LIKE Mother Like Daughter! Unaweza sema hivyo baada ya mama mzazi wa rapa wa kike anayekimbiza kunako Muziki wa Hip Hop kutoka Marekani, Nicki Minaj, Carol Maraj kutangaza kuingia rasmi kwenye muziki.
Mama huyo wa Nicki ambaye kwa muda mrefu alikuwa nyuma ya mafanikio ya mwanaye kwa kumpa sapoti kwenye kazi zake, ameshaingia studio na kuutambulisha wimbo wake mpya wa What Makes You. Carol Maraj ametangaza pia mpango wa kuja na albamu baada ya kuungwa mkono kwa 100% na Nicki.
0 Comments