JE, WAJUA MAANA HALISI YA NDOA??

Ndoa ni muunganiko wa watu wawili wenye nia ya kuishi pamoja kwa maisha yao yote. Pia ni muungano wenye malengo ya kujenga familia pamoja na kuiongoza kwa namna ambavyo itakuwa bora kwao kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.

Hata biblia inasema "Ndoa ni muunganiko wa mwanaume na mwanamke kuwa mwili mmoja ikiwa kwa mtazamo wa nje tunawaona wao ni wawili" (Mwanzo 2:24).

Kwa ujumla Ndoa ina maana zifuatazo;
Ndoa, ni kujitoa muanga kumpokea mwenza wako wa ndoa katika maisha ya aina yoyote yale, ya taabu na raha, na kila ndoa ina taabu zake na pia ina raha zake, hili halikwepeki.

Ndoa, ni maisha ya kuvumiliana na kuchukuliana msalaba, katika mtazamo wa kikristu ninaweza sema, mume anakubali kubeba msalaba wa mke wake na mke anakubali kubeba msalaba wa mume wake kila siku za maisha yao.

Ndoa, ni kujitoa kumpenda mwenza wako siku zote za maisha yako na kuweka moyo wako kwake na kila siku lazima ujiulize nimefanya jambo zuri kwa mume au mke wangu.

Ndoa, ni kuishi maisha ya kushirikiana na kusaidiana kwa kila jambo, hakuna jambo dogo au kubwa katika ndoa, kila jambo lina umuhimu katika ndoa.

Ndoa ni maisha ya kuheshimiana na kujaliana hisia. Maisha ya ndoa ya vitendo zaidi kuliko maneno, hivyo lazima kujifunza kusoma ishara na kutambua kile mwenza wako anachomaanisha hata kabla hajasema. Kwa sababu siyo kila wakati mwenza wako ataongea na wewe kwa maneno muda mwingine atatumia lugha ya ishara na vitendo.

Ndoa ni kuungana, ndoa siyo “part-time” leo upo na mume wako kesho na mtu mwingine au mwanaume mwingine, ndoa ni kukubali kufarijiawa na mwenza wako wa ndoa kwa kila jambo.

Ndoa, ni maisha Mapya ya kutimiza wajibu wa ndoa, wajibu wa familia na wajibu wa muunganiko na hili siyo kadili unavyotaka bali ni wajibu wa lazima, kama huna uhakika, isijaribu kucheza na ndoa.

Ndoa siyo majaribio ya kuangalia kama unaweza kuishi na mwanaume au mwanamke mmoja, ndoa ni maisha ya kujitoa kikamilifu bila kujibakisha na kuunganika na mwenza wako kimawazo, kihisia, kimahaba, kimapenzi na zaidi ya yote katika upendo.
Ndoa siyo fashion ya nguo au kuburudisha watu, ndoa ni agano la kuishi maisha matakatifu na mume au mke wako, mbele ya jamii na zaidi mbele ya Mungu, ukiishi kikamilifu katika ndoa na kufuata agano mliloweka.

Usiingie katika ndoa kama hauna uelewa wa kutosha nini maana ya ndoa, ndugu zangu ni wakati wa kuamka tujifunze kwa undani nini maana ya ndoa na nini maana ya kupenda, tusiishi kwa mazoea, ulimwengu umebadilika lazima kurudi katika busara za wazee wetu na katika maandiko matakatifu kutafakari kuhusu uchumba na maisha ya ndoa.

Nashukuru kwa kuwa nami katika makala hii.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUMFANYA MWANAMKE AKOJOE HARAKA WAKATI WA TENDO

JINSI YA KUMKOJOLESHA MWANAMKE KWA HARAKA

JINSI YA KUMFANYA MWANAMKE ASIKUSAHAU KATIKA TENDO LA NDOA