IFAHAMU SIRI YA KUPATA USINGIZI MZURI USIKU

Mzunguko wa kulala na kuamka ni miongoni mwa tabia za mwanadamu.

Huwa tunatumia muda mwingi kulala katika maisha yetu na hatuwezi kuishi bila kulala.

Tunapolala, ubongo wetu unapata wakati wa kutunza kumbukumbu na kufanyia kazi taarifa ilizonazo.Ni muda ambao sumu au uchovu uondoka katika miili yetu na kuturuhusu kufanya kazi vizuri tunapoamka.

Hata muda mdogo ambao mtu anaweza kulala una faida katika afya zetu.

Wengi wetu huwa tunadhoofika tukikosa usingizi hata wa usiku mmoja, na tukikosa usingizi kwa usiku tatu lazima utendaji wa kazi kuwa chini ya kiwango.

Katika utafiti mmoja ambao ulisema kuwa mara baada ya saa 17 hadi 19 mtu anapokaa macho bila kulala anakuwa sawa na mtu ambaye amekunywa sana na kulewa.

Madhara ya ukosefu usifu wa usingizi huwa yanaongezeka kadri muda unavyoongezeka.

Ukosefu wa usingizi unaweza kusababisha tabia ya mtu kubadilika na kutokuwa makini lakini vilevile kuwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu.

Ingawa wanasayansi wamekuwa wanaelewa umuhimu wa mtu kupata usingizi wa kutosha, lakini walikuwa hawaelezi kuhusu mwanga ambao mtu anaweza kuupata akiamka.

Jitengenezee saa katika mwili

Sababu inayofanya mwanga kuwa jambo muhimu ni katika kutengeneza saa ya mwili,

Macho yetu huwa yanahisi katika mazingira ya mwanga na giza na yanaweza kuuelekeza mwili kile ambacho inataka kufanya ndani au nje.

Nguvu hii kubwa ambayo watu wanayo katika macho wanaweza kuitumia vizuri kama wataweza kuondokana na tatizo la usingizi.

Bila ya upatikanaji wa mwanga wa aina yeyote, saa ya mwili wa binadamu huwa inaenda taratibu kwa kuongeza nusu saa katika mzunguko wa saa 24 katika kila siku ambayo ina giza.

Mwanga huwa unatusaidia kuuelekeza miili yetu katika saa za eneo husika tuliopo, kwa kutuambia sasa ni muda sahihi wa kulala au kuamka.

Watu wengi duniani kote huwa wanafanya kazi kwa kutegemea mabadiliko ya muda wa usiku au mchana.

Tumekuwa viumbe ambavyo tunategemea mwanga katika maisha yetu. Hivyo ili kupata usingizi mzuri na kuwa na afya nzuri lazima ajue muda ambao anapaswa kupata mwanga.

Nchini Uingereza, tatizo la sonona limewaathiri asilimia 2-8 ya watu kwa ukosefu wa mwanga wa jua.

Kuna wengi huwa wanakosa mwanga asilia na kupata madhara.

Kufanya kazi usiku

Ikiwa wengi wetu huwa hatupati mwanga wa kutosha ambao ni asilia haswa kwa wale ambao huwa wanafanya kazi wakati wa usiku.

Watu ambao wanafanya kazi wakati wa usiku huwa wanafanya kazi wakati ambao saa ya mwili inajiandaa kulala na hata huwezo wa kufanya kazi unakuwa mdogo.

Hata kama watajaribu kulala mchana lakini mara nyingi huwa wanalala kidogo na hawawezi kupata usingizi mzuri kama ambao wangeweza kuupata usiku.

Na matokeo yake ni kufanya kazi wakiwa na usingizi na kupata madhara ya kiafya.

Baada ya muda mfupi wa kukosa usingizi ipasavyo , mwili huanza kushindwa kufanya kazi vizuri na hata taarifa inashindwa kupokelewa kwa uhakika.

Wataalamu wanasema athari za kiafaya zinazotokana na kazi za usiku za muda mrefu zinaweza kupunguza miaka sita ya mtu kuishi.

Huku asimilia 97 ya wafanyakazi wa usiku wameshindwa kukabiliana na mfumo wa kazi yao bila kujali miaka mingi kiasi gani wamekuwa wanafanya kazi hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUMFANYA MWANAMKE AKOJOE HARAKA WAKATI WA TENDO

JINSI YA KUMKOJOLESHA MWANAMKE KWA HARAKA

JINSI YA KUMFANYA MWANAMKE ASIKUSAHAU KATIKA TENDO LA NDOA