Msanii wa Muziki Tanzania Shilole, kupitia kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kila siku ya Jumatano kuanzia saa 8 : 30 Mchana hadi saa 9 : 30 Mchana, kwenye kurasa za Facebook na YouTube ya East Africa TV, amesema anajivunia kutoka kimapenzi na Mumewe Uchebe
akiwa amemzidi miaka 2, na kuwataka vijana wakiume waoe wanawake ambao ni wakubwa kwao.
Shilole amesema kwa sasa yeye ana miaka 31 na mumewe ana miaka 29, na amekuwa na msaada mkubwa sana kwa mumewe hasa linapofika suala la kupanga maisha.
Shilole amesema kuwa "mume wangu Uchebe nimezidi miaka 2, kwa kuwa mimi nina miaka 31 na sioni ajabu kutoka na mwanaume ambaye nimemzidi umri kama tulivyo mimi na mume wangu".
"Hakuna shida mwanamke kumzidi umri mwanaume, tena niwaambie vijana oeni wanawake waliowazidi umri kwa sababu wanamaarifa makubwa na akili ya maisha, mtawaoa hao wakina Mwajuma Ndalandefu ambao hata kuoga hawajui" amesema Shilole.
Aidha Shilole amesema kuwa moja ya mambo ambayo huwa anayafurahia kwa mume wake Uchebe ni kupigwa, kwa kile alichokidai ni ishara ya kuwa anampenda na ana mapenzi ya kweli.
0 Comments