LULU DIVA ATOA SIRI YA RIYAMA ALLY

Staa wa Bongo Fleva Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amemfungukia staa mwenzake kwenye tasnia ya filamu Bongo, Riyama Ally kuwa anajua kuvaa uhalisia kama inavyotakiwa kwenye sanaa .

Lulu Diva amesema kuwa, kama unaigiza muvi moja na Riyama halafu uwe na chongo kwenye filamu, anaweza kulichamba hilo chongo lako hadi ukashindwa kujibu chochote.

“Yule dada anakuchamba kama anachamba kweli, unaweza kumuomba msamaha kwenye muvi. Akimaliza kushuti unaweza kumfuata na kumuuliza dada pale ulikuwa unamaanisha au?” alisema Lulu Diva

Post a Comment

0 Comments