NA JEREMIA ERNEST
MLINZI binafsi wa msanii Harmonize, Mudy Mnyama ambaye pia ni mwigizaji wa filamu, amesema anatumia shilingi 1,000,000 kila mwezi ya mazoezi ya kuimarisha mwili wake wa miraba minne.
Akizungumza na Papaso la Burudani jana, Mudy Mnyama alisema hiyo ndiyo siri ya kuwa tofauti na walinzi wengine binafsi wanaowalinda wasanii kwani mwonekano wake umekuwa wa kipekee.
“Natumia shilingi milioni moja kwa ajili ya kufanya mazoezi kama sitojibana sana, nafanya hivyo kutumia gharama kubwa ili kulinda ‘brand’ (nembo) yangu ili kujiweka tofauti na wengine,” alisema Mudy.
0 Comments