Vyakula vya asili vinavyoongoza nguvu za kiume kwa haraka

Katika makala hii tutasoma juu ya vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume kwa haraka zaidi na nitakueleza chakula kimoja baada ya kingine kiundani zaidi.

Unachotakiwa ni kujijengea mazoea ya kuhakikisha mlo wako kwa siku haukosi hivi vyakula. Ukiwa mbunifu kwenye kupika kuna uwezekano ukatumia vyote au nusu yake katika chakula chako cha kutwa nzima

Vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume

NDIZI –

Wakati unafikiria uwezo wa kufanya vema tendo la ndoa unatakiwa kuwaza juu ya uimara wa misuli ya mwili ambayo inatajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye muhimu katika kujamiiana.

Kwa msingi huo ulaji wa ndizi mbivu unatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini na kumfanya mtu aweze kuwa hodari katika tendo la ndoa.

Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamini B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito.

Ndizi ina kimeng‟enyo cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume na ashki ya mapenzi (libido).

Ndizi ni tunda zuri na tamu sana, lina potasiamu na vitamini B kwa wingi viinilishe ambavyo ni mhimu ili kuamsha hamu ya tendo la ndoa na uzalishwaji wa homoni ya „testosterone‟ kwa ujumla.

Ndizi huongeza nguvu ya mwili kwa ujumla ikiwemo nguvu za kushiriki tendo la ndoa kwa wanaume pia kwa wanawake.

Kula ndizi 2 hadi 3 zilizoiva kila siku.

2. TIKITI MAJI –

Tikiti maji ni tunda mhimu sana kwa kulinda ndoa na inatakiwa walau kwa siku upate vipande viwili au vitatu na sasa yapo kwa wingi ushindwe wewe na ni muhimu ukala na mbegu zake kwani ndizo ambazo huwa na nguvu za kiume.

Tunda hili lina faida nyingi pamoja na kuwa ni chanzo kikuu cha Protini, Mafuta, Nyuzinyuzi, Wanga, Calcium, Phosphorus, Chuma,Vitamini A, B6, na C.

Viinilishe vingine kwenye tikiti maji ni pamoja na Potasium, Magnesium, Carotene, anthocyanins na Virutubisho vingine vingi.

Tunda hili linasaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kuimalisha misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kukuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la juu la damu.

Tikiti maji linasemwa kuwa ni mkuyati wa asili pia kama lilivyo parachichi. Kwenye tikiti maji kuna vitu hivi vitatu mhimu sana kwa afya ya mapenzi navyo ni „lycopene‟, „beta-carotene‟ na „citrulline‟ ambavyo husaidiwa kuweka mishipa ya damu katika hali ya utulivu.

Tikiti maji ni viagra ya asili inayoweza kutumika kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa watu wa jinsia zote mbili bila kukuacha na madhara yoyote mabaya.

Faida nyingine 12 za tikiti maji kiafya ukiacha hii ya nguvu za kiume ni pamoja na:

Asilimia 92 yake ni majiVitamini A ndani yake huboresha afya ya machoVitamini C ndani yake huimarisha kinga ya mwili,Huponya majeraha,Hukinga uharibifu wa seliHuboresha afya ya meno na fizi•  Vitamini B6 husaidia ubongo kufanya kazi vemaHubadilisha protini kuwa nishatiChanzo cha madini ya potasiamuHusaidia kushusha na kuponya shinikizo la damuHurahisisha mtiririko wa damu mwiliniHuondoa sumu mwilini

Kula tikiti maji kila siku huku ukitafuna na zile mbegu zake, fanya hivi mara kwa mara.

3. KITUNGUU SWAUMU –

Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.

Sifa kuu za kitunguu saumu zinazokifanya kuwa na uwezo na faida nyingi mwilini ni kuwa na viasili kadhaa ambavyo vina uwezo tofauti tofauti.

Baadhi ya viasili hivi husaidia kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation kwa lugha ya kiingereza) kwa kubadilisha polysulphides zilizo ndani yake

kuwa hydrogen sulphides kwenye seli nyekundu za damu.

Pia, kitunguu saumu husaidia kuthibiti kiwango cha kemikali

iitwayo homocystine mwilini na hivyo kupunguza madhara ya kisukari.

Kitunguu saumu kina allicin, kiambato ambacho husaidia mwili kuwa na mzunguko mzuri wa damu hadi kwenye viungo vya uzazi.

Kuwa na damu ya kutosha katika uume husababisha hiki kiungo kusimama na hivyo kustaimili tendo la ndoa kwa muda mrefu.

Namna ya kutumia kitunguu swaumu:

1. Chukuwa kitunguu swaumu kimoja

2. Kigawanyishe katika punje punje

3. Chukua punje 6

4. Menya punje moja baada ya nyingine

Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10

6. Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala.

Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.

Fanya hivi kila baada ya siku 1 unapoenda kulala kwa wiki 3 mpaka 4.

Unaweza pia kuendelea kukitumia hata kama umepona tatizo lako.

Ukiona kichwa kizito au kinauma pumzika kutumia kitunguu swaumu kwa siku 3 hivi kisha endelea tena, mhimu usitumie kila siku bali ni kila baada ya siku 1

Imehaririwa mara ya mwisho 20 May, 2019 Saa 2:33 am

Post a Comment

0 Comments