NLIMFUMANIA MUME WANGU NA BFF WANGU KITANDANI

Mwanadada kwa jina la Norah alisimulia mojawapo ya visa ambavyo wanandoa wengi wanasumbuka nazo humu nchini. Mipango ya kando.

Alifichua kuwa alimfumania mumewe wa miaka saba kitandani na rafikiye wa karibu, almaarufu BFF. (Best friend forever).

Kulingana na Norah, siku moja aliondoka na kwenda kazini lakini alipigiwa simu na kuambiwa kuwa mwanawe ni mgonjwa. Alipompeleka hospitalini na kumrudisha shuleni, aliamua kurudi nyumbani na hapo alikipata cha mtema kuni.

Anadai kuwa mumewe alikuwa nyumbani na alipofungua mlango aliwafumania wakila uroda na rafikiye wa dhati, jambo lililomvunja moyo.

Anasema kuwa aliishiwa na nguvu na badala ya kubishana nao alifunga virago vyake na kwenda nyumbani kwao.

Cha kushangaza ni kuwa mwanadada yule amekuwa rafiki yake tangia wawili hao walipokuwa katika shule ya upili, na pamoja wakasomea chuo kikuu kimoja kabla ya kufanya kazi pamoja.

Soma usimulizi wake.

Mimi hata nilitoka juzi, I got my husband akiwa na my best friend. Niliwapata kwa nyumba wakila uroda.

Walikuwa hao wawili pekee, sasa bwanangu alikuwa ameniambia yuko job na mtoto naye alikuwa mgonjwa na nikamwendea shuleni na nikarudi kwa nyumba.

Nilikuwa nafikiria bwanangu yuko job na vile nilirudi nikapata mlango umefungwa na nilipopiga hodi nikampata huko kwani hakuwa anajua ni mimi.

Nilimpata na yule mwanadada ambaye tumesoma naye kutoka shule ya upili tukasoma naye campus na hata tukafanya kazi mahali pamoja. Niliwaangalia tu na nikatoka

Tumekaa na bwana yangu kwa miaka saba, niliondoka Jumanne iliyopita na sasa niko nyumbani kwetu.


Photo Credits: courtesy

Post a Comment

0 Comments