Mlela aanika pesa anayotumia kwa Ebitoke

Muigizaji mkubwa wa Bongo Movie, Yusuph Mlela ameweka wazi kiasi cha pesa anachotumia kwa mpenzi wake wa sasa, Ebitoke pamoja na stori za kuishiwa pesa kuwa ndiyo sababu iliyomfanya kuwa na mwanadada huyo.

Mlela amesema hayo kupitia Enewz ya EATV, ambapo kuhusiana na kiasi cha pesa anachotumia kwa Ebitoke, amesema kuwa huwa hana kiwango maalumu lakini mara nyingi huanzia Shilingi laki 1 au 2.

"Kwa kawaida natumia gharama ya laki 1 au laki 2 ni kawaida tu kulingana na kitu tunachokitaka na inaweza kufika hadi milioni kwa sababu mambo yamebadilika sasahivi anafanya mambo makubwa", amesema.

Kuhusu stori za kuchunwa na wanawake wenye gharama kuwa ndiyo sababu iliyompelekea kumfuata Ebitoke, Mlela amesema, "mimi nimefanya sanaa kwa miaka 14 sasa, nimewekeza vya kutosha. Nimefanya 'project' za kimataifa kama Kenya na hapa nchini kwahiyo mimi siyo marioo"

Post a Comment

0 Comments