ZAMARADI AMPIGA KIJEMBE MAKONDA

Zamaradi akiwa anawatambulisha wageni hao kwa kutambua uwepo wao, alisema uwepo wa wawili hao unaonyesha kweli tamasha lao ni kubwa kuliko.

MSHEREHESHAJI  Zamaradi Mketema ni kama amewapiga kijembe kimtindo wageni waalikwa katika hafla ya Kubwa Kuliko iliyoandaliwa na klabu ya Yanga, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Hafla hiyo inafanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam ikiwa na lengo la kuchangisha pesa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Zamaradi akiwa anawatambulisha wageni hao kwa kutambua uwepo wao, alisema uwepo wa wawili hao unaonyesha kweli tamasha lao ni kubwa kuliko.
"Mpaka wa upande wa pili wamekuja kweli hii ni kubwa kuliko ndugu zangu naomba tupige shangwe kidogo," alisema.
Makonda mara kwa mara amekuwa akishindwa kuficha hisia zake klabu ya Simba, baada ya hivi karibuni kutoa zawadi kwa wachezaji wa Simba waliofanya vizuri msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara.
Kwa upande wa Waziri Mkuu, Majaliwa licha ya kuwa ni mgeni mwalikwa naye ni shabiki wa klabu ya Simba.

Post a Comment

0 Comments