BARAKA THE PRINCE AANZA MIPANGO YA NDOA

NA JESSCA NANGAWE

MSANII wa Bongofleva Baraka Andrew maarufu Baraka ‘The Prince’amefunguka kwamba tayari yupo kwenye mipango ya kumuoa msanii mwenzake ambaye pia ni mpenzi wake, Najma Dattan mapema mwaka huu.

Akizungumza Baraka alisema  alisema kuwa haoni sababu ya kutomuoa Najma kwa sababu ni msichana aliyekamilika kila idara, ana heshima, hana mambo mengi kama ilivyo kwa wasichana wengine, lakini sifa kubwa anayoipenda zaidi kutoka kwake ni mvumilivu na muelewa.

“Unajua mimi na Naj tumekaa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa kipindi kirefu sasa, hivyo sioni sababu ya sisi kuendelea kuwa wapenzi pia nimechoka kukaa naye mbali nataka nimuoe kabisa. “Nataka nimuweke ndani kwa sababu ana kila sifa za kuwa mke wa mtu, kwanza ni mzuri, ana heshima, muelewa lakini kubwa zaidi ni mvumilivu”Alisema Baraka.

Alisema anatarajia  mapema mwezi Agosti mwaka huu maandalizi ya ndoa yataanza na ikibidi mwaka huu huu watafunga ndoa.

Post a Comment

0 Comments