YAFAHAMU MAMBO AMBAYO WANAUME HUSHINDWA KUYAZUNGUMZA HADHARANI

Kila sekundi 40 mtu hujitoa uhai duniani. Mara nyinig huwa ni wanaume wanaoamua kujitoa uhai, kwa kiasi fulani kutokana na kwamba ni nadra wao kuzungumzia matatizo yao au kutafuta usaidizi.

Basi ni mambo gani ambayo wanaume wanapaswa kuyazungumzia wazi zaidi?

Matumizi ya mitandao ya kijamii huenda yakaathiri afya ya akili.

Utafiti kutoka chuo kikuu cha Pennsylvania umebaini kwamba muda mwingi tunakuwa katika mitandao ya kijamii, inatuweka katika hatari ya kujihisi mpweke na kuwa na msongo wa mawazo.

“Kupunguza kutumia mitandao ya kijamii inasaidia kupungua pakubwa msongo wa mawazo na upweke,” anasema mhariri wa utafiti huo na dakatari wa magonjwa ya akili Melissa Hunt. “Athari hizi zinajitokeza pakubwa kwa walio na kiwango kikubwa cha msongo wa mawazo alipofika kushiriki katika utafiti huo.”

Lakini mitandao ya kijamii inadhuru vipi?

Kinachofanyika katika mitandao ya kijamii ni nadra kuwa yaliomo katika maisha halisi ya mtu, lakini hua ni vigumu kutoyamithilisha anasema Oscar Ybarra, mhadhiri katika chuo kikuu cha Michigan.

“Sio lazima watu watambue kwamba hili linafanyika, lakini linafanyika. Kila unapozidi kutumia mitandao ya kijamii unazidi kutofuatisha maisha na hilo huchangia hisia wanazo kuwanazo watu.”

Upweke

Katika utafiti mkubwa wa aina yake, utafiti kuhusu upweke wa BBC kwa ushirkiano na Wellcome Collection umegundua kwamba vijana walio na umri wa kati ya miaka 16 na 24 wana upweke mwingi.

Utafiti wa mnamo 2017 wa Oxford umebaini kwamba ni vigumu kwa wanaume kufukuza upweke.

“Kilichobaini iwapo kuna urafiki na wasichana ni iwapo walijaribu kuwasiliana kwa simu,” anasema Robin Dunbar, aliyeongoza utafiti huo. “Kilichochangia kudumu kwa urafiki wa wanaume ni kwamba wanashirkiana zaidi – mfano kwenda kutazama mechi za soka pamoja, kwenda kujivinjari au kupata kinywaji pamoja. Ilibidi wajitahidi. Kulikuwa na tofuati kubwa ya kijinsia.”

Upweke unapokuwa tatizo kubwa, unawezakuwa na athari kubwa katika afya ya mwili na akili. Utafiti umehusisha upweke na hatari ya kuugua kama ugonjwa wa kusahau magonjwa mengine makubwa na tabia zenye hatari kwa afya.

Kulia

Haki miliki ya pichaSTEFAN HEUNIS

Utafiti mwingi umeashiri kwamba kulia hakuliwazi tu, lakini pia inashinikiza imani na husaidia katika kukubalika katika jamii.

Kwa mujibu wa utafiti nchini Uingereza, 55% ya wanaume walio na umri wa kati ya miaka 18-24 wanahisi wanapolia wanakuwa io wanaume thabiti.

“Tunawafunza vijana au awavulana wakiwana umri mdogo wasionyeshe hisia zao, kwasbabau unakuwa ‘dhaifu’ ukifanya hivyo,” anasema Colman O’Driscoll, mkurugenzi mtendaji wa Lifeline, shirika la misaada nchini Australian linalotoa huduma ya usaidizi wa kuzuia visa vya watu kujitoa uhai.

Mtafuta riziki

Utafiti wa hivi karibuni Uingereza umeonyesha kwamba 42% ya wanaume wanahisi wanapswa kupata kipato kikubwa zaidi ya wake zao. Olumide Durojaiye ni mmoja wao.

Haki miliki ya pichaBBC SPORT

Image captionOlumide Durojaiye

“Babangu alikuwa mtafuta riziki, akifanya kazi usiku na mchana akisafiri kila mahali nchini na nilitamani kuwa kama yeye ” Olumide anasema. “Ilinibidi nitafute riziki kwasababu nilipaswa kuwa mwanamume ambaye mpenzi wangu anamuhitaji”.

Uzito wa jukumu la kifedha unaweza kuizidisha afya ya akili ya mtu yoyote kuzidi.

“Tunalelewa maisha yetu yte kujihukumu na vijana wenzetu na kuwana ufanisi kiuchumi ,” anasema Simon Gunning, mkuu wa kampeni ya kupambana na visa vya wanaume kujitoa uhai (Calm).

“Wakati tunaposhindwa kukabiliana na matatizo ya uchumi, hali inakuwa ngumu.”

Urembo wa kuvutia

Shinikizo la kutaka kuwa na muonekano mzuri ni kubwa kwa wanaume kama ilivyo kwa wanawake wengi wakiishia kufanyiwa upasuaji wa urembo ili kulifikia hilo.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Picha katika mitandao ya kijamii na vipindi katika televisheni zinatajwa na wataalamu kuwa ndio chanzo cha wanaume wengi kutaka kubadili umbo lao.

Hatahivyo bado kuna vizingiti katika kulizungumzia hili wazi kama ilivyo kwa wanawake na urembo jambo ambalo linazidi kuhatarisha wanaume kufanyiwa upasuaji visivyo.

Na zaidi kwa wanao kwenda katika mitandao ya kijamii na kuchunguza kliniki za bei nafuu zinazofanya upasuaji wa aina hii, mwisho wa kwisha wanahatarisha uzima au afya zao. (chanzo BBC)

Post a Comment

0 Comments