DOGO JANJA: "SIJAWAHI KUWA SINGLE"

NA JESSCA NANGAWE

MSANII wa kizazi  Abdulaziz Chande maarufu kama Dogo Janja  amefunguka kuwa anajipanga kuoa tena na amesema hajawahi kuwa single katika maisha yake tangu aingie kwenye mahusiano.

Akizungumza Dogo Janja ambaye alifunga ndoa na staa wa Bongomovie Irene Uwoya na kisha ndoa hiyo kuvunjika alisema anatambua kuoa ni mipango ya Mungu na hilo kwa sasa ni miongoni mwa mipango iliyo kwenye ratiba yake.

“Kuoa ni jambo la kheri najipanga kufanya hivyo kwa kuwa hayo ni maisha yaliyo ndani ya uwezo wangu, nimepitia mengi na nimejifunza mengi naamini kabisa changamoto nilizopitia zimeniweka katika ramani nyingine na kunipa somo”Alisema Dogo Janja.

Aidha aliongeza kuwa pamoja na kutokua na ukaribu na aliyekua mke wake Uwoya lakini ni miongoni mwa watu anaowasiliana nao na ikitokea kuhitaji msaada wake ndani ama nje ya kazi zake hatasita kufanya hivyo.

Post a Comment

0 Comments