ATHARI ZA WOGA KABLA YA TENDO LA NDOA

Woga kabla ya tendo la ndoa ni tatizo linaloweza kuwatokea wanaume katika kipindi cha maisha yao na kuwasababishia kushindwa au kushiriki chini ya kiwango tendo hilo na wenza wao.

Ni tatizo ambalo kama linampata mtu mara kwa mara linaweza kuwa chanzo cha kupata tatizo la kuwahi kufika mshindo, kushindwa kuendelea mizunguko mingine ya tendo au kukosa hamu ya tendo.

Tatizo hili linapomkabili mwanaume inaweza kuwa chanzo cha kuvunjika uhusiano au kuleta mifarakano. Mwanaume anaweza akaonekana mtulivu na anayeongea kuliko mwanamke lakini ndani ya mioyo yao huwa hofu hali inayomfanya kuwa mwoga hasa nyakati za matayarisho kabla ya tendo.

Yafuatayo ni mambo mbalimbali yanayompa hofu mwanaume na kumfanya kuwa mwoga.

Hofu ya kuwa hanithi (Impotence) ndiyo tatizo linaloongoza kuwafanya wanaume wapate woga wa kujamiiana na wenza wao.

Nchini India gazeti maarufu la Times India liliwahi kuripoti kuwa karibu asilimia 90 ya wanaume wenye tatizo la kushindwa kusimika husababishwa na matatizo ya kisaikolojia na huku asilimia 10 huwa ni ya kibaiolojia.

Hofu ya maumbile madogo ya kiume ni mojawapo ya tatizo linachangia woga, wanaume kujihisi kuwa na maumbile madogo na kumfanya kuwa na dhana kuwa atashindwa kukidhi hisia za kimwili za mwenza wake.

Wanaume wengi wanashindwa kufahamu kuwa umbile dogo si chanzo cha kushindwa kumridhisha mwenza. Mwanamke anaweza akaridhishwa na kufika keleleni hata kwa mbabaa wenye saizi ndogo kabisa. Hofu ya tatu ni tatizo la kuwahi kufika mshindo kabla ya kumridhisha mwenza, hili ni tatizo linalomweka mwanaume katika mawazo na kumfanya kuwa mwoga kushiriki tendo akihisi kuaibika kwa kutomridhisha mwenza.

Baadhi ya wanaume huweza kujihisi kuwa hawako kawaida wanapojilinganisha na wanaume wengine, anaposikia wenzake wanapojisifu kwa maumbile makubwa na uwezo wakwenda mizunguko mingi bila kuchoka huwasabishia hofu isiyo na lazima.

Post a Comment

0 Comments