UKIFANYA HAYA WANAWAKE WATAKUKIMBIA

Mwanzoni mwa mahusiano, mambo huwa motoo, pande zote mbili hufurahia kila hatua ya mwanzo. Tabia mbaya kiasi huanza kujitokeza baada ya wiki mbili, lakini ni mpaka mwezi wa sita hivi ndo tabia zetu halisi hujionyesha

Ni tabia zipi hasa zinaweza mkata stimu mpenzi wako, akakuona sio? Jarida la Daily Star liliandika yafuatayo:

Kwa wanawake

Tafiti iliyofanywa na ‘Vapourlities.com’ iliyojumuisha wanawake 846 na wanaume 827 iliwahoji juu ya nini huwafanya wawachoke wapenzi wao. Soma hapa chini kujua ni nini kinaweza mfanya mpenzi wako akuchoke na asitamani kuendelea kuwa na wewe.

Uvutaji wa Sigara

Asilimia 26 ya wanawake walisema ni uvutaji sigara huwakata stimu, kwamba mwanaume akiwa mpenda sigara sana basi hatopata sana.

Kusahau au kuvunja Miadi

Unaweza kuta mnaahidiana na mwenzi wako mkutane saa Fulani, lakini yeye anakuja masaa mawili baadae, hii hufanya mtu akuoni sio. Sasa bora achelewe, wengine huvunja kabisaa miadi. Tafiti hizo zimeonyesha kwamba, asilimia 19 ya wanawake, walikua wanachukizwa na kusahau au kuvunja miadi.

Ulevi na Kubeti

Tafiti hizo pia zilionyesha, asilimia 14 ya wanawake walichukizwa na tabia za kubeti za wanaume, huku asilimia 11 wakichukizwa na ulevi uliopitiliza. Unakuta mwanaume analewa mpaka usiku wa manane, halafu anategemea mwanamke atafurahi kushiriki nae tendo au tu kufurahi kua nae kwa ujumla. Ni vyema kuziangalia tabia hizi.

Kunuka harufu mbaya

Tafiti zilizopita pia zimeonyesha kuwa, asilimia 80 ya wanawake hawawezi kufanya tendo la ndoa na mwanaume ambaye ananuka vibaya au ana harufu mbaya, ambayo kwa kiasi kikubwa husababishwa na jasho baya. Na pia wanawake hupendelea wanaume wenye tabia njema kuliko wenye tabia mbaya/ Bad boys.

Kwa Wanaume

Kiujumla, tafiti hizi zinaonyesha kuwa, wanawake hawapendezwi na tabia za wanaume ambazo zinahusiana na masuala ya afya na usafi.

Hii ni tofauti kwa upande wa wanaume, wenyewe tabia zinazowachukiza dhidi ya wanawake zinahusiana na tabia zinazokubalika kwa ujumla, wao hujali sana masuala ya tabia. Zisome hapa chini tabia za wanawake ambazo wanaume huzichukia.

Kutumia muda mwingi kwenye simu

Wanaume wengi, huchukizwa na tabia ya wanawake kutumia muda mwingi sana kwenye simu hasa mitandao ya kijamii.

Kujiandaa muda mrefuu

Unakuta mwanamke anatumia mwaka mzima kujiandaa kwa safari au mtoko tu mdogo, tabia hii huwakera sana wanaume.

Umbea

Wanaume pia huchukizwa na tabia za wanawake kukaa na kuzungumzia marafiki au ndugu kwa kuwasengenya. Hii inafuatiwa na tabia ya unywaji pombe na uvutaji sigara pia.

Kwa tabia tajwa hapo juu, unakuta mtu anaanza mahusiano hajui kama mwenzi wake ni mvutaji au mywaji, lakini kadri siku zinavoenda na kuona mwenzi amekuzoea na kuonyesha tabia zake hizo, unaweza jikuta haupo tayari nazo, zinakupa wakati mgumu kuzikubali. Unakuta hata kama havuti sigara mbele yako au hata kunywa, harufu inakuwepo na inakera.

Kama utaweza kumshawishi kuacha ni vyema, lakini ukishindwa hatari yake ni mahusiano hayo kuelekea ukingoni.

Mwana saikolojia Susan Whitbourne alisema kuwa, tabia hizi ndogo ndogo zisizopendwa zinaweza athiri ukaribu na faragha baina ya wapenzi.

Amesema, kama mahusiano hayapo imara, matatizo madogo madogo yanaweza yakawa ishu kubwa na kutishia kuvunjikakwa mahusiano.

Post a Comment

0 Comments