HAMISA MOBETTO AHOFIA USALAMA WAKE


Siku za hivi karibuni mwanamitindo ambaye pia ni mwimbaji Hamisa Mobetto, amekuwa karibu na msemaji wa klabu ya Simba na wamekuwa wakionekana kuwa pamoja kwenye mambo mbalimbali ikiweko uwanjani.

Ukaribu huo umezua maswali mengi huku Hamisa mwenyewe akionekana anahofia kupigwa kutokana na ukaribu huo, ambapo ameeleza hofu hiyo kupitia post ya Manara kwenye mtandao wa Instagram iliyowaonesha wakiwa pamoja.

Manara alipandisha picha hiyo Jumapili Juni 2, 2019 na kuandika hivi ''Team Samata tushampiga Kiba Sita na baadae tunafuturu kichanpioni Serena hotel''. Hamisa baadae alicomment na kuandika, ''Ipo siku utafanya tupigwe''.


Post a Comment

0 Comments