Kwa Nini Ujiuwe Kisa Mapenzi eti Umemsomesha na Wazazi Wake Wasemaje?


Kuna mambo ambayo unatakiwa kuyatafakari katika maisha yako ya kila siku hivi upo tayari kifo chako kisababishwe na mapenzi.

Ifike wakati tuwe tunafanya maamuzi ambayo yana faida. Hivi unapotaka kujiua kisa mwanamke wakati unafikiria hayo jiulize wazazi wako walipokutoa.

Ni kweli wakati mwingine changamoto za mahusiano zinatesa lakini sio kufikia maamuzi ya kujiua ama kumuua mwenzako.


Kuna mambo ya msingi ya kuyakubali katika maishani kuachwa sio issue ya kukufanya ujiue.

Kwani kukataliwa katika mahusiano haina haja ujichukie ama kumuua aliyekukataa chukulia ni moja ya changamoto za maisha unazopitia.

Unataka kuniambia katika maisha yako hujawahi kupitia changamoto ngumu je hivi kila mtu akisema ajiuwe kupitia matatizo anayopitia hivi atabaki nani humu duniani.

Nataka nikuelimishe jambo moja sio kila changamoto ni kuanza kujutia nyingine zinakwenda kutengeneza baraka kwako na kukutoa sehemu ulipo na kukupandisha viwango.



Ukikataliwa muambia Mungu nashukuru kwa kila jambo huenda mungu anakutengeneza mke wako huyo angeweza kukutesa maisha yako.

Sio wakati wa kuanza kumng’ang’ania umezungumza naye hataki kubadilisha mawazo yake muambie umekubaliana na uamuzi wake.

Mapenzi yanaumiza asikuambie mtu lakini isifikie wakati unataka kutoa roho ya mwenzako kisa amekukataa haijalishe vitu ulivyomfanyia.



Mbona wazazi wenu wanawafanyia kila kitu na ukipata hela zako unamuona mke ni zaidi kuliko wazazi waliokusomesha. Mbona mzazi hasemi anakuua kwa vile amekusomesha na hujataka kumthamini.

Kuna baadhi ya watu wameachwa na mimba na hawajajiua unataka kusema hawana maumivu au hawajui kupenda mbona maishani yanakwenda.

Tujifunze kukubalinana na kile ambacho kinatokea katika maisha yako na kuzitumia changamoto kama ni fursa ya kukuvusha katika hilo jaribu.

Pia unapopata changamoto ya kimaisha usikae kimya tafuta mtu wako unayemuamini na kuongea naye usikae kimya huku ukiendelea kuumia.



Muambie mwenzako akushauri maana ukijifungia ndani mwenyewe huku unawaza utajikuta unachukua maamuzi ambayo sio sahihi.

Usiwe mwepesi wa kutoa roho yako kisa unapitia magumu hilo ni jaribu utalivuka jitahudi kuwa karibu na watu na kuomba ushauri.

Mwingine kisa kamsomesha mpenzi wake na baada ya muda akamkataa basi unataka kumuua hayo sio maamuzi mazuri.

Kumbuka huyo binti amesomeshwa na wazazi wake na ni tegemeo la wazazi wake hivyo haina maana kuitoa roho yake.



Pia wanawake wenzangu kama unajijua mwanaume hauna malengo yake ni vizuri ukaachana naye mapema kabla ya kumsababishia maumivu.

Post a Comment

0 Comments