Watu wengu hujisikia vizuri wanapowavutia wenzao wa jinsia
nyingine. Je, unafikiri ni kitu gani kinachomfanya mwanamke aonekane wa
kuvutia?
Kuna vitu vingi vinavyojulikana vizuri zaidi kwa upande wa
mwanamke kama vile; mwili mzuri, sauti yenye mvuto, nywele, mikono
mizuri na mengineyo mengi. Lakini, kuna vingine ambavyo siyo vya kawaida
vinavyohusu mwanaume kumvutia mwanamke.
Je, ni vitu au mambo gani ya kipekee ambayo, humfanya
mwanamke aguswe na mwanaume fulani na huku mwanamke mwingine akishangaa
ni kwa nini mwanamke mwenzake ameguswa sana na huyo jamaa?
Inawezekana yapo mengi ambayo, huyajui. Kwa mfano, mwanamke
anaweza akavutiwa na jina la kwanza au la ukoo la mwananume fulani.
Hapa mwanamke hufikiri kwamba, huyo mwenye hilo jina hawezi kuwa mtu wa
kawaida, na kila kitu anachofanya ni lazima kiwe cha ajabu.
Labda ni kutokana na jina hilo kuwa ni la kigeni au anatoka
kwenye ukoo ambao ni bora au wa kipekee au anafikiri labda huyo
mwanaume atamwezesha kile ambacho, mara nyingi amekuwa hakipati.
Lakini, inawezekana kabisa kwamba, mwanamume huyo si mzuri
sana wa kuvutia au ni mbaya sana kuliko wengine. Hakuna anayejua, labda
anachotaka mwanamke huyo ni kujaribu bahati yake ili aone kitakachotokea
kwa uhakika ziadi.
Inawezekana pia kuwa, mwanamke anaweza kuchanganyikiwa
zaidi baada ya kuona umbo la mwanamume huyo au gari lake. Pengine mambo
hayo ndiyo ambayo, amekuwa akiyapenda zaidi. Inawezekana ikawa ni dalili
ya bahati kwake kwamba, ametokea katika maisha yake mtu ambae, kwa muda
mrefu amekuwa akitamani kumpata.
Upo uwezekano pia kwamba, mwanamke akavutiwa na mwandiko au
sahihi ya mwanamume fulani. Wakati mwingine mwanamke hutokea kuwa na
uhakika zaidi na kuamini yale anayoambiwa kuhusu tabia ya mwanaume huyo,
bila hata kufanya uchunguzi wa kina. Hata hivyo, ukweli ni kwamba, upo
uwezekano wa kuisoma tabia ya mwanaume huyo kwenye sahihi au mwandiko
wake.
Mwanamke pia huvutiwa na lafudhi ya mwanamume, fani yake,
hobi, na kitu kingine kisicho cha kawaida ambacho mwanamume huyo
anakipenda na kukifanya. Hata hivyo, mwanamke anatakiwa awe mwangalifu
mno na upande wa pili wa mtu huyo ambao, yeye haujui. Hapa ikiwa na
maana kuwa , pamoja na sifa zote hizo alizozibaini kutoka kwake,
anapaswa kujua kwamba, mwanamume huyo kama binadamu asiyekamilika pia
ana mapungufu na udhaifu mwingi.
Kuufahamu ukweli huu, kutamsaidia katika kuimarisha zaidi
na kumfanya awe makini anapotafuta mwanaume wa kuishi naye. Na akumbuke
kuwa, wapo wanaume ambao huficha makucha yao au kasoro zao kwa wapenzi
wao.
Kuna mwanamke mwingine hupenda mwanaume mwenye vituko,
kilema au mwenye kasoro nyingine za kimwili. Yote hayo hutokana na asili
ya mwanamke. Na ni mambo yanayoongea ndani mwake kwamba, anataka
kumjali na kumhurumia mwanaume huyo.
Kwa kawaida, mwanamke huvutiwa zaidi na kwa urahisi, pale
mwanaume anapoonyesha tabia ya usikivu na utulivu. Hata hivyo, mtazamo
huu kwa upande wa mwanamke, huhesabika kuwa ni ushindi kwake.
Hali kadhalika, mwanamke huvutiwa na tabia fulani ya
kipekee ambayo, mwanaume anayo. Kwa mfano, jinsi mwanaume huo
anavyoutumia mkono wake wa kushoto, kwani watu wengi wanatumia mkono wa
kulia. Ukweli ni kwamba, labda huyo ndiye mwanaume ambae mwanamke huyo
anamtaka, kwani pia wanawake wengine hawawezi kujizuia kuwapenda wanaume
wenye macho ya bluu. Hilo pia ni jambo la kawaida.
Mwanamke anaweza kumpenda mwanaume kutokana na jinsi
anavyofanya kazi za nguvu au kutokana na mwili wake kuwa na misuli. Ni
jambo la kawaida kwa wanawake kufurahia wanaume waliojazia, na
inavyoonekana wanawake huwaona wanaume ambao ni lainilaini kuwa wana
haiba ya kike au ni mashoga.
Hapo ndipo mwanamke anapolazimika kufikiria kwa makini,
kuhusu mwanaume anayetumia muda mwingi kujipodoa na fedha nyingi kwa
mambo ya urembo na vipodozi kuliko hata mwanamke, kama kweli anamvutia
na anamfaa.
Na kitu kingine ni kwamba, mwanamke humpenda mwanaume
anayesaidia kufanya kazi za nyumbani. Kwa kufanya hivyo, mwanamke
huamini kwamba, mwanaume huo anamjali na kumthamni.
Kwa kumalizia ni kwamba, mambo mengi yanayomchanganya
mwanamke kuhusiana na mwanaume anayemtaka, kwa kweli ni ya kipekee sana
na wakati mwingine huonekana kuwa ni kituko, ingawa wakati mwingine
yanaweza yakaeleweka vizuri. Mara nyingi vigezo hivyo huonekana kuwa
sahihi, iwapo tu mwanamke huyo atajisikia vizuri na kupata ridhiko la
nafsi yake.
0 Comments