Afariki Dunia Akidungwa Sindano ya Kuongeza Makalio ili Kuwanasha Wanaume

Daktari mmoja nchini Marekani, Donna Francis ameshtakiwa mara baada ya kusababisha kifo cha mwanamke wa miaka 34 aliyekuwa anamfanyia upasuaji wa kuongeza makalio.

Donna Francis amekiri mashtaka ya mauaji hayo yametokana na uzembe hali iliyopelekea daktari huyo kufungiwa leseni yake ya kufanya shughuli za kitabibu.

Alifanya upasuaji huo wa kuongeza maumbile kwa mwanamke huyo mnamo Mei, 2015, ambapo wakati wa upasuaji mgonjwa alipatwa na mshtuko wa moyo uliopelekea kupoteza uhai wake.

Inaelezwa kuwa kifo cha mwanamke huyo kilisababishwa na dawa ya kuongeza maumbile ambayo alichomwa sindano na daktari wakati wa matibabu.

 Upasuaji huo ulimgharimu dola 16000 sawa na milioni 2 na zaidi kwa pesa ya kitanzania kwa ajili ya kuchomwa sindano hiyo ambayo ingemsaidia kuongea makalio, lakini bahati mbaya mara baada ya kudungwa sindano hiyo alipata mshtuko wa moyo na kupoteza maisha.

 Aidha, imekuwa utamaduni wanawake wengi karibu duniani kote kufanya upasuaji wa kuongeza au kupunguza baadhi ya sehemu zao za mwili hasa sehemu za makalio, matiti na kadhalika.

Japo yapo madhara mengi yanayotokana na mtindo huu wa maisha ambapo madhara hayo yanaweza kuwa ya muda mrefu au muda mfupi.

Tanzania wapo wadada ambao wamesafiri nje ya nchi na kutumia gharama nyingi sana kubadilisha mionekano yao kwa kuiongeza au kuipunguza kwa lengo la kuongeza mvuto zaidi.

Japokuwa teknolojia inakuwa na huu utamaduni wa kuongeza makalio unaweza ukaenda ukifa mara baada ya kugundua nguo za ndani ambazo tayari zimewekwa makalio bandia na hatua hii ni kufuatia madhara makubwa yatokanayo na kuongeza vitu bandia mwilini.

Post a Comment

0 Comments