DALILI 10 ZA MTOTO WA KIKE WAKATI WA UJAUZITO


Kawaida mwanamke anapokua mjamzito, moja ya mambo ambayo huyafikiria kwanza kabisa ni jinsia ya mtoto.

Ultrasound katika wiki ya 20 ya ujauzito ni njia sahihi ya kujua jinsia ya mtoto, mbali na maoni ya daktari kutabiri jinsia kutokana na ultrasound, tamaduni na desturi zimekuwa zikitumika kutabiri jinsia.

Makala hii itakujuza dalili za asili zinazoweza kukujuza kama utakuwa na mtoto wa kike;

Kubadilika badilika kwa mihemko ya hisia (mood)

Kubadilika kwa homoni kunaweza sababisha wanawake kubadilika mudi zao. Baadhi ya watu hudhani, wajawazito wanaotarajia mtoto wa kike wana kiwango kikubwa cha aestrogen hali inayopelekea mudi kubadilika. Licha ya hivyo, hakuna tafiti zinazosapoti jambo hilo.

Homa za asubuhi

Baadhi ya watu huamini kwamba uchovu mkali wakaati wa asubuhi (Morning sickness) ni dalili za mtoto wa kike, si mazoea ya watu tu bali hata tafiti zinaonyesha kuumwa wakati wa ujauzito kunahusiana na jinsia ya motto.

Uzito kuongezeka

Ikiwa mwanamke ataongezeka uzito kipindi cha kati cha ujauzito, baadhi ya watu hudhani kuwa anatarajia mtoto wa kike. Lakini, tafiti za kisayansi hazina uthibitisho juu ya hili.

Kupenda sukari

Baadhi ya watu huamini kwamba, mjamzito kupenda sukari ni dalili ya kubeba mtoto wa kike na kwa upande mwingine kupenda chumvi ni dalili ya kubeba ujauzito wa motto wa kiume.

Mapigo ya moyo ya haraka kwa mtoto

Baadhi ya watu huamini kwamba, mapigo ya moyo ya motto yanapoenda mbio inaashiria kuwa ni mtoto wa kike

Ngozi ya mafuta na nywele zilizochoka

Baadhi ya watu huamini kwamba, ngozi kuwa na mafuta, na nywele kuchoka, kuwa kavu na kukosa mvuto yaweza kumaanisha mwanamke anabeba mimba ya mtoto wa kike. Lakini hii pia haijathibitishwa kisayansi kwani hali ya ngozi kuwa na mafuta na nywele kuchoka yaweza sababishwa na mabadiliko ya homoni.

Rangi ya chuchu

Rangi ya chuchu kipindi cha ujauzito yaweza kuashiria jinsia ya motto, rangi hiyo ikiwa haijabadilika, inaashiria mtoto wa kike, lakini inapokua kiza zaidi (Darker) huashiria motto wa kiume.

Tumbo la uzazi kuwa juu au chini

Kama tumbo la mjamzito litakuwa juu, basi ni dalili za kuzaliwa mtoto wa kike, na kama litakuwa chini basi huashiria mtoto wa kiume.

Ukubwa wa matiti

Wengine huamini kwamba, matiti kuongezeka ukubwa ni dalili mojawapo ya kuwa na mtoto wa kike, na kama saizi ni kama ya siku zote basi ni mtoto wa kiume. Lakini hakuna tafiti zinazothibitisha hilo, ni uzoefu tu.

Chunusi usoni

Wengine husema, kuwa na chunusi usoni wakati wa ujauzito kunaweza ashiria kuwa unatarajia motto wa kike na tofauti na hapo basi ni dalili ya mtoto wa kiume.

Njia nyingi zilizotajwa hapo juu ni kutokana na uzoefu wa jamii tofauti tofauti katika kutabiri jinsia ya mtoto. Je unajuaje jinsia ya motto kulingana na mazoea ya jamii yenu? Zitaje kwenye koment hapo chini:

Post a Comment

0 Comments