SMS AMBAZO MWANAMKE HUPASWI KUMTUMIA MPENZI WAKO

Wanaume hupenda sana kuwasiliana na wanawake kupitia kwa SMS na njia nyingine za mitandao. Wanaweza kukusumbua siku nzima na SMS hizi.

Halafu pindi ukianza kuongea na wao wanaweza kuja na mitindo mingine ya jumbe ambazo zinakuamuru ufanye jambo flani ama kutaka uwaonyeshe kitu flani.

Ijapokuwa unaweza kuona kuwa ni mbinu nzuri ya kuwasiliana nao, wakati mwingine ni tabia mbaya. Unaweza ukamtumia mwanaume kitu flani na mwishowe akakudhalilisha ama kukushusha hadhi.

So kama mwanamke, unapaswa kuweka mipaka kwa kile ambacho utamtumia mwanaume. Leo tumekuja na mambo ambayo hupaswi kumtumia mwanaume yeyote wakati wowote ule. [Soma: Mambo ya kufanya ukipata mchumba mpya]

SMS unazopaswa kuepuka kumtumia mwanaume.

#1 Picha za uchi.

Hapa ni moja kwa moja. Usijaribu kumtumia mwanaume yeyote picha zako za uchi. Hata kama atatumia mbinu yeyote usikubali. Kutuma picha za uchi kwa mwanaume kuna madhara makubwa sana. Ukikosana na yeye anaweza kuzisambaza kwa mitandao na aibu ukurudie wewe.

#2 Uongo.

Usitumie uongo wowote kuteka atenshen ya mwanaume. Hii haina manufaa yeyote. Unachotakiwa kufanya ni kuwa mkweli kwa kila kitu ambacho unafanya. Akikupenda tu atakukubali bila kutumia uongo wowote.

#3 “Hallo, mambo vipi?”

Huu ni mfano mmoja wa meseji ambazo huboesha na huudhi. Aina hizi za sms ziwaachie wenyewe. Mara nyingi aina hizi za sms huhusishwa na wanaume ambao wanapata ugumu wa kuwasiliana na mwanamke.
[Soma: Jinsi ya kumtongoza mwanaume bila kukushuku]

#4 Emoji

Emoji ni nzuri kuteka atenshen ya mwanaume lakini pia lazima ujue matumizi yake. Usitumie emoji za chakula, hoteli, pesa, kuboeka ama emoji zozote ambazo unajua zinaweza kumuudhi yeyote.

#5 SMS pacha

Labda unaweza kusema ni tatizo katika simu yako, lakini hili ni jambo ambalo hupaswi kujaribu. Kumtumia mwanaume SMS za kujirudia rudia unapaswa kuacha. Hii ni tabia ya kuonyesha kuwa una uchu wa kuwasiliana na mwanaume.

#6 Kuandika aya

Kama uko katikati ya mazungumzo, unaweza kuandika aya vile ambavyo unataka wewe lakini kama ndio mazungumzo yanaanza basi hupaswi kuandika ujumbe mrefu. Anza tu na sentensi moja kama tu, hi! Mambo! Niaje! Na SMS kama hizo.

#7 SMS za ulevi

Hizi ni SMS ambazo mtu huandika kimaksudi kana kwamba amelewa. Unamuuliza swali hili yeye anakujibu nje ya mada. Aina hii ya SMS achana nazo. Waachie walevi waendelee nazo.

#8 SMS za kujifanya

Wanawake wengi hupenda kutumia mbinu hii kutaka mazungumzo na mwanaume. Wanakutumia meseji kimakosa halafu wanarudi kusema, “Samahani, nimekutumia sms hii kwa bahati mbaya.”
Mbinu hizi zimepitwa na wakati, achana nazo. [Soma: Jinsi ya kuwa na mahusiano marefu na mpenzi wako]

#9 Udaku

Kuzungumza udaku wa wasanii inakubalika lakini kama unataka kuteka atenshen ya mwanaume kwa kutumia udaku ama uvumi wa uongo basi hutafaulu.

#10 Kumuuliza kwa nini hajakujibu

Ijapokuwa utahitaji akujibu kwa nini hakujibu sms zako wakati uliotangulia, mbinu hii si nzuri kabisa. Achana nayo. Hii ni kwa kuwa mara nyingi wanaume ukiwatumia sms kama hii watakuambia kuwa walikuwa busy ama wanaweza kukudanganya ama kuboeka na wewe tu.

Upo!? Kazi kwako sasa.

Post a Comment

0 Comments