anahitaji kubadilishwa nepi. Nepi zenye mkojo au haja kubwa zinaweza kumsababishia mtoto kuungua ngozi, hivyo ziondolewe kwa haraka.

Mtoto anayelia anahitaji msaada na anatoa mawasiliano kuwa ana shida. Kwa kuwa hawezi kusema wala kuonesha ni nini, unahitaji kuangalia mambo yote ya msingi kama yalivyotajwa ili kujua anasumbuliwa na nini. Ugonjwa wa tumbo una changamoto kubwa zaidi kukabiliana nao na kwa kweli unawasumbua watoto wengi na wazazi pia kwa kuwa hakuna kikubwa ambacho unaweza kufanya kuondoa maumivu kwa mtoto wako.

USHAURI

Mbinu zilizotajwa zinaweza kusaidia kukabiliana na matatizo yanayosababisha mtoto mchanga kulia usiku au mchana. Mtoto akilia sana usiku au mchana mpeleke kwa daktari akampime na kujua tatizo atalitibu.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUMFANYA MWANAMKE AKOJOE HARAKA WAKATI WA TENDO

JINSI YA KUMKOJOLESHA MWANAMKE KWA HARAKA

JINSI YA KUMFANYA MWANAMKE ASIKUSAHAU KATIKA TENDO LA NDOA