MBINU ZA KUMTONGOZA MWANAMKE BILA YEYE KUKUKATAA




Kuapproach wanawake wakiwa katika kikundi ni jambo gumu sana kwa mtu yeyote kutimiza. Hata kwa wale ambao wanajiamini mbele ya wanawake inafikia wakati flani wanapatwa na changamoto moja au nyingine. Lakini kama kawaida mambo kama haya yanaeleweka kwa kuwa unaaproach wanawake wengi wakati mmoja na pia kunaweza kutokea maswala mengine ambayo yanaweza kujeuka changamoto kwako.

Kuapproach wanawake wakiwa kwa kikundi si sawa na kubadilisha gemu ya kutongoza mwanamke mmoja bali ni mbinu tofauti kabisa ambayo inahitajika kutumika. Mbinu ambayo lazima uijue na kuielewa.

Kwa nini unahitajika kujua kutongoza wanawake katika kikundi

Jambo muhimu ambalo unapaswa kujua wakati unapoapproach wanawake kwa kikundi ni kuwa unaaproach kundi zima, na wala si mwanamke mmoja ambaye unataka kuongea naye. Kama unaaproach kwa kikundi, ni vyema uende pekeako. Mkiapproach kama kikundi mnaweza kuonekana kuogopesha na wanyemelevu, hivyo ni vizuri zaidi kama marafiki zako watangojea kwa dakika, ili uweze kuwatambulisha vyema kwa kikundi hicho cha wanawake.

Wasalimie wanawake wote wakati mmoja

Ikija na swala la kusalimia wanawake katika kikundi, ni vizuri kuwasalimia wote wakati mmoja. Vile ambayo utawasalimia wanawake katika kikundi ni kama vile utakavyomsalimia mwanamke mmoja; unatoa matamshi ya mizaha na ucheshi, halafu inafuatiliwa na tabasabu halafu sasa unaanza kufunguka zaidi kwa kuongea zaidi na wale wana kikundi ambao wanapenda kuongea. Ni bora kuwasalimia wanawake wote kwa wakati  mmoja hata kama kuna mwanamke kikundini ambaye ulitaka kumvizia ama kuongea naye. Hii haitaonyesha ya kuwa unakimbilia kukutana na mwanamke mrembo pekee, bali unajionyesha ya kuwa umekuja hapo kujumuika na watu na kuinjoy muda wako ipasavyo.

Ipunguze makini yako

Pindi unapoendelea kuongea na wanawake wote, halafu rafiki au marafiki zako wakatokezea, inakubalika kupunguza umakini wako hadi kwa mwanamke mmoja au wawili. Labda bado unataka kuongea na mwanamke ambaye ulimpangia kuongea naye, ama umepata mwanamke mpya kutoka kwa kikundi hicho, unaweza kuyapendua maongezi yako zaidi. Unaweza kuanza na maneno rahisi kama "nimependezwa nawe" ama "unaonekana uko sawa." Hapa unapaswa kumsifu mwanamke kando na umbo lake, halafu baadaye uanzishe gumzo la "nataka kukujua zaidi"

Jaribu kuwa na kisaidizi

Kuwa na kisaidizi wakati unaaproach wanawake katika kundi kubwa inakuwa rahisi sana. Kwa mara, wanaweza kuchat na wanawake wale wengine huku wewe ukimakinika na mwanamke mmoja ambaye ulikuwa umeazimia kukutana naye. Zaidi ni kuwa wanaweza kutoa presha ambayo inakuja wakati unapotaka kuapproach, hii inasaidia kwa kuwa inakupa ujiaminifu kama mwanaume wakati unapoapproach wanawake katika kikundi.  Sababu ni kuwa unajua kuwa usaidizi hauko mbali na wewe na muda wowote wanaweza kutokezea ili kuondoa presha zozote ambazo zinaweza kujijenga.

Mtenge mmoja kutoka kwa kikundi

Kama kuna mwanamke ambaye umeonyesha interest kwake, jaribu kutafuta wakati muwe pekeenu. Hii haimaanishi ya kuwa ni lazima mujitenge katika sehemu moja ya hio klabu ama baa bali pia inaweza kumaanisha ya kuwa unaweza kuamua kutoka ziara hadi katika mkahaha ama sehemu nyingine ya kuvutia ambayo itawaruhusu nyinyi wawili kupata nafasi ya kuongea moja kwa moja ili mjuane vyema zaidi

Post a Comment

0 Comments