JAMAA ADAI MTU ASIYEJULIKANA ALIINGIA CHUMBANI KWAKE AKAFANYA USAFI KISHA KUONDOKA

Jamaa kutoka Massachusetts, Marekani alipatwa na mshtuko baada ya kurejea nyumbani na kupata nyumba yake ikiwa imenadhifishwa.

Katika ukurasa wake wa Facebook, Nate Roman alisema kuwa, hamna chochote kilichoibwa ila mtu huyo alisafisha vyumba vyote na hata bafu kabla ya kuondoka.

Roman Nate alisema alirejea nyumbani kwake na kupata imenadhifisha na mtu asiyejulikana. Picha: Roman Nate/Facebook. Source: Facebook

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May athibitisha kujiuzulu, kuondoka afisini Juni 7

Kabla mtu huyo kuondoka, alitandika vitanda, akasugua vyoo na kuunda ua akitumia tishu kabla ya kutoweka.

Roman hata hivyo alishuku huenda mtu huyo aliingia katika jumba lake akitumia mlango wa nyuma ya nyumba kwani alikuwa amesahau kuufunga akiwa katika harakati ya kuelekea kazini.

"Nilisahau kuwasha kamera zangu fiche na hivyo basi sina video yoyote ya tukio hilo. Hamna mahali popote palivunjwa wakati mtu huyo akiingia katika nyumba yangu," Nate alisema.


Aidha, aliongeza kuwa huenda ikawa jamaa ambao wanaohudumu kufanya usafi katika nyumba za watu walinadhifisha nyumba yake kimakosa.

Post a Comment

0 Comments