NJIA 8 ZA KUFANYA NGOZI YAKO IWE NZURI NA YA KUVUTIA

Watu wengi husumbuliwa na tatizo la ngozi zao kuzeeka haraka, kukosa mvuto na kupoteza mvuto wake wa asili, wengi husumbuliwa na VIpele, chunusi, ngozi kukauka, madoa na mashimo kwenye ngozi. Na hii husababisha wengine kutumia gharama kubwa kununua vipodozi kwa ajili ya kutibu ngozi zao. Leo nitawaletea dondoo chache tu za kufanya na kutunza ngozi yako ili iendelee kuwa na mvuto.

1. Tumia vipodozi vinavyoendana na ngozi yako
Watu wengi huharibu ngozi yao wenyewe bila kujua kutokana na kutumia vipodozi visivyoendana na ngozi zao. Utakuta mtu ana ngozi yenye mafuta lakini anatumia vipodozi vya watu wenye ngozi kavu au mtu mwenye ngozi kavu anatumia vipodozi vya mtu mwenye ngozi ya mafuta, hapo lazima ngozi yake itaharibika.

2. Usilale na ‘make-up’ usoni
Unapokuwa umetoka nyumbani na kurudi usiku usilale na ‘make-up’ usoni hata mchana unapoamua kulala, usilale na make-up, unapolala mwili huitaji kupumzika na ngozi huhitaji kupumua, ‘make-up’ huziba matundu ya ngozi hivyo kuzui ngozi kupumua vizuri na matokeo yake husababisha ngozi kuchoka, kuzeeka haraka na wakati mwingine kupata vipele au machunusi, hivyo kabla hujalala hakikisha umeondoa ”make-up’ zote kwa kutumia ‘make-up remover’.

3. Safisha uso kabla ya kulala
Kama hautaoga usiku au kabla ya kulala basi hakikisha umesafisha uso wako kwa maji safi na sabuni kabla ya kulala hata kama haukupaka vipodozi usoni, ngozi ya uso ni ngozi ambayo hukumbana na changamoto nyingi, hivyo ni vema ukahakikisha umesafisha ngozi ya uso kabla ya kulala ili kuipa ngozi nafasi ya kupumua vizuri.

4. Kunywa maji mengi
Ili kufanya ngozi yako iwe na mvuto kunywa maji mengi, angalau lita moja na nusu kwa siku, maji pamoja na kusafisha mwili huongeza unyevu kwenye ngozi, kinga na kuondoa sumu kwenye ngozi.

5. Usitumie vipodozi venye kemikali mbaya
usitumie vipodozi vyenye kemikali kali zisizofaa kutumiwa na binadamu, kemikali kama mercury au hydrochloric acid ni hatari sana kwa afya ya ngozi na mwili wako kwa ujumla. Kemikali hizi ambazo ukianza kutumia hukufanya uonekane mweupe na mwenye ngozi ya kuvutia baada ya mUda hubadilika na kuharibu ngozi yako pamoja na kukuletea matatizo ya kiafya.

6. Kula chakula bora
kula vyakula bora venye vitamini na protini kama matunda, mboga za majani na vyakula vevye protini kama samaki, mayai, maharage na kuku.

7. Jikinge na jua
Unapokuwa juani, funika ngozi yako kwa mwamvuli au nguo, pia unaweza kujipaka mafuta maalum kwa ajili ya kujikinga na jua. Miale ya jua huunguza ngozi, huondoa mafuta ya kwenye ngozi, hufanya ngozi kuwa nyeusi na huweza kusababisha kansa. Jua baya kwa ngozi ni lile la mchana. Jua linalofaa kwa ngozi ni lile la asubuhi na jioni.

8. Paka mafuta na vipodozi vinavyoendana na hali ya hewa
Hali ya hewa hubadilika, kuna majira ya kiangazi ambayo hukausha ngozi, kipupwe ambapo huwa na baridi na upepo na majira ya joto na mvua ambayo huwa na unyevu mwingi, hali ya hewa husabaisha ngozi nayo kubadilika, hivyo ila kuafanya ngozi yako isiathiriwe na hali ya hewa unatakiwa kubadilisha vipodozi kuendana na hali ya hewa.

Credit: LON FFB

Post a Comment

0 Comments