MAWIGI YAZUA MJADALA BUNGENI

Dodoma. Mapendekezo ya Serikali kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye nywele bandia zinazotengenezwa ndani ya nchi yaibua shangwe bungeni.

Wabunge kwa mtindo wa kupiga meza wameshangilia mapendekezo hayo leo Alhamisi Juni 13, 2019 wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akiwasilisha bungeni  mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2019/2020.

Dk Mpango alilazimika kusita kwa nusu dakika kuendelea kusoma mapendekezo hayo kutokana na wabunge kushangilia,  hasa wanawake huku Spika Job Ndugai akitania, kutaka hata kucha kuongezwa ushuru.

Katika mapendekezo hayo Dk Mpango amesema kwa nywele zinazotengenezwa nje ya nchi,  mapendekezo ni kuongeza ushuru kwa asilimia 25 kwa zinazotambuliwa kwa HS Code 67.03: 67.04 na 05.01, kwamba lengo ni kuongeza mapato ya Serikali.

Post a Comment

0 Comments