Kupata maumivu makali wakati wa kukojoa kitaalamu inaitwa Dysuria. Kitendo hichi huwapata zaidi wanawake kuliko wanaume. Maumivu haya mara nyingi hutokana na maambukizi kwenye njia ya mkojo (UTI) au maambukizi ya magonjwa ya zinaa(STD), lakini pia maumivu haya yanaweza kuashiria tatizo kubwa la kiafya kama saratani au kisukari.
Dalili Mbaya ni kama
Kukojoa kwa shidaKujisikia hali ya kuchomachoma wakati wa kukojoaMuwasho wakati na baada ya kukojoaMkojo kuwa na rangi ya mawinguKupata mkojo wenye chembechembe za damu (hematuria), kwa kesi hii ni muhimu kumwona daktari mapema ili ufanyiwe vipimo kugundua chanzo.
Chanzo cha Maumivu Makali Wakati wa Kukojoa
Maaambukizi ya bakteriaMaaambukizi kwenye njia ya mkojo(UTI)Kuvimba kwa tishu za ndani za mrija kwa kutolea mkojoKufanya ngono iliyo rafuKuosha uke mara kwa maraMatumizi ya njia za kupanga uzazi hasa za kuweka ukeniMatumizi ya sabuni kuosha ukeniMagonjwa ya tezi dumeSarataniMatatizo kwenye figo mfano mawe ya figoLisheTiba ya Chemotherapy radiotherapy kwa ajili ya sarataniVimbe kwenye utumbo mdogoMatatizo kwenye kibofu cha mkojo
Kwa watoto mamumivu haya (Dysuria) yanaweza kutokana na kitendo cha mkojo kurudi kutoka kwenye kibofu kwenda kwenye figo kutokana na kuwepo kwa jeraha au kizuizi kwenye njia ya kutolea mkojo
Makundi yaliyo Katika Hatari zaidi ya Kupata Dysuria
WanawakeWanawake wajawazitoWagonjwa wa kisukariKukua kwa tezi dumeKuwa na matatizo kwenye kibofu cha mkojoKufanya ngono bila kutumia kinga, unakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa ya zinaa.
Tiba asili ukiwa nyumbani kwa Tatizo la Maumivu Makali Wakati wa Kukojoa
Kunywa maji ya kutosha
Kunywa maji mengi kunasaidia kusatoa nje sumu na taka na hivo kupunguza mamumivu wakati wa kukojoa. hakikisha kila unapopata kiu kunywa maji na siyo soda.Mafuta ya karafuu
mafuta ya karafuu yanafahamika kwa kupambana na vimelea wbaya na fangasi na pia kuimarisha kinga ya mwili. Mafuta ya karafuu yasitumike zaidi ya week mbili kama unameza.Vitamin C
Ni muhimu kula kwa wingi vyakula vyenye vitamin C pale unapohitaji kuimarisha kinga ya mwili kupambana na maambukizi. Vyakula hivi ni kama machungwa, strawberries, papai, mananasi,mapera, maembe na mboga za broccoli.Kula vyakula vinavyosaidia kuongeza bakteria wazuri tumbo. Vyakula hivi ni kama maziwa mtindi.
Angalizo
Kama tatizo lako la mamumivu wakati wa kukojoa limetokana na magonjw aya zinaa, ni muhimu kwa mwanamke mwenye maambukizi haya kumaliza dozi vizuri ili kuzuia hatari ya kuwa mgumba na maatizo mengine ya uzazi.
Kama tatizo lako limesababishwa na UTI ni muhimu kutibu kwanza ugonjwa husika. Kama usipotibu UTI vizuri inaweza kusababisha matatizo kwenye figo.
0 Comments