Rasmi: Singida United wamuuza Habibu Kyombo kwa Mamelodi Sundowns


Mshambuliaji wa Klabu ya Singida United Habibu Kyombo ameuzwa katika klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini baada ya kufuzu majaribio yake aliyokuwa anayafanya katika timu hiyo.

Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga amesema kuwa Mshambuliaji huyo tayari washamuuza na atajiunga na timu hiyo mwezi Juni baada ya Ligi kuu Tanzania bara kumalizika.

"Biashara ya Habibu Kyombo tayari imeishamalizika na mkataba wake na Mamelodi Sundows utaanza mwezi juni baada ya Ligi kumalizika,msije mkawa mnamuona Kyombo hapa mkajua yupo tu, yupo kwa sababu mkataba wake unaanza mwezi Juni" amesema Sanga

    

Post a Comment

0 Comments