MENINAH MAISHA YANAENDELEA!




MSANII wa Bongo Fleva na mwigizaji Menina Attick ‘Meninah’, amesema hata kama ataamua kujifungia ndani, lakini ukweli unabaki palepale kuwa, lazima maisha yaendelee.
Meninah ameliambia Gazeti la Ijumaa Wikienda kuwa, kwenye maisha lazima kuna jambo litakupata bila kutarajia, lakini cha msingi ni kuangalia pale ulipoanguka na kusimama haraka ili maisha yaendelee na hicho ndicho kilichotokea kwake baada ya kusambaa kwa video yake chafu hivi karibuni.
“Binadamu watambue chochote kinachompata mtu, lazima ufafanuzi upatikane, lakini si kukaa ndani na kujifungia kwani lazima maisha yaendelee,” amesema Meninah.
STORI: IMELDA MTEMA

Post a Comment

0 Comments