Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba
wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua
muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani
kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha.
Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu
kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao
kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa
ni zaidi ya uzuri.
Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma
ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za
kuolewa.
Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa
tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke
anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata
mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu
lakini haitatokea mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa.
1. Mwenye mapenzi ya kweli.
Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke na ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto hao ndio furaha ya ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga. Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake.

Mwanamke asiye na mapenzi ya dhati utamgundua tu, muda
mwingiutamuona macho yake yako kwenye mfuko wa mwanaume. Akiona kwamba
mfuko umetuna utaona anaonesha mapenzi ya hali ya juu lakini pindi hali
inapokuwa kubwa mbaya kifedha mapenzi yanaanza kufifia.
Kwanini wanaume wanapenda wana wake wenye mapenzi ya dhati
kutoka mioyoni mwao na si kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na
ukweli kwamba maisha siku zote yanabadilika, kama waswahili
wanavyosema, kuna kupanda na kushuka.
Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama
itatokea hivyo basi ushukuru mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima
afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote
wa maisha yao na si kwa kipindi fulani tu cha neema.
Si hivyo tu pia asilimia kubwa ya maisha ya ndoa
yanatawaliwa na mapenzi, kwa hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana kwa
wanaume wengi kuiangalia ili wasije wakajikuta wanaoa mwanamke ambaye
baada ya muda mapenzi yanakwenda likizo hali ambayo inaweza kuwafanya
wasiishi maisha ya raha mustarehe.
2. Wenye tabia nzuri
Tabia njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda, hiyo ni katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja sualana kuoa tabia inakuwa kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na ukweli kwa sababu wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani utaambiwa anatabia mbaya.

Naweza kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa kwa baadhi
ya wanawake kukosa wanaume wa kuwaona. Hakuna mwanaume hata mmoja kati
ya wale ambao nimejaribu kuongea naye ambaye ameonesha kulidharau suala
hilo la tabia.
Si hivyo tu wapo wanaume ambao wameingia kichwa kichwa na
kuoa kwa kuangalia sura tu bila kujali tabia, matokeo yake baada ya siku
chache yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo imepelekea
kuvunjika kwa ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo mwanamke.
3. Mwenye uchu wa maendeleo
Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani ‘golikipa’. Kama atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa maendeleo kwa kujituma kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio vijijini na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijijini na hata vijijini.

Ile dhana ya kusema mwanamke ni mama wa nyumbani wa kukaa
na kujipodoa akimsubiria mwnaume arudi amstarehesha, sasa hivi imepitwa
na wakati. Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye
ndoto za maendeleo katika maisha yao. Hata kama watakuwa si wafanyakazi
lakini wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao juu ya jinsi gani wafanye
ili wafanikiwe.
4. Wasiopenda makuu.
Kuna wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali hali halisi ilivyo. Kuna wanawake naweza kusema wana tamaa, kila wikiendi utamsikia “leo tunakwenda wapi dear?”

Akimuona rafiki yake kanunua simuya laki tatu na yeye
utamsikia akisema, ‘na mimi naomba uninunulie simu kama ya Grace’.
Ukienda naye Pub anakuambia,”mimi sinywi pombe za chupa natumia za kopo
tena Heineken’. Yeye hajali kiasi cha pesa mwanaume alicho nacho na
usipotekelezea anachukia na anaweza hata kupunguza mapenzi.
Wanawake kama hawa wako katika mazingira magumu sana ya
kuweza kupata wanaume wa kuwaoa. Mara nyingi katika maisha fedha
huzungumza, kama mwanaume atakuwa na pesa ya kutosha itakuwa rahisi sana
kwa mwanamke kupata kila atakachopenda lakini si kwa kumwambia mimi
nataka kitu fulani.Mwanaune mwenyewe utamsikia akisema, ‘unataka
nikununulie simu ya aina gani, au leo unataka twende wapi?’ hapo ndipo
utakuwa na nafasi ya kusema, ‘mimi nataka uninunulie simu kama ya fulani
ama leo nataka twende sehemu fulani.’
Wanaume ni warahisi sana wa kuwapatia wale ambao
wanatarajia kuwaoa chochote ambacho watahitaji kama tu pesa haitakuwa
tatizo. Kitu ambacho kinawaudhi wanaume wengi ni ile tabia ya mwanamke
kupenda mambo makubwa bila kuangalia uwezo uliopo kwa mwanume.
Kuna wanawake wengine wao si wasemaji kabisa, yeye
anasubiri leoamemletea hiki, anapokea na kushukuru, kesho akiambiwa
twende beach anakubali. Au wengine wanasubiri mpaka waulizwe wanataka
nini, ndio wanasema.
Sisemi kwamba uwe mkimya tu hata kama una shida ya kitu
fulani na unafahamu kwamba ukimweleza mwenza wako anaweza kukusaidia,
hapana! kama unaona kwamba uwezekano wa kupata kile ambacho
unakihitajiupo mweleze kwa utaratibu naamini atakuelewa na
kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi wanaume wengi ni ile ya kulazimisha
ufanyiwe kitu fulaniwakati inawezekana uwezekano haupo.
5. Wavumilivu.
Wapo wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha.Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanume, huyo siyo mwanamke wa kuoa.

Wangapi leo hii huwatoroka waume zao pindi inapotokea
kuumwa, kufilisika ama kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja
ama nyingine yanaweza kuwafanya maisha yao kutingishika?
Uvumilivu kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi
ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke mweye mapenzi ya
dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha
ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya starehe.Hawa ndio wale ambao
wanaume wengi wengependa kuwa nao maishani mwao.
Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto kwa wanawake. Wajue
kwamba wanaume wanafurahi kuwa na wanawake wa aina gani. Hata kama
utakuwa umeshaolewa, kama kuna wakati kunakuwa na kutokuelewana baina
yenu, chunguza yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya tabia ambazo
nimezitaja hapo juu. Waweza kubadilika kwani inawezekana.
0 Comments