KWANINI BAADHI YA WANAWAKE HUOGOPA KUJIFUNGUA??

Mercy Chepkorir Mercy alijifungua mtoto wake kupitia kwa upasuaji wa kuchagua.

Upasuaji wakati mama anapojifungua hufanyika mara kwa mara wakati hali ya mama au mtoto iko hatarini, Lakini katika karne hii ya 21 wanawake wengi ambao ni wajawazito huchagua kufanyiwa upasuaji kwa Imani kwamba kuzaa kwa njia ya uzazi ni uchungu au husababisha njia ya uzazi kupanuka na hivyo kumfanya mama kuachwa na mumewe.

Ni Imani ambazo zimewasababisha wanawake wengi hasaa ambao ni wajawazito na wanatazamia kujifungua mtoto wa kwanza kuogopa kujifungua kwa njia ya kawaida.

Hii ni kutokana na mambo ambayo wao wameyasikia kutoka kwa rika lao ama pia kuyatizama kwenye vyombo vya habari au kwenye mitandao ya kijamii.

Wengi wao wanaamini kwamba kujifungua kwa njia ya kawaida ni uchungu na wasingelitaka kuhisi uchungu huo.

Mercy Chepkorir ni mama wa mtoto mmoja kutoka mjini Nakuru nchini Kenya. Mercy alijifungua mtoto wake kupitia kwa upasuaji wa kuchagua.

"Nilipata ujauzito nikiwa katika chuo cha uuguzi. Mara kwa mara nilikuwa nawaona wamama wajawazito wakiumia, wakilia kutokana na uchungu. Wakati huo ndio niliogopa kuzaa kama kawaida." Mercy alinieleza

"Niliogopa pia uchungu wa muda mrefu ambao ungesababisha nipatwe na Fistula -ugonjwa unaomsababishia mwanamke kushindwa kudhibiti haja ndogo.

Kutokana na mambo aliyoyashuhudia Mercy, uwoga ulimuingia na kumsababisha kuamua kufanyiwa upasuaji wakati alipojifungua.

Kama wasemavyo wahenga uchungu wa mwana aujuae ni mzazi lakini kama wanavyosema watu wengi uchungu wa mwana aujuaye ni mama kutokana na uchungu anaohisi mama wakati wa kujifungua,kulingana na Mercy uchungu huo bado mama aliyejifungua kwa kuchagua upasuaji bado anauhisi wakati wa kutibu kidonda

" Hata wakati unafanyiwa upasuaji, kama ni uchungu bado unahisi . Kutibu hicho kidonda cha upasuaji si rahisi. Kwa sababu wakati huo uko na ugumu wa kufanya kazi, lazima uwe na msaidizi, si kama kwa mtu alyejifungua kwa njia ya kawaida."

Mercy ambaye anapangia kuongeza watoto watatu anasema kwamba bado atachagua kufanyiwa upasuaji kwa sababu kulingana na yeye hakupata changamoto yoyote ambayo ni hadithi za kina mama wengine. Mfano kidonda kuchukua muda mrefu kupona.

Valentine Wanjiru alijifungua watoto watano kwa nji ya kawaida

"Kidonda changu kilipona baada ya muda mfupi sana. Ukitizama mahali ambapo nilikatwa, haikai kama nilifanyiwa upasuaji.."

"Mimi bado nitachagua upasuaji, kwa sababu ninaogopa kuhisi uchungu"

Mbali na uwoga, baadhi ya wanawake huamini kwamba kujifungua kwa njia ya kawaida kunaweza kufanya njia ya uzazi kuwa pana.

Kinyume na hayo, kuna thuluthi ya wanawake ambao wamezaa zaidi ya mtoto mmoja, na kulingana nao hawajashuhudia mabadiliko yoyote.

Valentine Wanjiru ni mama wa watoto tano. Alijifungua watoto wawili nyumbani na wengine watatu hospitalini.

"Sijawahi kufanyiwa upasuaji, watoto wote watano nilijifungua kwa njia ya kawaida"

Kulingana na Valentine, njia yake ya uzazi haijabadilika.

