EPUKA JAMBO HILI KATIKA MAISHA YAKO

Dunia huwa inatupa kile tunachokitaka na tunakizungumzia kila mara katika midomo yetu. katika jamii zetu kulalamika ndiyo utamaduni uliozoeleka, ukienda ofisini watu wanalalamika, kwenye usafiri watu wanalalamika, kwenye nyumba za ibada watu wanalalamika. Hivi ni eneo gani la maisha yako umeona sehemu ambayo watu hawana utamaduni wa kulalamika?

Binadamu tumekuwa ni watu ambao tumekosa shukrani, hata tupewe nini hatuwezi kukosa shukrani. Tunajiona hatuna kitu fulani kwa sababu maisha yetu tumeyaweka katika vitu, tunaishi kwa ulinganishi wa vitu na pale tunapojaribu kulinganisha tunajikuta tunaumia na hatuna kitu.

Hakuna mtu ambaye amejitosheleza kwa kila kitu, tunatakiwa kushukuru kwa kile ambacho kipo ndani mwetu, tusiangalie tumekosa nini, badala yake tukumbuke tumepata nini, tukiwa tunaangalia vile ambavyo tunavyo maisha ni mazuri sana lakini tukiwa tunaangalia vile ambavyo hatuna maisha yanakuwa siyo mazuri sana.

Tunapoteza maana ya maisha yetu pale tunapokuwa tunajilinganisha na watu wengine. maisha yako ni maisha yako, yapende na yafurahie kwa sababu hakuna mtu mwenye maisha mazuri kama wewe hapa duniani.

Rafiki, siku hii ya leo fanya zoezi la kutolalamika na badala yake fanya zoezi la kushukuru tu, shukuru kwa kile ambacho unacho na siyo kile ambacho huna. Furahia kwa kile ambacho kipo mkononi mwako na usitegemee kile ambacho hakipo mkononi mwako, kitegemee pale ambako tayari umekuwa nacho mkononi lakini vinginevyo hapana.

Kulalamika ni roho ya umasikini, utamaduni wa kulalamika una haribu dunia yetu, tumekuwa na jamii ya watu wanaolalamika kwenye kila  eneo la maisha watu wanaolalamika wapo. Dunia ina uhaba wa watu wanaoshukuru ndiyo maana leo nakusihi sana fanya zoezi la kushukuru tu na kufurahia kwa yale ambayo Mungu amekujalia katika maisha yako.  sherekea kwa kile ambacho unacho, jione wewe ni wa kipekee na umebarikiwa kuliko watu wote.

Tunaondoa Baraka katika maisha yetu kwa sababu ya kulalamika. Tunajiona ni watu tulioonewa, hivyo tunaona kulalamika ndiyo njia kuu ya kupata kile tunachotaka. Tunapolalamika tunapoteza nguvu na muda hivyo ni bora kukaa kimya kama umeshindwa kuchukua hatua ya kukibadilisha kile unachotaka kiwe.

Ukiwa unahisi dunia imekutenga, una mawazo hasi basi na mara nyingi utajikuta maisha yako yanafanana na mawazo ambayo yako akilini mwako.  Usijiwazie mabaya wala kulalamika, kila siku jione mtu aliyebarikiwa kwenye kila eneo la maisha yako.

Hatua ya kuchukua leo; jione wewe ni mshindi, jitamkie maneno chanya na vunja laana ya kulalamika, unapolalamika juu ya kitu fulani unakuwa unajizibia Baraka eneo hilo, hutaona mazuri bali mabaya tu.

Kwahiyo, maisha ni mazuri kama tukiwa ni watu wa kushukuru kwa vile ambavyo tunavyo na siyo kulalamika kwa vile ambavyo hatuna.

Kumbuka, ulichonacho kinatosha kama ukifikiria vya kutosha.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUMFANYA MWANAMKE AKOJOE HARAKA WAKATI WA TENDO

JINSI YA KUMKOJOLESHA MWANAMKE KWA HARAKA

JINSI YA KUMFANYA MWANAMKE ASIKUSAHAU KATIKA TENDO LA NDOA