Diamond Platnumz akutana na El Hadji Diouf



Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz amekutana na mchezaji nguli wa zamani wa timu ya taifa ya Senegali, El Hadji Diouf na kitu kinachoashiria ni biashara kati yao.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao Instagram, Diamond aliweka picha ya pamoja akiwa na Mkurugenzi Wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga na nguli huyo ikiwa imeandikwa; 'Only i see is Money here'(hapa ninaona fedha tu).

Utakumbuka hivi karibuni Diamond Platnumz pia amekuwa na safari zinazomkutanisha na wachezaji wakubwa wa mpira wa miguu, ameshakutana na wengine kama Didier Drogba na Samuel Eto'o.

    

Post a Comment

0 Comments