WAMSHAMBULIA MAMA YAO NA KUMUUA KISA WIVU WA MAPENZI

Kaka wawili kutoka kijiji cha Kilungu kaunti ya Makueni nchini Kenya wamekamatwa baada ya kumshambulia na kumuua jamaa aitwaye Onesmus Kivuna aliyedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mama yao.

 Wawili hao wanasemekana kumvamia jamaa huyo akiwa kwenye nyumba ya mama yao majira ya saa nne usiku Jumanne Juni 4,2019 na kumkatakata Onesmus Kivuna kwa panga hadi akafariki dunia. 

 Maafisa wa polisi waliupata mwili wa marehemu kwenye kichaka kilichoko mita 300 kutoka kijiji chake cha Mbukuni kata ndogo ya Kilome. 

Kulingana na taarifa ya polisi, marehemu alikuwa na majeraha mabaya kwenye shingo na kichwani, ishara kwamba alikatwa kwa panga. 

Naibu kamishna wa kaunti ya Makueni Rebecca Ndirangu alithibitisha kisa hicho na kusema mama huyo pamoja na washukiwa wanazuiliwa huku uchunguzi ukiendelea.

 Jirani wa mama huyo ambaye pia ni mjane, Muthini Kilonzo anasema kwamba marehemu alikuwa ameonywa mara kadhaa na vijana hao dhidi ya kumtongoza mama yao ila hakutilia maanani onyo hilo.

 ” Nilikuwa mwendo wa saa nne usiku ambapo tulisikia mtu akipiga yowe akiomba usaidizi, tulipofika kwa jirani yetu, tulimpata jamaa huyo akiwa sakafuni akivuja damu nyingi, alikuwa na majeraha mabaya kwenye shingo na kichwani, “Kilonzo alisema.

 Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi wafu cha hospitali ya Kilungu

Post a Comment

0 Comments