" Sijaona mabadiliko yoyote kwenye mwili wangu kutokana na kujifungua kwa njia ya kawaida. Ukijifungua njia ya kawaida, unarudi katika hali ile ya kawaida, kwa sababu kama ungekuwa unapanuka, mtu angekuwa anakuambia. Kwa hivyo watu wengi huamini hivyo, na si hivyo"

"Siwezi kupenda kufanyiwa upasuaji kwa sababu unawekewa alama, kukatwa mahali... huwa si vizuri, ni vile tu watu wanaamini lakini si sawa."

Hata hivyo Valentine anashauri kwamba kufanyiwa upasuaji wakati ambapo wa dharura ni sawa.

" kuna mwingine anawezashindwa kusukuma mtoto,mwingine misuli zake zinakataa kufunguka, njia ya uzazi inakataa kufunguka , hiyo inaweza kusema ni sawa mtu afanyiwe upasuaji lakini kama mtu anaweza jifungua kupitia njia ya kawaida, ajifungue tu kupitia njia ya kawaida"

Eunice Chebet, Daktari wa wanawake

Shirika la afya duniani WHO linapendekeza kwamba upasuaji wakati wa kujifungua kina mama unapaswa kufanywa wakati ambapo unahitajika kiafya.

Hii ni kumaanisha kwamba upasuaji huo unapaswa kufanywa wakati mama na mtoto wako katika hatari ya kupata maambukizi au hata kifo.

Pia wanapendekeza kwamba upasuaji wa mara kwa mara kwa mama aliye na ugonjwa wa Ukimwi si sawa.

Eunice Chebet mhudumu wa afya kutoka hospitali ya Kakamega magharibi mwa Kenya anasema kwamba visa hivyo ni vingi siku hizi.

" Kina mama wengi sikuhizi huchagua upasuaji. Mgonjwa anaruhusiwa kufanya uamuzi wake. Mgonjwa akikueleza sababu ambayo inamfanya kutaka kufanyiwa upasuaji, huwa anafanyiwa upasuaji. Wengi wao husema kwamba hawataki kuhisi uchungu kutokana na kile ambacho amesikia kwa watu."

Upasuaji huu unakubalika katika vituo vyote vya afya lakini shirika la afya linatoa mwongozo kwa mazingira ambayo upasuaji unapaswa kufanyika. Kwamba kabla kumfanyia mama upasuaji mhudumu wa afya anapaswa kumuelezea na kumuelewesha mama athari za kufanyiwa upasuaji na kuwapa fursa ya kufanya uamuzi ili kuzuia upasuaji usiyohitajika.

"Huwa tunawashauri kina mama , tunawaambia uzuri wa kufanyiwa upasuaji na uzuri wa kuzaa kawaida.Mara nyingi wengine hufika mahali na kubadilisha mawazo kwa sababu awali hawakupata watu wa kuwaeleza kwamba mara wanapofanya upasuaji wana athari ya kuzaa watoto wengine kwa njia ya upasuaji,au kutibu kidonda ambacho wakati mwingine kinaweza patwa na maambukizi kutokana na mazingira chafu au uchungu kwenye tumbo. Unapowaeleza waelewe wengi wao hubadi nia." Alieleza Eunice.

Kulingana na Mercy, upasuaji uko na athari nyingine kama vile kupata maambukizi kwenye kidonda, kukaa hospitalini kwa muda mrefu au kufuja damu nyingi.

Hata hivyo amekana madai kwamba kujifungua kwa njia ya upasuaji husababisha njia ya uzazi kupanuka na kupelekea mama kuachwa na mumewe.

"Wengine husema wakizaa kwa njia ya kawaida, njia ya uzazi hupanuka, ambayo si kweli, kwa sababu wakati wa kuzaa misuli hupanuka na punde tu unapojifungua, misuli hurudi kawaida. Pia kuna mazoezi ya kufanya ambayo husaidia hayo misuli kurudi hali ya kawaida kwa muda mfupi. "

Mwaka jana utafiti uliochapishwa kwenye jarida la kimatabibu la Lancet ulionyesha ongezeko la upasuaji wakati wa kujifungua kutoka asilimia 12% mwaka wa 2000 hadi 21% mwaka wa 2015.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUMFANYA MWANAMKE AKOJOE HARAKA WAKATI WA TENDO

JINSI YA KUMKOJOLESHA MWANAMKE KWA HARAKA

JINSI YA KUMFANYA MWANAMKE ASIKUSAHAU KATIKA TENDO LA NDOA