PENNY ATOBOA SIRI YA NDOA YAKE

Mtangazaji wa Kipindi cha Harusi Yetu kupitia Runinga ya Magic Swahili, Penieli Mwingilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa anapenda kuona watu wakivalishana kwake lakini kwa upande wake hajawa tayari kwakuwa hapendi kabisa kuingia katika ndoa.

 Penny amesema kuwa, moyo wake bado hauko tayari kuingia kwenye ndoa kwa sasa mpaka atakaporidhia hapo baadaye.

“Nafanya kipindi cha harusi, lakini huwezi amini napenda sana kuona watu wakioana na kuvaa mashela vile lakini mimi sipendi kabisa kuingia kwenye ndoa. Nafsi yangu inaona wazi bado haihitaji ndoa,” alisema Penny.

(Visited 1 times, 1 visits today)

Post a Comment

0 Comments