Wanawake Wengi wa Siku Hizi Hawajui Kupika..Urembo Umechukua Nafasi

Tofauti na miaka ya zamani wakati tunakua,wazazi wetu walikuwa wakipika chakula watoto mnafurahia chakula kutokana na mapishi mazuri.

Kwa mfano, wa mama na wa dada wa zamani(waliozaliwa miaka ya 60 kurudi nyuma) wengi wao walikuwa wapishi wazuri kwenye familia zao kiasi kwamba wakipika chakula mfano pilau, wali, samaki,chapati,maandazi,n.k, wanafamilia chakula mnakifurahia tofauti na siku hizi.

Hivi sasa unaweza kuta mwanamke mrembo ila akipika chakula,unaweza kula tu kwa kumuonea aibu na hali hii ni hata kwa ma-house girl wa siku hizi ambae ukimleta kwako inabidi umpe darasa la kupika chakula chenye ladha.


Kwenye migahawa na wa mama ntilie na kwenye nako hali ni hio hio.Mtu unaagiza chakula kula unashindwa na bado ukibadili mgahawa hakuna guarantee kwamba unakohamia kuna unafuu (afadhali).


Inawezeka mfumo wa maisha ya kisasa ndio unachangia hali hii kwa kiasi kikubwa na hasa kwa waloizaliwa kuanzia ya miaka ya 80 mwishoni na kuendelea.

Wanachojua wanawake wa siku hizi ni kupaka make up na wapi yanauzwa mawigi

Post a Comment

0 Comments