SAMATTA ATOA OFA KWA WAKAZI WOTE WA DAR

Awali, mshambuliaji wa Genk, Mbwana Samatta kabla ya kusajiliwa na klabuni hapo, alizichezea TP Mazembe ya DR Congo na Simba ya Tanzania.

Dar es Salaam. Hivi unajua kuwa staa wa Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta wakati mwingine ana vituko sana? Sasa cheki alichokifanya leo Jumamosi.
Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa Stars iliyoondoshwa kwenye fainali za AFCON nchini Misri mwanzoni kabisa katika hatua ya makundi.
Kwenye mtandao wake wa kijamii, amewapa ofa ya bure watu wote, kila atakayemwona yuko huru kumkumbatia.
"Leo hii nitahagi kila nitakayekutana naye kwa sababu najiamini bana,"amekaririwa Samatta ambaye huenda msimu ujao asicheze tena Genk kutokana na klabu mbalimbali hasa za England kumuwinda.
Samatta ambaye kwa kipindi chote hapa jijini Dar es Salaam, tangu amerudi kwenye mapumziko, amekuwa akifanya dhiara mbalimbali kwa ajili ya kuwajulia hali ndugu na jamaa.
Siku mbili zilizopita, aliweka wazi kuwa alikwenda Gereza la Keko kwa ajili ya kuwajulia hali kiongozi wa zamani wa  TFF, Jamal Malinzi na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu'.

Post a Comment

0 Comments