UZURI WAMFANYA MOBETTO ASITAKE WANAUME

Kwel i? Mwanamitindo, mwigizaji na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto  amesema anajijua ni mzuri hivyo hana shida ya kuhangaika na wanaume kwa sasa kwa sababu anajua wakati wowote atampata.

Mobeto aliliambia Gazeti la Ijumaa kuwa anajitambua kuwa ni mwanamke mzuri na kuna mengi amepitia hivyo anaamini akitulia na kufanya mambo yake ni bora kuliko kuhangaika na wanaume. “Ninachojua mimi ni mzuri, kwa nini nihangaike na wanaume? Nahitaji kutuliza kichwa na kufanya mambo yangu kwanza maana wanaume wapo tu,” alisema Mobeto ambaye ni mama wa watoto wawili.

Post a Comment

0 Comments