ALIYEKUWA PENZINI NA P DIDY ATANGAZA KUWA MJAMZITO

Baada ya penzi kati ya mwimbaji Cassie na P Diddy kuvunjika rasmi October 17, 2018 sasa mwanadada huyo amekuja na good news kwa mashabiki zake na kutangaza kuwa ni mjamzito na anategemea kupata mtoto hivi karibuni na mpenzi wake mpya Alex Fine ambaye ni mjasiriamali.

Cassie alitoa taarifa hizo za ujauzito kupitia ukurasa wake wa instagram na mastaa kibao walimpongeza kwa taarifa hizo nzuri akiwemo Khloe Kardashian ambaye aliandika “Hongera Cassie, utakuja kua mama bora” huku Cassie akiwa aliandika caption inayosomeka “Siwezi kusubiri kumpokea mtoto wetu wa kike , nakupenda daima na milele”

Inaelezwa kuwa Diddy na Cassie walikutana rasmi mwaka 2000 hii ni baada ya Cassie kujiunga na record label ya Bad Boys na ilipofika 2012 wawili hao waliamua kuweka wazi mahusiano yao lakini August 2016 inadaiwa kuwa waliachana na baadae kurudiana na October 17,2018 waliachana rasmi. 

Post a Comment

0 Comments