WANAUME WASHAURIWA KUTOKULA CHIPS

Wataalamu wameshauri wanaume nchini waache kula vyakula vilivyokaangwa zikiwemo chipsi, baga, unywaji wa pombe, uvutaji sigara.

Wameshauriwa wale zaidi vyakula aina ya njugu kama vile karanga, korosho, mbegu za maboga na jamii ya aina hiyo ili kuimarisha mbegu zao za uzazi.

Wamesema, wanaume pia wanapaswa kula vyakula visivyokobolewa, matunda, mboga za majani, samaki, nyama na kuepuka vyakula vya mafuta mengi ili kuimarisha viungo vyao vya uzazi.

Utafiti Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam kuonesha asilimia 24 ya wanaume wana tatizo la nguvu za kiume kutokana na uchafuzi wa mazingira, uvutaji sigara na aina za vyakula.

Wataalamu wamesema kuna ushahidi kuwa ulaji wa chakula bora unasaidia masuala ya uzazi na kwamba karibu pea moja ya wenza kati ya saba ina ugumu katika kushika mimba na asilimia 40 hadi 50 ya tatizo ni wanaume.

Daktari wa tiba na lishe viwandani, Sweetbeth Njuu amesema vyakula jamii ya njugu hupunguza hatari ya mtu kupata magonjwa ya kisukari, moyo, shinikizo la damu la kupanda, na saratani ya utumbo. Dk Njuu amesema, magonjwa hayo kwa kiasi fulani huchangiwa na sumu zinazojikusanya mwilini.

Amesema, njugu zina virutubisho na madini ambayo hupunguza sumu zinazochangia kupata magonwa hayo.

"Upungufu wa nguvu za kiume unachangiwa na kutokula lishe bora vyakula vinavyojenga mwili kama mboga mboga, nyama, mayai, maziwa na vyakula vinavyoongeza nguvu kama ugali wa dona, muhogo na matunda ya aina mbalimbali kama nanasi, tikiti maji, ndizi mbivu, chungwa, matango na mengine watu hawali kwa mpangilio," alisema.

Kwa mujibu wa Dk Njuu, njugu zina mkusanyiko wa virutubisho vingi hasa protini, wanga, mafuta ya omega-3, na omega -6, madini, vitamins na vitoa sumu mwilini.

"Mazoezi nayo ni changamoto, kwa sababu ya mfumo wa maisha, unakuta mtu anakosa hata muda wa kufanya mazoezi ambayo yanasaidia pia kumwimarisha, hivyo unawaathiri pia,"amesema.

Amesema pia msongo wa mawazo ni chanzo kikuu cha upungufu wa nguvu za kiume kwa kuwa tendo la kujamiana linahitaji utulivu wa akili ili uweze kuridhishana na kulifurahia tendo hilo.

Post a Comment

0 Comments