HATUA 6 ZA KUCHUKUA ILI KUANZISHA MAHUSIANO MAPYA


Kuanza mahusiano mapya mara tu baada ya kuachika au kuachana na mwenzi wako ni jambo ambalo linahitaji umakini wa hali ya juu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, kukurupuka kuanzisha mahusiano mapya nijambo ambalo laweza kukupelekea kua mtu wa kubadilisha wapenzi mara kwa mara.

Kuachana kupo, matatizo yanatokea, lakini, kwa kuendekeza mambo ya kukurupuka mtu anawez jihisi ana mkosi kwamba hadumu katika mahusiano, kumbe tatizo lipo katika mfumo wake mzima wa kujiingiza katika mahusiano.

Wengi, wanapotaka kuanzisha mahusiano mapya huwa na uwoga, kwamba makosa yasijirudie, au wengine huofia kupotezewa muda. Hivyo huwa wanajiuliza, waanzishe mahusiano mapya, au wapotezee kwani ni mapema sana.

Ukweli ni kwamba hakuna wa kukulaumu kwa uamuzi wowote utaochukua sababu ni mambo yanayoeleweka, mapenzi hayana fomula. Na wengi hujiuliza nisubiri muda gani ili kuanzisha mahusiano mapya, ukweli ni kwamba hakuna muda maalum. Mambo yote hutegemea utayari wako.

Makala hii itakujuza mambo ya kufanyawakati wa kuanzisha mahusiano mapya, mara tu baada ya kutoka kwenye mahusiano mengine kama ifuatavyo;

Hakikisha upo tayari kuingia katika mahusiano mapya

Tafakari, amua, hii ni sababu kukurupuka kunaweza kukufanya  ukaingia katika mahusiano sababu tu ya upweke hali ya kua nafsi yako haipo tayari.

Kuwa na mtazamo chanya

Epukana na ile hali ya kujihisi kwamba wewe ni mkosefu, una mapungufu, kwamba hata mahusiano mapya utaharibu. Au kwa upande mwingine kuwaza kwamba, huyo uliyempata anakupotezea muda tu, hana nia njema na wewe sababu mambo hayo yatakusababishia matatizo kwani hutajiweka huru kwa mwenza wako. Ukiwa na mtazamo chanya utafurahia mahusiano.

Usimfananishe mpenzi wako mpya na wazamani

Ingawa utakua unatarajia mambo mazuri zaidi kwa mpenzi wako mpya ambayo pengine hukuwahi fanyiwa na mpenzi wazamani, epukana na hiyo hali.kufanya hivyo kutakupelekea kushindwa kumfahamu mpenzi wako kiundani na kushindwa kufahamu mambo mazuri ya kipekee aliyonayo na mwisho wa siku kutofurahia mahusiano, maana utajikuta unakua unaatishwa taamaa tu.

usifanye pupa

Mara nyingi tunaingia katika mahusiano na kutaka mambo yaende haraka haraka, yaani ile furaha ya kua katika mahusiano mapya inaweza kutuponza. Unajikuta unachukulia mahusiano mapya kama tiba ya kupona maumivu na mumsahau mwenzi wako wa zamani. Jitahid kuchukua muda kumjua mwenza wako na kukataa baadhi ya mambo inapobidi.

Fanya mambo mengine

Mnapokua katika mahusiano ni vyema mkafanya mambo mengine madogo madogo ya kuimarisha mahusiano yenu. Mnaweza kuenda angalia movie, kufanya shopping pamoja, kutembea pamoja kijua kikitulia au hata kujichanganya na marafiki zenu. Hii itawaongezea ukaribu, na pia mwisho wa siku mtakua na matukio ya kukumbukana. Sio mjikute hata kumbukumbu nzuri hamna.

Kujiwekea malengo yenye ukweli

Malengo ya ukweli, ni malengo ambayo yanaweza yakatekelezeka. Licha ya kuwa si vizuri kuwa na mategemeo kupita kiasi kutoka kwa mwenzio maana naye ni binaadamu, si mbaya kuweka baadhi ya malengo. Kutokua na malengo au mategemeo yoyote kunaweza mfanya mwenzii wako akuchukulie poa. Ila hakikisha malengo yako yana uhalisia ndani yake, sio ndoto za Alinacha.

Ni hayo tu kwa leo, tujulishe kwenye koment mambo gani mengine ya kufanya unapoanzisha uhusiano mpya mara tu baada ya kuachana na mwenza wako wa zamani.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUMFANYA MWANAMKE AKOJOE HARAKA WAKATI WA TENDO

JINSI YA KUMKOJOLESHA MWANAMKE KWA HARAKA

JINSI YA KUMFANYA MWANAMKE ASIKUSAHAU KATIKA TENDO LA NDOA